MADA: Fahamu kuhusu matumizi au ulaji wa mafuta kwenye gari aina ya Toyota harrier 3.0L (2990CC)

Chukua Suzuki Grand Vitara 2.7litre mana bei sawa tu na Vanguard
9c712bb64ea77410f6dad02db7858505.jpg
hii safi
 
Binafsi huwa nashauri mtu aangalie roho yake inataka nini na kama mfuko unaruhusu.
Kama una mfuko mwepesi hiyo gari itakuumiza, achana nayo. Tafuta cheaper options either yenye CC ndogo au model nyingine yenye CC ndogo.
Thank you so much mkuu Bavaria! Point taken!
 
Harrier 3.0L ina engine ya 1MZ VVTI ambayo pia ipo kwenye Kluger na magari mengine mengi.

Consumption ndugu bila kudanganya ni 5.5-6.5km/l kwenye urban areas, halafu inatembea 6.5 hadi 8 kwenye safari.

Gari hii unaweza fikisha 10-12km/l kama hautazidi speed 80 (yani speed 60,70-80) ukiwa safarini, lakini nachoweza kukwambia kwa nguvu ya engine na konfotabiliti yake huwezi heshimu mwendo huo na pia kwenye safari utachoka sana which means utajikuta unafall kwenye matumizi ya 6.5-8km per litre.

Asante
 
kama ni 3000cc hybrid chukua maana wese ni kama vits ila kama ni vvti kimbia, maana wese lake kwa mwaka unajenga apartent mbili unakula kodi yako ya 450000

What are you talking about?

Harrier Hybrid ina engine ya 2.5L 2AR - FE au 3.3L 3MZ FE Engine which means hizi engine zinasaidiwa na electric motor kuongeza nguvu ya gari kwa kupunguzia pistoni kazi ya ziada kwenye speed na matumizi mengine ya umeme.

Kwa hiyo naweza kusema Harrier Hybrid haina engine ya 3.0L mkuu, na kutokana na kuongezewa kifaa kingine kwenye efficiency (yani electric motor) basi imesaidia kupunguza matumizi ya mafuta though cylinder capacity inaonekana kubwa kwenye 3.3L. Unaweza kutembea 10-13km/l kwa urban areas na unaweza fika 15km/l kwenye safari mkuu ikiwa engine yako bado ni nzuri na haina shida.

Hybrid ni level nyingine mkuu ambayo naona kama jamaa atahitaji kuongeza budget yake tena.

Nasisitiza tena factory made harrier hybrid haina engine ya 3000cc
 
Ushauri wako ni upi kwa hizi harrier yenye less consumption
Ndio mkuu, Harrier hiyo 2.4 ni bora kidogo kwenye matumizi kuliko ile ya 3.0

Ina engine ya 2AZ ambayo unaikuta kwenye RAV4,Alphard,Kluger na magari mengineyo pia.

Gari hii inatumia km8 kwa litre maeneo ya mjini na foleni ila kwenye high way inatembea kilometer 10-11 kwa lita mkuu.

Angalizo kama ukitembea speed 70-80 kwenye high way unaweza ukasave mafuta sana yani consumption inaweza range kwenye km13-15 kwa lita mkuu kama hutakua na papara kwenye driving
 
Ulaji mbovu wa mafuta ya gari unategemea na vitu vifuatavyo
1.uendeshaji wako kaka wewe ni mzee wa kukamua unaingia road unanza kwa kukanyagia lazima wese liende.

2.foleni za magari epuka kutembea kwny foleni sehemu ya dakika tano unatumia nusu saa aheri upaki gari utafute tz 11 uendelee hapo mafuta yanaenda km umewasha jiko la mchina.

3.oxygen sensor nzima kama mbovu lazima unywewe mafuta kama mademu wanavyokunyeea vyabe bulee.

4.plug mbovu feki usitegemee plug za buku 6 zikawa nzuri itakula kwako mazima nunua plug za ukweli huna hela park gari.

5.tafuta sweet speed yako kwny highway unatulia na kubarizii siyo ukamue 150 utegemee tank lisiwe na matobo walau izizidi 120.

6.usiache madirisha wazi kwny highway garibinakuwa nzito na wese linaenda jingi.

7.kama ni ya petroli mara mojamoja weka petrol treatment inasafisha njia za mafuta na kurahisisha uchomaji wa haraka.

8.epuka safari fupi fupi na sisizo na tija uokoe mafuta. Ukishindwa yote haya na unakuwa kinga'angaanizi basi usisumbue watu kwa maswali nenda baa tafuta mchemso saafi wa gari lako.
 
Back
Top Bottom