Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

LEGE nina Toyota Raum old model. Majuzi nilibadilisha alternator, fan na timing belts. Pia nilibadilisha oil filer, oil seals na kumwaga engine oil.
Baada ya hapo nikiweka reverse gear gari haidendi mpaka baada ya kukanyaga sana mafuta. Baade tena inachelewa kubadili gear na ikiwa kwenye silence inakuwa kama inataka kuzimika, wakati mwingine inazima kabia. Ila ikiwa kwenye parking inakuwa okay.
Geabox oil haijabadiishwa kwa muda mrefu kama miaka 4 hivi.
Tatizo ni nini?
 
Hivi hizi gari vw golf 5 diesel engine huwa huwa zina matatizo gani?
Sidhani kama kuna gari linakuja na shida moja kwa moja, eti kisa tu labda ni toleo fulani au ni brand fulani.
Uimara na ubora wa gari ni matunzo yako mwenyewe tu. Kama upo rafu hata uwe na Land Rover 109 utakuja tu kusema zina shida fulani.
Cha msingi fuata masharti yaloainishwa na gari husika.
Sio gari unapeleka kwa mafundi uchwara na kila kona lina fundi.
Au Oil inatumika hadi inatoka kama maji ya jaruba za mpunga! Au waweka oil uchwara. Kwa mfano: kwanini watu wanasema Nissan xtrail ni mbovu? Oil (Magumashi)+ATF (Magumshi)+Mafundi feki= lazima useme gari bovu.
Kimsingi VW ni gari zuri kama nawe utakuwa na nidhamu nalo kwa kufuata miongozo yake na kukiuka miiko.
 
wakuu naombeni msaada Gari yangu Subaru forestar Jana imeanza kutoa mvumo flani hiv kufuatilia nkagundua ni kwenye tairi nkapiga jeki nakawa nalichezesha tairi likawa linacheza cheza, tatizo litakuwa ni nini?
 
Wakuu naomba ushauri,
nataka kununua BMW 3 series, maneno ya watu yanatisha gharama kumantain pia ni ndoa huwez kuuza.....

Kwa uzoefu wenu imekaaje hii?
 
Inategemea unatumia oil za kilometers ngapi kuna 3000 5000 nk
IMG_20170707_223527_688.jpg
 
Wakuu naomba ushauri,
nataka kununua BMW 3 series, maneno ya watu yanatisha gharama kumantain pia ni ndoa huwez kuuza.....

Kwa uzoefu wenu imekaaje hii?
 
Naomba kujua kuhusu mazda tribute, zina matatizo gani, upatikanaji wa spare, gharama za spare na ulaji wa mafuta.
Mazda tribute ina share components na dada yake Ford Escape. Ila kwa uzoefu wangu, parts zake sio nyingi mtaani. Hasa body panels. Ulaji wa mafuta unategemea na engine utakayo chagua. Ila ile 2.0L inline 4 ulaji wake haupishani saana na rav4 ya same engine. (7 to 9km per litre kwa mjini) kutegemeana na matumizi yako.
 
Ni kweli mkuu fundi yupo sahihi.
Kwanza nianze kukulaumu na kuseme huo ni uzembe wa hali ya juu sana .

Kwa upande wangu hapo najua kitu ambacho kimeharibika ni valve lazima zitakuwa zimepinda ndio maana gari ina miss sana na hiyo pesa usilalamike wala sio nyingi kama ni jumla kwa kazi zote pamoja na garama ya kifundi.ina maana hapo lazima ufungue cyrinder head ubadili valve zilizo pinda,ubadili valve seal,cyrinder head gaskate,na kuifanyia service kbs.

Au kama vipi kanunue engine nyingine mswaki kama laki 7 au 8 hivi weka hapo..


Maana gx100 huwa inakuwa na kamiss flani hivi kanakera sana.hutokana na valve.
Kama engine inauzwa bei hiyo, ni bora anunue engine tuu.
 
Safari ndefu hiyo unayoizungumzia ni kutoka wapi mpaka wapi mkuu.

Na kama ni hivyo basi usihangaike sana mkuu nifahamuvyo mm unaweza ukatoka na gari from dar to mwanza kama iko powa haina shida na haiwezi chemsha labda kama kuwe na shida kwenye gari yako.labda cooling systerm haijakaa sawa.
Kweli kabisa. Na gari ikiwa kwenye highway ina cool kirahisi kuliko mjini.
 
Gari imeleta mushikeli kadri ninavyokanyaga accelerator ile gear box inapiga kelele kama vyuma vinapigana, awali iliwekwa ATF isiyo sahihi, baada ya kuiweka ATF sahihi mlio wa kelele umepungua kiasi lakini bado nahitaji msaada zaidi kujua nini kimeathirika na inatibikaje. Msaada tafadhali wandugu
Aise, hebu cheki level ya coolant. Kilishawahi nitokea kitu kama hicho.
 
Gari imeleta mushikeli kadri ninavyokanyaga accelerator ile gear box inapiga kelele kama vyuma vinapigana, awali iliwekwa ATF isiyo sahihi, baada ya kuiweka ATF sahihi mlio wa kelele umepungua kiasi lakini bado nahitaji msaada zaidi kujua nini kimeathirika na inatibikaje. Msaada tafadhali wandugu
Pia hakikisha ATF Level iko sawa as recommended by the manufacturer.
 
Pia hakikisha ATF Level iko sawa as recommended by the manufacturer.
asante kwa ushauri, iliwekwa BP 40 ATF badala ya DExtron A3 kwa sasa nilipata Dextron A1 angalau mlio unapotea kabisa yaani si sawa na awali maana ilikuwa hata mwingine aliye nje akidrive gari yake anasikia hio kelele. kwa sasa mlio umshuka zaidi, japo kuna miss nyingi licha ya kubadili spark na plug zake mpya origino za gari sahihi.

Sent from my XT1052 using JamiiForums mobile app
 
Acha uongo mkuu kama hujui bora kukaa kimyaa kuliko ukaongea na kusababisha hasara kwa mwomba ushauri
Ubarikiwe mkuu nilibaki kidogo tu niubebe ushari wake kilichonizuwia ni nasaha zako

Sent from my SM-G925F using JamiiForums mobile app
 
Shukrani maana kuna fundi ameniambia kuchek engine kwa computer nimpe 50 daahh tutalizwa sana tusiojua asante kwa Uzi huu
Mkuu shukuru mungu mimi nishapigwa elfu hamsini hiyo na tatizi halikuondoka

Sent from my SM-G925F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom