Machangu: Wabunge wa katiba wanalipa vizuri

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Wasichana wanaofanya biashara ya kujiuza katika maeneo mbalimbali mjini hapa wameelezea neema iliyowafikia kufuatia kujikusanyia pesa ndefu kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba ambao wanadaiwa kuwalipa vizuri.

Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, wadada hao ambao baadhi wanatokea Mikoa ya Dar, Arusha, Mbeya na kwingineko walisema kipindi hiki wanakiita ni cha mavuno kwao kwani waheshimiwa hao si watu wa kulipa pesa ndogo wanapowaopoa.

"Yaani sasa hivi ni kipindi cha mavuno, wateja ni wengi na wanalipa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma. Kwa mfano ukibahatika kumpata mjumbe wa bunge hili linaloendelea sasa, mbona utafurahi na roho yako! Wanalipa vizuri ile mbaya.

"Kipindi cha nyuma unaweza kulala na mtu akakulipa shilingi 30,000 au 20,000 lakini sasa hivi ni 50,000 kwenda juu, hakuna longolongo, tusipojenga safari hii basi tena," alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Husna ambaye kiwanja chake kikuu cha biashara ni eneo Chako ni Chako.

Mwingine ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini akidai yuko Dodoma bila ndugu zake walioko Dar kujua alisema: "Unajua hii biashara inakuwaga na usumbufu sana, unaweza kuchukuliwa na mtu asikulipe lakini sasa hivi wateja wetu wakuu ni hawa wabunge, wengine wametugeuza nyumba ndogo zao kabisa."

Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, biashara hiyo sasa imeshika kasi kiasi kwamba baadhi ya waheshimiwa humalizia posho zao za siku kwa kuzitumbua na madadapoa hao.

Mwandishi wetu alifanya doria siku za wikiendi maeneo ya Chako ni Chako, Mwenga Bar na zaidi katika kumbi za starehe kama vile Club 84 na Maisha na kushuhudia magari yakipaki na kupakiza wasichana kisha kuondoka.

Gazeti hili linatumia nafasi hii kuwaasa waheshimiwa kufanya walichokifuata bungeni na kuacha michepuko isiyokuwa na maana na wale wasichana walioona njia sahihi ya kutafuta maisha bora ni kwa kujiuza, wajue kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.

Chanzo: Ijumaa Wikienda
 
duuh, wakumbuke kufatlia mchakato WA katiba pia!
 
Mapenzi yanarun dunia..unatafuta pesa ili uitumie na hayo ndo matumizi yenyewe !!tusiwanyooshee wabunge na wajumbe wa bunge la katiba tujitafakari sisi wenyewe kwanza je tu usafi wa kuweza kuwasema wengine ?!!!?
 
Kwaio elfu hamsin ndio dhahabu au jaman hii cheapness sana imezd kwel biashara zko tofauti sana.
 
wewe unadhani kwanini wafanya fujo kila siku ili bunge lichelewe kumalizika na ikibidi liongezewe muda washalewa na mbunye za chako ni chako,kitu ful mnato na pesa za bure za wadanganyika
 
1381613_496097700496949_1414230489_n.jpg
 
Wasichana wanaofanya biashara ya kujiuza katika maeneo mbalimbali mjini hapa wameelezea neema iliyowafikia kufuatia kujikusanyia pesa ndefu kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba ambao wanadaiwa kuwalipa vizuri.

Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, wadada hao ambao baadhi wanatokea Mikoa ya Dar, Arusha, Mbeya na kwingineko walisema kipindi hiki wanakiita ni cha mavuno kwao kwani waheshimiwa hao si watu wa kulipa pesa ndogo wanapowaopoa.

"Yaani sasa hivi ni kipindi cha mavuno, wateja ni wengi na wanalipa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma. Kwa mfano ukibahatika kumpata mjumbe wa bunge hili linaloendelea sasa, mbona utafurahi na roho yako! Wanalipa vizuri ile mbaya.

"Kipindi cha nyuma unaweza kulala na mtu akakulipa shilingi 30,000 au 20,000 lakini sasa hivi ni 50,000 kwenda juu, hakuna longolongo, tusipojenga safari hii basi tena," alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Husna ambaye kiwanja chake kikuu cha biashara ni eneo Chako ni Chako.

Mwingine ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini akidai yuko Dodoma bila ndugu zake walioko Dar kujua alisema: "Unajua hii biashara inakuwaga na usumbufu sana, unaweza kuchukuliwa na mtu asikulipe lakini sasa hivi wateja wetu wakuu ni hawa wabunge, wengine wametugeuza nyumba ndogo zao kabisa."

Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, biashara hiyo sasa imeshika kasi kiasi kwamba baadhi ya waheshimiwa humalizia posho zao za siku kwa kuzitumbua na madadapoa hao.

Mwandishi wetu alifanya doria siku za wikiendi maeneo ya Chako ni Chako, Mwenga Bar na zaidi katika kumbi za starehe kama vile Club 84 na Maisha na kushuhudia magari yakipaki na kupakiza wasichana kisha kuondoka.

Gazeti hili linatumia nafasi hii kuwaasa waheshimiwa kufanya walichokifuata bungeni na kuacha michepuko isiyokuwa na maana na wale wasichana walioona njia sahihi ya kutafuta maisha bora ni kwa kujiuza, wajue kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.

Chanzo: Ijumaa Wikienda
It the way of sharing resorces ,you need them to keep monies?
 
Sisi wabunge wa Katiba tukilalamika hela haitoshi mnachonga.
 
Ni vema kwamba sehemu ya pesa ilipwayo Dodoma huwafikia wahitaji wakubwa.
 
Mapenzi yanarun dunia..unatafuta pesa ili uitumie na hayo ndo matumizi yenyewe !!tusiwanyooshee wabunge na wajumbe wa bunge la katiba tujitafakari sisi wenyewe kwanza je tu usafi wa kuweza kuwasema wengine ?!!!?
Huyo atajuwa mboe na wenje
 
hata angekuwa mimi lazima tuu ningechepuka siku hizi maua yanang'aa sana,
acha wale vitu ilimradi watimize kilichowapeleka.
 
]Stori: Mwandishi Wetu, DODOMA

Wasichana wanaofanya biashara ya kujiuza katika maeneo mbalimbali mjini hapa wameelezea neema iliyowafikia kufuatia kujikusanyia pesa ndefu kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba ambao wanadaiwa kuwalipa vizuri.Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, wadada hao ambao baadhi wanatokea Mikoa ya Dar, Arusha, Mbeya na kwingineko walisema kipindi hiki wanakiita ni cha mavuno kwao kwani waheshimiwa hao si watu wa kulipa pesa ndogo wanapowaopoa.

"Yaani sasa hivi ni kipindi cha mavuno, wateja ni wengi na wanalipa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma. Kwa mfano ukibahatika kumpata mjumbe wa bunge hili linaloendelea sasa, mbona utafurahi na roho yako! Wanalipa vizuri ile mbaya.

"Kipindi cha nyuma unaweza kulala na mtu akakulipa shilingi 30,000 au 20,000 lakini sasa hivi ni 50,000 kwenda juu, hakuna longolongo, tusipojenga safari hii basi tena," alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Husna ambaye kiwanja chake kikuu cha biashara ni eneo Chako ni Chako.

Mwingine ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini akidai yuko Dodoma bila ndugu zake walioko Dar kujua alisema: "Unajua hii biashara inakuwaga na usumbufu sana, unaweza kuchukuliwa na mtu asikulipe lakini sasa hivi wateja wetu wakuu ni hawa wabunge, wengine wametugeuza nyumba ndogo zao kabisa."

Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, biashara hiyo sasa imeshika kasi kiasi kwamba baadhi ya waheshimiwa humalizia posho zao za siku kwa kuzitumbua na madadapoa hao. Mwandishi wetu alifanya doria siku za wikiendi maeneo ya Chako ni Chako, Mwenga Bar na zaidi katika kumbi za starehe kama vile Club 84 na Maisha na kushuhudia magari yakipaki na kupakiza wasichana kisha kuondoka.

Gazeti hili linatumia nafasi hii kuwaasa waheshimiwa kufanya walichokifuata bungeni na kuacha michepuko isiyokuwa na maana na wale wasichana walioona njia sahihi ya kutafuta maisha bora ni kwa kujiuza, wajue kufanya hivyo ni kuhatarisha Maisha yao.
 
Khaa!! Wacha tule ile posho wote. Siku hizi duka langu la vipodozi nauza kwelikweli. Hawa madada wahalalishwe tu na wapewe EFDs
 
Back
Top Bottom