Naomba nijibu mimi hili swali;
1. Nauli ya kwenda Zanzibar kwa Boat kwa daraja la mwisho kabisa (economy class) ni Tsh. 30,000/= na daraja la juu (Royal class) ni Tsh. 60,000/=
2. Vitu ambavyo ukinunua lazima ulipe kodi TRA ni vile unapokuwa na vitu vingi ambavyo kiuhalisia utaonekana unakwenda kufanya biashara na sio matumimizi binafsi. Halafu TV kuanzia juu ya Nchi 32 na Friji utapaswa kulipia kodi japo sio kubwa kivile.
3. Huku Zanzibar vifaa vya kutumia umeme bei yake ni nafuu kidogo tena vile used ndio kabisa ila vitu used muda mwingine ni kama kucheza kamari.
NB! Biashara ya ubuyu wa babu Issa kutoka Zanzibar inalipa sana huko Bara ukiwa na goli zuri tu.Naishi huku Zanzibar mkuu ukitaka kufanya biashara njoo utakuwa mgeni wangu nitakupitisha chocho zote.