Elections 2010 Machozi ya samaki huenda na maji, machozi ya mtu kamwe.......

MovingForward

JF-Expert Member
Nov 10, 2009
489
49
Kuna msemo usemao kilio cha samaki machozi huenda na maji. Lakini ni tofauti kwa machozi ya binadamu........ Hata kama mwehu atafariki leo kwa namna yoyote ile, ni lazima watatokea watu watambue kwamba hapa mwehu amefariki.

Kilio cha Watanzania juu ya vyombo vyetu vya usalama, hayawezi kwenda na maji.

Malalamiko juu ya POLICE na Usalama wa taifa juu ya uhusikaji wao katika kuvuruga uchaguzi yamesikika katika ardhi yetu na taifa letu kwa ujumla wake. Kilio chake, hakiwezi kwenda na maji, ni lazima kitasikika tu mbele za Mungu.

Kuna wakati ambapo vyombo vyetu vya usalama vinatakiwa kuketi chini na kujiuliza vinafanya haya yote kwa maslahi ya nani???. Matatizo yanayotukabili katika taifa letu nao hawawezi kuyakwepa yanawahusu. isitoshe wao ndio wanaoumia sana!!. Pale wanapotumika vibaya, kwa kweli wafike mahali watambue kwamba wanajimaliza wao wenyewe.

Matumizi ya nguvu mahali pasipotakiwa na uhujumu wa uchaguzi ni vitu ambavyo machozi yake hayawezi kuisha hivi hivi. Vyombo vyetu vya usalama kuendelea kukumbatia tabaka la watu wachache kwa manufaa ya hao wa chache ni kuendelea kusindika baruti ndani ya chombo cha kulipulia mwamba mugumu. Vyombo vya usalama ndivyo vitakuwa ni chimbuko la kuleta machafuko ndani ya nchi yetu kwa kuwa vinakiuka misingi iliyoviweka vyombo hivyo. Ipo siku ambayo ghadhabu ya Mungu itafurika na kujaa pomoni, na matokeo yake tutayaona.

Yafuatayo yataanza kutokea kwa sababu ya dhuruma ya vyombo vyetu vya usalama:
(i) Fitina miongoni mwa watu ndugu walio na itikadi tofauti za kisiasa, kwa vile tu haki haikutendeka

(ii) Mgawanyiko miongoni mwa vyombo vyenyewe vya usalama kwa vile si wote watakaoendelea kukubaliana na mwenendo mbaya ya vyombo vya usalama.- Mkumbukeni Deo Mwanyika, MD wa Barrick North Mara, hivi karibuni, alisema "Kama mtanzania mzalendo, ninaona serikali haijaweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kwamba tunanufaika na madini". Huyo ni mzalendo aliyekaa mahali anapolipwa vizuri lakini sauti yake ilitoka hivyo katika TV taarifa ilipokuwa ikitolewa. Wapo wengi ndani ya vyombo vyetu vya usalama ambao hawapendi tabaka la wachache ndani ya vyombo vyetu vya usalama kuendelea na michezo michafu na ya hatari kwa taifa letu.

(iii) Ulinzi shirikishi, kwa maana ya POLICE Jamii, utaanza kudhorota kwa vile wananchi wameonyeshwa kwamba POLICE wenyewe na vyombo vya uslama wanahusika katika uharifu.

(iv) Utendaji wa wale walioshinda kwa wizi utakuwa si mzuri kwa vile dhamira zitakuwa zikiwasuta kwamba wameingia madarakani kwa uhuni. Isitoshe tutaongeza gharama za matibabu kwa serikali kwa sababu wengi watakuwa wakipata magonjwa ya mioyo, kwa kufanya kazi kwa wasiwasi na kutokujiamini. Hawa watakaoendelea kuumwa ndio watakuwa wakitumia rasirimali zetu kwenda kujitibia nje ya nchi.

(v) Tutaanza kushuhudia vifo vya watu wengi, wakiwemo viongozi wa ngazi za juu kwa presha zinazotokana na kudhurumiana maslahi ya dhuruma. Wanapoitafuna nchi, watatokea kudhurumiana na hapo ndipo watazidi kujenga chuki miongoni mwao. Viongozi walafi wataiongia madarakani kwa wizi, lakini ulafi utawatokea puani, na hapo ndipo vifo vitakapo wakumba kama nzige wavamiapo shamba.

kumbuka maneno haya: Tamaa ikichukua mimba huzaa dhambi na dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.

machozi ya Watanzania, hayawezi kwenda na maji. Machozi ya samaki wa Magufuli yalikwenda na maji, lakini ya Watanzania, yatakwenda na mtu mwovu..........
 
Back
Top Bottom