Macho ya Bundi

ILIPOISHIA Salome alishangaa, “Au jana aligundua nimeona kitu kinachopumua sandukuni mwake?” alimuuliza mwenzake. SASA ENDELEA... Mei hakunijibu haraka swali hilo. Alinitazama kwa sekunde chache, tukaendelea kupata kifungua kinywa. Baada ya kumeza funda moja la chai alinijibu: “Siyo kwamba aligundua jambo, anasema ulimuudhi, inawezekana kuna kitu alikuambia nawe ukakataa.” “Kama ulikuwepo. Aliniambia ana jambo anataka kuniambia akataka turudi chumbani mimi nilimkatalia.” “Basi kama ni hivyo ni bora tungoje nini atashuka nacho kutoka huko ghorofani.” Hakuchukua muda mrefu Chinchi alishuka akiwa na kifurushi mkononi. Nilihisi kile kifurushi kile ndicho kilichokuwa kwenye sanduku kikipumua. Chinchi baada ya kufika kwenye meza yetu alikiweka juu kikawa kinaendelea kuonekana kana kwamba ndani kuna kitu kinapumua. “Salome hii ni zawadi yako,” alisema Chinchi. Sikutabasamu wala kuifurahia zawadi hiyo kwa kuwa sikuwa najua nini kilichowekwa, tena basi kinachopumua. Niliogopa hata kukishika kifurushi hicho. “Mbona unaonekana kutofurahia hii zawadi.” “Sijui ni zawadi gani, naiogopa, mbona kuna kitu kama vile kinapumua humu ndani na kwa nini unizawadie.” “Sikiliza Salome. Usiwe na wasiwasi, kwani kitu kibaya naweza kukupa tena mbele ya watu namna hii?” Alichukua kile kifurushi na kukifungua. Mimi na rafiki yangu Mei tukiwa tunatumbua macho kukiangalia. Mimi na rafiki yangu tuliangua kicheko baada ya kukiona kilichokuwemo ndani ya kifurushi. “Mbona mmecheka sana, au zawadi hii ziyo nzuri?” Niliishuhudia saa nzuri sana ambayo ilikuwa ina umaridadi wa hali ya juu. Ilikuwa imetengenezwa mfano wa tumbo na kila dakika zinapogonga, tumbo lilikuwa likifutuka kana kwamba inapumua. Baada ya kumshukuru aliniambia ameniita kwa nia moja tu, kwamba anataka kunioa. “Hujawahi kuwa na mke katika maisha yako?” “Sijawahi.” * * * Tulioana na Chinchi. Ndoa ilikuwa ya kifahari kutokana na uwezo mkubwa wa kifedha aliokuwa nao. Baada ya ndoa nilimshauri mume wangu twende tukamtembelee Mei nyumbani kwake, akakubaliana nami. Alinisindikiza hadi nyumbani kwa rafiki yangu huyo. Kiumri Mei alikuwa mkubwa kuliko mimi japokuwa tulikuwa marafiki sana. Mwenzangu tayari alikuwa na binti wa kike aliyekuwa anasoma kidato cha pili anayeitwa Pili, mimi nilikuwa bado sijazaa. Karibu na nyumbani kwangu kulikuwa na jirani yetu ambaye alikuwa anaitwa mama Koki, siku moja alipofika kwangu nikasikia mtu anagonga mlango kwa nguvu. “Karibu, mama Koki.” “Sijui utanielewaje, nimeona nikuambie ujue la kufanya.Una kifua shoga?” “Niambie tu mama Koki.” Mama Koki alinyamaza kwa muda akaniambia kuwa jambo analotaka kuniambia ni zito. “Sikiliza Salome. Kuna msichana ulinifahamisha siku moja kuwa anaitwa Pili na ni mtoto wa rafiki yako Mei. Huwa anakuja hapa kwako mara kwa mara kila unapokuwa umeenda kazini. Anamkuta mumeo tu,” mama Koki alinyamaza akaniangalia. “Huyu binti nina wasiwasi naye, atakuvunjia ndoa yako. Fanya uchunguzi.” Machozi yalinitoka na kujiuliza kweli mtoto wa Mei anaweza kuniingilia katika ndoa yangu? Nilichanganyikiwa.



Itaendelea
 
Feb 12 ILIPOISHIA “Sikiliza Salome. Kuna msichana ulinifahamisha siku moja kuwa anaitwa Pili na ni mtoto wa rafiki yako Mei. Huwa anakuja hapa nyumbani kwako mara kwa mara kila unapokuwa umekwenda kazini. Anamkuta mumeo tu,” mama Koki alinyamaza akaniangalia. “Huyu binti nina wasiwasi naye, atakuvunjia ndoa yako. Fanya uchunguzi.” Machozi yalinitoka na kujiuliza kweli mtoto wa Mei anaweza kuniingilia katika ndoa yangu? Nilichanganyikiwa. SONGA NAYO... Mama Koki hakukaa sana baada ya kutoa taarifa aliyokuwa ameniletea lakini aliniachia mawazo tele kichwani mwangu nikawa najiuliza hili na lile bila kupata jibu. ‘Haya aliyoniambia huyu mama ni kweli au anataka kunigombanisha na rafiki yangu?’ Wakati naendelea kuwaza hayo nilisikia mngurumo wa gari nikajua kwamba ni mume wangu Chinchi anarudi. Alipoingia sebuleni alinikuta nikiwa nimelala kwenye sofa la watu watatu. Sikuinuka kumpokea. “Leo unaumwa?” aliniuliza. Nilijishitukia machozi yakitiririka kwa hasira na niliendelea kuwa kimya. “Nakuuliza Salome, una nini leo?” “Najisikia naumwa sana kichwa,” nilimdanganya. “Umeanza kuumwa saa ngapi?” “Siyo muda mrefu. Mchana.” “Twende hospitali.” “Hapana, nimekunywa dawa ya kutuliza maumivu na tangu ninywe naona kuna nafuu,” nilimdanganya. “Umekula chakula chochote?” “Baada ya kula ndipo nilianza kusikia kichwa kikinigonga.” “Ni vyema kama tutakwenda hospitali wakaangalie vipimo mke wangu.” Nilimsisitizia kuwa tusubiri kwa kuwa nimemeza vidonge na kama nitaona hali inazidi kuwa mbaya nitamuambia. Aliniaga kwamba anakwenda kumuona rafiki yake mmoja ambaye alikuwa na ahadi naye kuhusiana na shughuli za kibiashara. Nilimruhusu kuondoka lakini moyoni mwangu nikiwa na wasiwasi mkubwa kwamba inawezekana anakwenda kukutana na Pili, mtoto wa rafiki yangu Mei. Saa mbili usiku mume wangu alirudi nyumbani akiwa hana raha kabisa. Nilijiuliza maswali mengi lakini nikaamini inawezekana hali ile amekuwa nayo kutokana na mimi kuumwa mchana kutwa. Wakati anaingia nilikuwa nipo chumbani kwetu. Nilitoka kwenda kumuandalia chakula. Alikaa kama dakika kumi bila kunyanyuka kitini na kwenda kwenye meza ya chakula. Alionekana wazi kwamba ana jambo rohoni. “Vipi dia, kwani nawe unaumwa kama mimi?” Nilimtupia swali la mtego. “Na mimi najisikia kama vile nina homa.” Niliinuka na kwenda kugusa shavu lake kupima kama ana joto au la. Nililikuta shavu baridi kabisa wala dalili za homa hazikuwepo. “Lakini unaonyesha huna homa kabisa, sijui unajisikiaje?” nilimuuliza. “Najisikia mapigo ya moyo kuongezeka sana.” “Kwa nini au umepoteza fedha nyingi huko ulikokwenda?” “Hapana.” “Sasa nini kinakuumiza mume wangu.” “Basi nadhani mwili tu umekataa leo.” “Basi inuka tukapate chakula.” Nilimuinua na kwenda naye moja kwa moja kwenye meza ya chakula. Nilikuwa nimeandaa ugali na nyama ya kuku wa kuchoma. Nikaandaa mezani. Tulianza kula huku kila mmoja akiwaza lake kichwani. Mimi nilikuwa namuwaza Pili mtoto wa rafiki yangu Mei. Nilikuwa siamini kama anaweza kunifanyia unyama wa aina ile. Haukupita muda mrefu alikuja rafiki yake mume wangu ambaye sikutarajia kama angefika wakati ule. Lakini ajabu ni kwamba badala ya kuzungumza pale sebuleni, walitoka nje kabisa ya nyumba na wakawa wanazungumza kwa kunong'ona




Itaelea mwakani
 
Kwani hadithi inasimuliwa na watu wangapi? Aaaah...!

Mi nasubiri aje Mzizi Mkavu asimulie ya huyo mwingine wala sijaisoma..!
 
Last edited by a moderator:

Hiyo ITALLIC ni kuweka msisitizo kuwa unaanza KUTUTEKA:smile-big:Maana inabidi sasa tuwe macho wazi muda wote kufuatilia muendelezo wa hadithi hii!!!! Haya LIKE yangu nimeiweka kwa maandishi kabisa....Nasubiri muendelezo Mkuu
 
Wanaweka afu wanachomoa aah wanatukatisha utam ujue ! Jukwaa linamambo! Ngja nivute kiti nkae labda itakuja teena!
 
Macho ya Bundi - 3-

ILIPOISHIA
Salome alishangaa, “Au jana aligundua nimeona kitu kinachopumua sandukuni mwake?” alimuuliza mwenzake.
SASA ENDELEA...


Mei hakunijibu haraka swali hilo. Alinitazama kwa sekunde chache, tukaendelea kupata kifungua kinywa.
Baada ya kumeza funda moja la chai alinijibu:
“Siyo kwamba aligundua jambo, anasema ulimuudhi, inawezekana kuna kitu alikuambia nawe ukakataa.”
“Kama ulikuwepo. Aliniambia ana jambo anataka kuniambia akataka turudi chumbani mimi nilimkatalia.”
“Basi kama ni hivyo ni bora tungoje nini atashuka nacho kutoka huko ghorofani.”
Hakuchukua muda mrefu Chinchi alishuka akiwa na kifurushi mkononi. Nilihisi kile kifurushi kile ndicho kilichokuwa kwenye sanduku kikipumua.
Chinchi baada ya kufika kwenye meza yetu alikiweka juu kikawa kinaendelea kuonekana kana kwamba ndani kuna kitu kinapumua.
“Salome hii ni zawadi yako,” alisema Chinchi.
Sikutabasamu wala kuifurahia zawadi hiyo kwa kuwa sikuwa najua nini kilichowekwa, tena basi kinachopumua.
Niliogopa hata kukishika kifurushi hicho.
“Mbona unaonekana kutofurahia hii zawadi.”
“Sijui ni zawadi gani, naiogopa, mbona kuna kitu kama vile kinapumua humu ndani na kwa nini unizawadie.”
“Sikiliza Salome. Usiwe na wasiwasi, kwani kitu kibaya naweza kukupa tena mbele ya watu namna hii?”
Alichukua kile kifurushi na kukifungua. Mimi na rafiki yangu Mei tukiwa tunatumbua macho kukiangalia.
Mimi na rafiki yangu tuliangua kicheko baada ya kukiona kilichokuwemo ndani ya kifurushi.
“Mbona mmecheka sana, au zawadi hii ziyo nzuri?”
Niliishuhudia saa nzuri sana ambayo ilikuwa ina umaridadi wa hali ya juu. Ilikuwa imetengenezwa mfano wa tumbo na kila dakika zinapogonga, tumbo lilikuwa likifutuka kana kwamba inapumua.
Baada ya kumshukuru aliniambia ameniita kwa nia moja tu, kwamba anataka kunioa. “Hujawahi kuwa na mke katika maisha yako?”
“Sijawahi.”
* * *
Tulioana na Chinchi. Ndoa ilikuwa ya kifahari kutokana na uwezo mkubwa wa kifedha aliokuwa nao.
Baada ya ndoa nilimshauri mume wangu twende tukamtembelee Mei nyumbani kwake, akakubaliana nami. Alinisindikiza hadi nyumbani kwa rafiki yangu huyo.
Kiumri Mei alikuwa mkubwa kuliko mimi japokuwa tulikuwa marafiki sana. Mwenzangu tayari alikuwa na binti wa kike aliyekuwa anasoma kidato cha pili anayeitwa Pili, mimi nilikuwa bado sijazaa.
Karibu na nyumbani kwangu kulikuwa na jirani yetu ambaye alikuwa anaitwa mama Koki, siku moja alipofika kwangu nikasikia mtu anagonga mlango kwa nguvu.
“Karibu, mama Koki.”
“Sijui utanielewaje, nimeona nikuambie ujue la kufanya.Una kifua shoga?”
“Niambie tu mama Koki.”
Mama Koki alinyamaza kwa muda akaniambia kuwa jambo analotaka kuniambia ni zito.
“Sikiliza Salome. Kuna msichana ulinifahamisha siku moja kuwa anaitwa Pili na ni mtoto wa rafiki yako Mei. Huwa anakuja hapa kwako mara kwa mara kila unapokuwa umeenda kazini. Anamkuta mumeo tu,” mama Koki alinyamaza akaniangalia.
“Huyu binti nina wasiwasi naye, atakuvunjia ndoa yako. Fanya uchunguzi.”
Machozi yalinitoka na kujiuliza kweli mtoto wa Mei anaweza kuniingilia katika ndoa yangu? Nilichanganyikiwa.



Je, Salome atamfanya nini mtoto wa rafiki yake? Tukutane baadae ................
 
Mwakani ujifunze basi kuweka na paragraphs
 
Macho ya Bundi - 4-


ILIPOISHIA

“Sikiliza Salome. Kuna msichana ulinifahamisha siku moja kuwa anaitwa Pili na ni mtoto wa
rafiki yako Mei. Huwa anakuja hapa nyumbani kwako mara kwa mara kila unapokuwa umekwenda kazini. Anamkuta mumeo tu,” mama Koki alinyamaza akaniangalia.

“Huyu binti nina wasiwasi naye, atakuvunjia ndoa yako. Fanya uchunguzi.”
Machozi yalinitoka na kujiuliza kweli mtoto wa Mei anaweza kuniingilia katika ndoa yangu?
Nilichanganyikiwa.

SONGA NAYO...


Mama Koki hakukaa sana baada ya kutoa taarifa aliyokuwa ameniletea lakini aliniachia mawazo tele kichwani mwangu nikawa najiuliza hili na lile bila kupata jibu.
‘Haya aliyoniambia huyu mama ni kweli au anataka kunigombanisha na rafiki yangu?’
Wakati naendelea kuwaza hayo nilisikia mngurumo wa gari nikajua kwamba ni mume wangu Chinchi anarudi.
Alipoingia sebuleni alinikuta nikiwa nimelala kwenye sofa la watu watatu. Sikuinuka kumpokea.
“Leo unaumwa?” aliniuliza. Nilijishitukia machozi yakitiririka kwa hasira na niliendelea kuwa kimya.
“Nakuuliza Salome, una nini leo?”
“Najisikia naumwa sana kichwa,” nilimdanganya.
“Umeanza kuumwa saa ngapi?”
“Siyo muda mrefu. Mchana.”
“Twende hospitali.”
“Hapana, nimekunywa dawa ya kutuliza maumivu na tangu ninywe naona kuna nafuu,” nilimdanganya.
“Umekula chakula chochote?”
“Baada ya kula ndipo nilianza kusikia kichwa kikinigonga.”
“Ni vyema kama tutakwenda hospitali wakaangalie vipimo mke wangu.”
Nilimsisitizia kuwa tusubiri kwa kuwa nimemeza vidonge na kama nitaona hali inazidi kuwa mbaya nitamuambia.
Aliniaga kwamba anakwenda kumuona rafiki yake mmoja ambaye alikuwa na ahadi naye kuhusiana na shughuli za kibiashara.
Nilimruhusu kuondoka lakini moyoni mwangu nikiwa na wasiwasi mkubwa kwamba inawezekana anakwenda kukutana na Pili, mtoto wa rafiki yangu Mei.
Saa mbili usiku mume wangu alirudi nyumbani akiwa hana raha kabisa.
Nilijiuliza maswali mengi lakini nikaamini inawezekana hali ile amekuwa nayo kutokana na mimi kuumwa mchana kutwa.
Wakati anaingia nilikuwa nipo chumbani kwetu. Nilitoka kwenda kumuandalia chakula.
Alikaa kama dakika kumi bila kunyanyuka kitini na kwenda kwenye meza ya chakula. Alionekana wazi kwamba ana jambo rohoni.
“Vipi dia, kwani nawe unaumwa kama mimi?” Nilimtupia swali la mtego.
“Na mimi najisikia kama vile nina homa.”
Niliinuka na kwenda kugusa shavu lake kupima kama ana joto au la. Nililikuta shavu baridi kabisa wala dalili za homa hazikuwepo.
“Lakini unaonyesha huna homa kabisa, sijui unajisikiaje?” nilimuuliza.
“Najisikia mapigo ya moyo kuongezeka sana.”
“Kwa nini au umepoteza fedha nyingi huko ulikokwenda?”
“Hapana.”
“Sasa nini kinakuumiza mume wangu.”
“Basi nadhani mwili tu umekataa leo.”
“Basi inuka tukapate chakula.” Nilimuinua na kwenda naye moja kwa moja kwenye meza ya chakula.
Nilikuwa nimeandaa ugali na nyama ya kuku wa kuchoma. Nikaandaa mezani.
Tulianza kula huku kila mmoja akiwaza lake kichwani. Mimi nilikuwa namuwaza Pili mtoto wa rafiki yangu Mei. Nilikuwa siamini kama anaweza kunifanyia unyama wa aina ile.
Haukupita muda mrefu alikuja rafiki yake mume wangu ambaye sikutarajia kama angefika wakati ule. Lakini ajabu ni kwamba badala ya kuzungumza pale sebuleni, walitoka nje kabisa ya nyumba na wakawa wanazungumza kwa kunong’ona.


Itaendelea baadae ............................
 
Dah! utamu unakuja halafu unakataaaa, endeleaaaa sasa...................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…