Ndio maana tunajiuliza kwa uwezo gani iliokuwa nao Yanga hadi sisi Simba tufungwe mabao 5

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
438
1,752
Yaani kwa jinsi uwezo wa hii timu ulivo wa kiwango cha kawaida, tunashindwa kuamini kama kweli yale mabao 5 yalikuwa ni uwezo wa timu yao, ushahidi ni hizi mechi za ligi ya mabingwa ambazo zinaonyesha kabisa kuwa hii timu hata Mashujaa ina uwezo mzuri kuliko wao.

Hawana uwezo wowote Yanga, kinachowasaidia ni hiyo kutoa misaada kwa yatima basi lakini uwezo wa kusakata soka ni wa kiwango cha kawaida sana, hao akina Max mzengeli ambao hapa kwetu ligi ya NBC wanatambaa dimbani utadhan akina Ronaldinho au Jay Jay Okocha wa enzi hizo, huko ughaibuni hawana weupe kabisa yaani.

Wameua nyota za wachezaji wa Simba ili wazichukue wao, walienda hadi mlima kilimanjaro kushusha kibegi chetu na wakaweka chao, hili Simba liangalieni sana, kule mlima kilimanjaro mlipopeleka kibegi kama kudumisha mambo ya jadi injinja alienda kule akafika hadi kileleni, kile kibegi na mambo yefu tuliyoyaweka kule kileleni wameyashusha yote halafu wamepandisha bendera na mambo yao.

Simba inao wachezaji wazuri kuliko hao wa utopolo, wachezaji wao ndio hao hao Pacome, Aziz, Max, Yao basi, hamna kitu.

Yaani mpira huu ndio mlitufunga mabao 5 nyie, mpira huu ndio mtupige mabao 5, aisee wale wote mlioshiriki kuhakikisha tunafungwa mabao 5 na hawa Utopolo mbarikiwe sana.

Msimlaumu Gamondi, uwezo wa timu yenu ni ule ule wa uchale tu, mnafunga watu mabao 5 halafu mnaenda kutia aibu ugenini kwa vitimu vya kawaida tu.
 
Yanga ya 5G but imebaki mkiani kwa nini hizo 5G hazijawatoa mkiani nyie Uto wa mkiani wahed
Sasa kwa offside ya mchongo namna hii unatokaje chini kimsimamo wewe Kolokhamsa?
Screenshot_2023-12-08-21-46-34-15_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
5G bado inawatesa na hii ndio Yanga yenye mechi 2 za nyumbani.
Lazima itutese kwasababu haikutegemewa wala kuzaniwa kwa uwezo wa Yanga kuifunga Simba goli zote hizo tena ndani ya kipindi cha pili. Wachezaji wa Simba walikuwa kama misukule wasielewe wafanya nini au waamue nini. Kweli Yanga mnajua kuroga 🤣🤣🤣🙌
 
Lazima itutese kwasababu haikutegemewa wala kuzaniwa kwa uwezo wa Yanga kuifunga Simba goli zote hizo tena ndani ya kipindi cha pili. Wachezaji wa Simba walikuwa kama misukule wasielewe wafanya nini au waamue nini. Kweli Yanga mnajua kuroga 🤣🤣🤣🙌
Bado hamjasema.
 
Back
Top Bottom