Revolutionary
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 456
- 86
go to hell....vizimba ni one square meter. Labda wauze karanga na vitumbua. What are you talking about dude!!!!
Watu wasipotoshe dhumuni la kujengwa majengo yale . ni lengo zuri na daima ni mfano wa kuigwa .
lakini wakitaka ufanisi wa majengo haya ni lazima wayaamishe makaburi pembeni yake na wajenge kituo cha mabasi ya daladala yaendayo mbagala na gongo la mboto nadhani wataona idadi ya watu itavyoongezeka masokoni pale
Wanajamii nina yafuatayo:
1. Mradi wa Majengo ya Machinga Complex ni failure tupu kweli kwa kuwa " wateja wa wamanchinga wako mitaani. Ni kweli kabisa ulibuniwa kwa maslahi binafsi na sio kwa WAMACHINGA. Ushirikishwaji wa wadau ni muhimu sana. Matokeo yake ni kujenga "White Elephants" za miaka ya 70 na 80. Miradi ya kutokana na hotuba za majukwaa; angalia viwanja vya michezo isiyomalizika kila mkoa. Imegeuzwa kuwa viwanja vya maonyesho!
2. Wateja wa Manchinga ni watu wa kipato cha chini wenye kutegemea daladala, baiskeli, miguu yao na wachache bodaboda ili wafike kwenye masoko. Hivyo "location" ya soko la Machinga sio kwa ajili ya biashsara ndogo ndogo za wamachinga. Usitarajie mtu anayetaka kununua suruali au shati la mtumba la sh. 500. 00 au 1,000.00 kutoka Buguruni, Tabata, Tandika au Tegeta apande daladala mpaka Ilala. Kwa mwenye uwezo wa kufikiri wa kati ni HAIWEZEKANI. Binafsi zaidi ya nguo zangu ni mitumba mipya au karibia mipya hununua maeneo ya mitaa yangu. Situmii nauli yeyote. Na ndio wengi wa watu wa kipato cha chini na cha kati.
3. Ujenzi wa Machinga Complex ulipingana na dhana nzima ya kutanua jiji la Dar kwa kujenga miji midogo ya pembezoni - "satellite cities" za Kibamba - Uluguruni, Pugu, Bunju, Kigamboni na sehemu zingine ili kuhudumia wakaazi wa maeneo hayo badala ya kwenda Ilala.
4. Nini kifanyike? Nakubaliana na na wazo la kuwakabidhi majengo hayo wafanyabiashara wa kati na wakubwa wenye uwezo wa kulipa kodi za pango na kuhudumia usafi wa majengo hayo. Wateje wake ni wenye kumudu kupanda daladala na wenye vipando vyao. Sio wanunjua chupi, soksi na sidiria za mitumba kutoka Marekani na Canada. Mamlaka za Halamshauri za Manispaa husika zikabidhiwe majengo hayo ili waweze kupangisha kwa wahusika na sio Wamanchinga! Na sio Halmashauri ya JIJI. Halmashauri ya JIJI haina walipa kodi wala wapiga kura. Wapo Ilala, Kinondoni na Temeke. Fedha zitakazopatikana zipelekwe kujenga masoka mazuri na madogo kwenye maeneo ya miji mipya ya pembezoni mwa jiji -satellite cities". Iwapo kungekuwa na ushirikishwaji sasa hivi tungekuwa na masoko ya aina hii zaidi ya matano kama yalivyo maghorofa ya Manchinga.
5. Kukusanya wadau husika sio rahisi na ni gharama. Tutumie wataalamu wetu kikamilifu wafanye kazi za kupanga maendeleo ya JIJI letu na sio WANASIASA! Tuwatumie maafisa maendeleo ya jamii (sociologists), wachumi, maafisa mipango miji (town planners), madaktari, wanamazingira na kadhalika. Wanasiasa watoe mapendekezo tu!
Akhsanteni!

CCM haina nia ya dhati ya kumkomboa Mtz ndio maana hata miradi inayobuni ni ya kitapeli.
Nssf wametumia mamilioni ya pensheni za watu kwenye mradi wa kijinga.
Jengo lenyewe limejengwa chini ya kiwango, saa hizi nyufa kila kona.
Waambie mzee! Hata UDOM nyufa kibao!