Benchika hawezi kuleta mabadiliko kwenye timu iliyofungwa 5 kama Friends of Simba hawaungi mkono uongozi uliopo

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
438
1,752
Timu iliyofungwa mabao 5 na Yanga imemleta Benchika, kocha ambaye unapotaja makocha 10 bora afrika na yeye yumo.

Benchika ana mbinu na uwezo wa kuwafurahisha wale waliokufa mabao 5 na kurudisha furaha.

Wachezaji wa timu iliyofungwa migoli 5 na Yanga ni wazuri na wana uwezo mkubwa sana.

Mtu yeyote anayesema kuwa wachezaji wa timu iliyofungwa mabao 5 ni wazee, cjui hawana kasi, hawajitumi, cjui wameuza mechi ni uongo, uongo na wanajificha kwenye kichaka.

Sisi tunaoijua hii timu mambo ya kutuhumu wachezaji pale inapofungwa hayakuanza leo.Akina Kaniki, Shekhan, Machupa, marehemu Athuman Machepe, emannuel Gabriel, Kaseja washakula sana adhabu kuwa wameuza mechi na kuitwa maduka.

Enzi hizo machawa akina Kisugu walikuwa uzaramoni huko wanauza nazi, eti leo ndio wanaonekana mainfluencer ndani ya timu.Very funny.

Benchika amekuja na benchi lake, hata hivyo hatoweza kuibadilisha hii timu na mwaka huu Yanga anakwenda kubeba tena ndoo kwa mara ya tatu mfululizo.Azam watashika nafasi ya pili msimu huu maana gari limeshachanganya tayari.

Benchika ni mwarabu, waarabu wana tabia ya hasira na kususa, anasema asipangiwe kikosi hivi siku mkicheza na yanga akamweka golini Ayubu, kulia Jimmson mwanuke, kushoto Israel, nne Kennedy na sentahafu Kazi, sita Mzamiru, winga Onana, winga Kibu, nane Kanoute, tisa Bocco kumi Baleke.Mtamwelewa kweli nyie? Hata kama wachezaji hao wanajituma kiasi gani wana uwezo wa kuikabili Yanga hii ya Pacome Zuzu?

Benchika, nisikilize, Hiyo timu uliyopewa ina migogoro ya kiuongozi, friends of Simba hawana ushirikiano na uongozi wa Mangungu, uongozi unapanga mikakati wenzao wanapangua mikakati na kwa sababu wanaijua timu A to Z, wanajua mipango ya timu A to Z, inakuwa rahisi kupigisha shoti.

Kiongozi wa timu hiyo iliyopigwa matano anakusudia kugombea ubunge jimbo la kilwa kaskazini mwaka 2025, akisema ajiuzulu leo kisiasa ataharibikiwa, hivyo hawezi kuachia uongozi kizembe, anajua madhara yake kisiasa.

Na hii Yanga ninavoiona na mikakati yao ilivyo mizito kwa wataalamu wao wa nje ya uwanja hasa kule Zanzibar na Pemba, nawahakikishia mechi ijayo mnakula kama sio 8 basi 10.Safari ijayo ndio mtakufa kabisaaaaaaaaaaa.

Njia pekee iliyobakia sasa hivi ni kuwapa timu friends of Simba otherwise sioni mabadiliko yoyote ndani ya timu, mkiendelea kushikia bango kuwa hamuwataki timu iliyofungwa mabao 5 haiwezi kufika mahali popote, mnapoteza muda wenu.

Hizi mbwembwe za Ahmed Ally leo kuwa timu imepata kocha cjui mara cjui sasa wapinzani mtakoma ni ujinga wa kiwango cha chuo kikuu.Tusubiri tuone.
 
Screenshot_20231128-212514.jpg
 
Back
Top Bottom