Machimbo ya dhahabu bado nayadai

Nipe uzoefu wa biashara ya mazao, unanunua mikoa gani haswa? Unadeal na mchele /mahindi?
 
Pole mkuu,
 
Basi bora kuwa mnunuzi wa kati na unapanda taratibu kwa uaminifu
Ila kwa gold detectors nimeziona za German ni nzuri ingawa inategemea na bei ipi unataka zipo mpaka 30m ya bongo lakini uhakika
Nimeona pia mpaka miwani ya kuona dhahabu chini ya ardhi au maji na bei ni 1.5m
Kweli ni biashara nzuri ila high risk
 
Nipe uzoefu wa biashara ya mazao, unanunua mikoa gani haswa? Unadeal na mchele /mahindi?
Mazao ni mpanda mkuu ninatuma vijana wananunua na kupakia ila kila biashara ina changamoto zake na mimi nina biashara za aina tofauti ili kujaziliza pakivuja sehemu

Kuna wakati nilipeleka behewa la mchele dar nikakutana na mafuriko na mchele wa kutoka nje niliuza kwa hasara sana Kama loss ya 5m ila nilirudisha kwenye miradi mingine baada ya miezi miwili
Ila ni kupambana tu mpaka unapata usafiri wako mwenyewe
 
Mkuu kama miwani ya kuona dhahabu chini unayo mnisaidie tuende pale saiti pangu palipo doda tukaangalizie kwa kutumia miwani ili tuone dhahabu zilipo tuanzie hapo nimechoka kufukuzia mwamba naona hiyo miwani itanisaidia
 
Kuna kipindi cha nyuma nilitembelea mji wa Katoro na kushuhudia maisha ya wachimbaji wa Kati na wakubwa! Niliona hii biashara inahitaji uvumilivu wa hali ya juu na mahusiano mazuri na suppliers mfano hardwares nk

Wachimbaji wengi hukopa, mpaka siku wakipata wanalipa cash.Pia wengi wana biashara nyingine inayowapa Mahitaji ya kila siku.

Naona wenye Plant wanafaidi kiasi na wanunuzi, ila yataka moyo.
 
Usikate tamaa ,jipange tena rudi mzigoni .
Pesa ndefu kuipata kwenye madini kibongo Bongo lazima upitie Trials and errors kama hizo
 
Biashara ya dhahabu ni ngumu heri uchimbe gemstone.... mzawa kwenye dhahabu anapiga hatua fupifupi angalie kwenye gemstone watu wanapiga billions kwenye tanzanite,ruby,spinal na green toumaline
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…