Mzizi mkavu wapi mkuu?
Mzizi mkavu wapi mkuu?
Nilisoma hiyo kitu nikaishia kucheka sana. Jamaa wanaeleza vizuri kuwa ni simple electrophoresis ya kidato cha tatu. Na changes kwenye maji zinatokana redox reactions za iron.Baabu Dark City nimesoma i see. So this is another utapeli wa kutuibia wadanganyika.Ndo maana nilikuwa sielewi mechanism yake, SIDANGANYIKI
Nilisoma hiyo kitu nikaishia kucheka sana. Jamaa wanaeleza vizuri kuwa ni simple electrophoresis ya kidato cha tatu. Na changes kwenye maji zinatokana redox reactions za iron.
Nina hakika siku za nyuma First Lady mtarajiwa Josephine nilikuwa namuona kwenye moja ya Tv station moja anaelezea jinsi ya matibabu ya hicho kifaa kwa ufasaha kabisa akiwa kama mtaalamu wa tiba mbadala kwenye cliniki yake
So kama vipi check naye yupo humu JF anaweza kukupa dondoo
jamani nimetolewa sumu kwa mashine hyo lakini ainipi akilini mwangu kabisa unafungwa belt kiunoni karibia na kitovu, alafu unatumbuliza miguu kwenye karai la maji wanaweka na chumvi eti inasaidia kuzibua matundu kwenye nyayo kisha wanatumbukiza kidude fulani kwenye maji ambacho kinachemka uku belt ulowekewa tumboni inapata joto la wastani wanasema eti ndio inalainisha sumu kweli nilimaliza nusu saa na maji yalibadilika rangi kiasi hofu yangu nahisi kile kidude wanachoweka kwenye maji ndicho kinachotengeneza huo uchafu unaoitwa sumu kwani kinavyochemka ndivyo maji yanavyobadilika na uchafu autoki miguuni kwako nilipouliza nikajibiwa hicho ndio kinavuta sumu
Nina shemeji yangu huko Bk nae alifanyiwa hii kitu. Alikuwa nauzito, na moyo ulikuwa unamuuma, kichwa. Wakamwambia the same thing kuwa ana sumu mwilini akaekewa mashine hiyo sumu ikatoka ktk karai as usual. Kwa madai yake amepona kabisa, anajisikia mwepesi, moyo hauumi, kitambi kimepungua na ameloose weight
Sasa najuliza je? hii treatment inaenda na imani? Nilivyoelewa nilishinwa kuelewa na hadi sasa sijaelewa bado.
Yaani ni chemistry babu, kabisaa. Eleectrolysis bila ubishi babu DC.
Kweli watanzania tunaibiwa sana, and it seems wengi tu wagonjwa so kila matibabu yanayokuja, bila hata kufikiri tunakuwa trapped nayo. Hata kufanya reseach kidogo tu.
Itakuwa unatania, First Lady mtarajiwa nae ni tapeli?!
Mkuu siriazi kabisa nilimuona kwa macho yangu akiitangaza tiba hiyo kama sikosei ilikuwa TBC akaelezea kwa ufasaha na alikuwepo mteja akweka miguu kunako maji na akafungwa mkanda fulani kisha yale maji yakaanza kugeuka rangi kama nyekundu/ugoro fulani hivi eti hiyo ndio sumu inatoka
Kama namsingizia Josephine first lady mtarajiwa aje akanushe hapa
Umesahau babu wa loliondo?
Kuna kaka alikuwa na kansa ya damu, alienda na ambulance. Akarudi kaketi poa kabisa. Alikuja kufa baadae lakini for a while alienda na kazini na kuwa fine. Achana na imani aisee!
Sorry Koku,
Ni electrolysis na siyo electrophoresis kama nilivyosema awali.
Kwa kuwa maji yanakuwa na chumvi, hiyo inayafanya kuwa conductor ya umeme kutoka electrode moja kwenda nyingine. Hizo changes jamaa wanazosema zinaweza kuwa ni reaction kwenye electrodes au Iron iliyoko kwenye maji. Kwa hiyo changes kutoka Fe2+ to Fe3+ zinasababisha brown colour inayoonekana kwenye maji na ndiyo wanaita sumu.
Ila kuna jamaa alijaribu kutetea kwamba electric potential ya cells (umeme mdogo sana wa kwenye chembe hai za mwili) ndiyo unayosababisha sumu itoke. Hata hivyo, hilo haliwezekani kwa sababu hakuna ushahidi wa kutiririka kwa solutions kutoka kwenye cell cytoplasm kwenda kwenye yale maji. Pia ilionekana kuwa ukitumia pure water, hutaona hizo changes!!
Ila wabongo ukiwaeleza haya watakuona wewe ndo chizi kama walivyotufanya kwenye issue ya Babu wa Loliondo na DECI!
Babu DC!!