geraldincredible
JF-Expert Member
- Mar 26, 2017
- 2,036
- 7,220
MKASA WA RAIS KICHAA
Miaka 11 iliyopita, mwanamuziki wa Reggae nchini Zambia, Maiko Zulu alitoa wimbo unaoitwa Mad President (Rais Kichaa). Wimbo huo ndiyo uliobeba jina la albamu yake aliyoitoa mwaka 2006.
Wimbo Mad President ulimwingiza Zulu kwenye matatizo ya kibiashara, kwani Shirika la Taifa la Utangazaji Zambia (ZNBC), lilikataa kuucheza wimbo huo, kwa maelezo kuwa ujumbe wake ulikuwa unamdhalilisha Rais wa taifa hilo kwa wakati huo, Levy Mwanawasa.
Alichokiimba Zulu kwenye wimbo Mad President ni kuwa Rais anakuwa kichaa kwa sababu ya mamlaka makubwa ambayo yupo nayo. Kwamba anateua na kufukuza kazi watu jinsi anavyojisikia. Anaweza kumpa mtu ajira na kumnyima amtakaye.
Zulu aliimba kuwa Rais anaweza kuamua kujipa mamlaka ya jaji na kutoa hukumu yeye mwenyewe. Rais anaweza kujifanya polisi na kumkamata amtakaye. Rais anaweza kujifanya mpelelezi na mwendesha mashtaka. Madaraka hayo makubwa ndiyo ambayo husababisha Rais awe kichaa.
Katika wimbo huo, Zulu hakutaja jina la Mwanawasa wala kiongozi yeyote ambaye alimlenga kufikisha ujumbe wake lakini lile jina la wimbo Mad President na kwa sababu Zambia, Rais alikuwa Mwanawasa, ilichukuliwa kuwa ndiye alikuwa mlengwa, hivyo kupata wakati mgumu kuchezwa na vyombo vya habari nchini humo.
Pamoja na kubaniwa kuchezwa, wimbo huo ulipata umaarufu mkubwa. Ujumbe ulipenya kwa sehemu kubwa. Ni kama ambavyo hutokea Tanzania, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA), wanapotangaza kuufungia wimbo, ndipo huupa umaarufu.
Kwamba Basata na TCRA wanapokataza wimbo fulani usichezwe, ni hapo huwafanya hata wale ambao siyo wapenzi wa muziki huutafuta ili wasikilize au kutazama kilichoonekana hakifai kimaadili na kufungiwa. Binadamu ameumbwa na malighafi ya umbea hasa kichwani!
Ni hiyo malighafi ya umbea kwenye kichwa cha binadamu, ndiyo ilifanya wimbo Mad President uwe maarufu sana nchini Zambia. Hata wasiopenda muziki, waliutafuta wasikilize kilichoimbwa na Maiko Zulu kwenye rekodi yake.
Wapo wasanii hutamani nyimbo zao ziingie kwenye migogoro na Serikali ili zipate umaarufu wa kibiashara. Mamlaka zinapaswa kutazama upya jinsi ya kudhibiti maudhui, vinginevyo zitaendelea kuwanufaisha wasanii kinyume na makusudio yao.
Copied mwandishi ni luqman maloto