Machali kujiuzulu ubunge?

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Kwa kile kinachoonekana kama hali kuzidi kuwa tete kwa upande wa chama cha upinzani-NCCR Mageuzi,leo mchana Mbunge Moses Machali ametoa tamko kali kwa wale aliowaita kuwa waleta fujo na vibaraka wa wasiotakia mema NCCR-Mageuzi na kusema wasubiri fyekeo la chuma linashuka juu yao muda si mrefu....

Akasema tuhuma dhidi ya M/kiti James Mbatia kuwa ni mbadhirifu ni za uongo na kwamba taarifa kuwa chama kinapokea ruzuku ya shs 100 m toka serikalini ni uzushi na ukweli ni kwamba chama kinapokea sh 10 m kwa mwezi.Amesema kuna watu wameingia NCCR-Mageuzi kwa lengo la kuimaliza na wengine ni watu wakubwa sana(hapa nahisi anawataja Mkosamali na Kafulila) na kadai hawatasita kuwafukuza ikibidi kwa maslahi ya chama chetu.

My take:
Hivi Moses Machali ni nani NCCR-MAGEUZI zaidi ya kuwa mwanachama na mbunge maana hamekuwa msemaji wa chama kuliko hata M/kiti na katibu au kiongozi yoyote wa chama.

source: RFA taarifa ya mchana.
 
Atakuwa ana mahusiano ya hali ya juu na lile jamaa lenye kiti:nerd:
 
Mh.Agripina Buyogera (Mb Kasulu vijijin) amesema yupo tayari kurudisha kadi ya NCCR endapo David kafulila atakuwa mwnyekiti wa NCCR Taifa .Kauli kama hii ilitolewa na Moses Machali wa NCCR mda mfupi kabla ya Jemus Mbatia Kupewa siku 21 za kutakiwa kujieleza kama yeye si kibaraka wa CCM.

Mpaka leo, Mkoa wa Kigoma, Mbeya, Zanzibar, Dodoma, wametoa msimamo kuunga mkono hatua ya kung'olewa Jemus Mbatia kwa makosa ya kuunga mkono CCM.

Kauli ya Agripina na Moses ni maneno yaleyale ambapo inaonekana yametengenezwa na CCM ili kuua Upinzani kupitia kwa Jemus Mbatia.
Agripina Buyogra ameongeza kuwa alimwacha Mume wake na kuungana na Jemus Mbatia katika harakati za siasa ambapo harakati hizo zimezaa matunda ya yeye na wenzake kuwa wabuge!!

Hivi Mbatia aliacha kufanya harakati jimbo la kawe ambako yeye aligombea akaenda kumunadi Mwanamke Agripina??.Inakuwaje Agripina na Halima Mdee ambao wote ni wanawake wapate Ubunge halafu Jemus Mbatia ashindwe na kufungua kesi???

Hivi kumusaidia mtu katika kampeni ni sambababu ya kumkuandamza asiwe na mawazo mbadala???
Mbona Lowassa anasema ndiye alimuweka Jk madarakani lakini Leo Kikwete huyohuyo anataka Lowassa ajivue gamba???

Ni kwa nini utaratibu wa kumupata Mwenyekiti Taifa utawaliwe na vitisho vya kutaka kurejesha kadi??
Hivi krejesha kadi ni kwa faida ya nani??

Wakati wabunge wa Chadema wanatok nje , Kafulila na Mkosamali walitoka nje kuunga CDM lakini Agripina na Moses hawa kutoka nje kutii maagizo ya Mbatia ambaye aliwataka waunge mkono CCM!!!
Je, ninani amewalaumu??

Hivi unaweza kumwacha Mume wako ukaenda kwenye kampeni badala ya kuambatana naye???

Sasa kama ulimwacha Mume wako Mbatia alizibaje Pengo hilo la Mume wako??
BI aGRIPINA umetudhalilisha wananchi kwani tegemeo letu ni kwa Wabunge wote wa Upinzani sasa kama wewe hutake kuwawaheshimu waliokuchagua kwasababu ya Jemus Mbatia ni bora ukaomba ushauri kwa Mume wako akushauli vizuri maana hata CCM ambao unawatumikia hawajasema kuacha Ubunge kwa sababu ya kuondolewa Rostam Aziz na makundi mengineya Mfisadi mabayo yanatakiwa kujivua gamba.
 
....Kwa kile kinachoonekana kama hali kuzidi kuwa tete kwa upande wa chama cha upinzani-NCCR Mageuzi,leo mchana Mbunge Moses Machali ametoa tamko kali kwa wale aliowaita kuwa waleta fujo na vibaraka wa wasiotakia mema NCCR-Mageuzi na kusema wasubiri fyekeo la chuma linashuka juu yao muda si mrefu....akasema tuhuma dhidi ya M/kiti James Mbatia kuwa ni mbadhirifu ni za uongo na kwamba taarifa kuwa chama kinapokea ruzuku ya shs 100 m toka serikalini ni uzushi na ukweli ni kwamba chama kinapokea sh 10 m kwa mwezi.Amesema kuna watu wameingia NCCR-Mageuzi kwa lengo la kuimaliza na wengine ni watu wakubwa sana(hapa nahisi anawataja Mkosamali na Kafulila) na kadai hawatasita kuwafukuza ikibidi kwa maslahi ya chama chetu.

My take:
Hivi Moses Machali ni nani NCCR-MAGEUZI zaidi ya kuwa mwanachama na mbunge maana hamekuwa msemaji wa chama kuliko hata M/kiti na katibu au kiongozi yoyote wa chama.

source: RFA taarifa ya mchana.
Mawazo ya Moses Machali ni mchanganyiko wa maoni ya mgonjwa wa degedege na ugonjwa wa akili!!!

Haina tofauti na mtazamo wa Mwanamke anayesema kuwa usipo nioa nitajiua!!!
 
Ni endapo David Kafulila (mb) au Hashim Rungwe atafanikiwa kuwa mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI.

Moses Machali ni mbunge pia kupitia NCCR-Mageuzi.

SOURCE: TBC1 news bulletin.
 
Tatizo watu au sera zao? Kama ni sera wanazoziamini anatakiwa kuwashawishi kuzikubali sera zake na wala sio kujiuzulu!!!!!!!!!!!! Ila kama shida ni watu hapo hamna mbadala kwani hamna namna wanaweza kubadilika. Vipi kasema atahamia wapi?
 
Huyo akijidanganya kujiuzuru ajue ndio kifo chake kisiasa kitafika.
 
Jamaa labda ana uhakika hao anaowapinga kwa namna yeyote hawawezi kuwa ndio maana ameamua kusema hivyo.
 
Mgogoro wa kiuongozi ndani ya chama cha NCCR Mageuzi unazidi kufukuta na moses machali,mbuge wa kasulu mjini NCCR ameibuka tena na kudai kuwa endapo mbatia atang'olewa madarakani na badala yake awe kafulila au hashim rungwe yeye ataachia ngazi kwenye ubunge na kuwa mwanaharakati.

Kwamba kafulila na huyo Rungwe wameshindwa kukisaidia chama katika nafasi walizonazo hivyo,hawataweza uenyekiti.

My take

Hawa jamaa wa NCCR wote ni wabunge vijana ambao tulitegemea walete mabadiliko sasa kama wanafanya siasa za maji taka namna hii watakiua chama na kutukatisha tamaa vijana wenzao.
 
Tatizo watu au sera zao? Kama ni sera wanazoziamini anatakiwa kuwashawishi kuzikubali sera zake na wala sio kujiuzulu!!!!!!!!!!!! Ila kama shida ni watu hapo hamna mbadala kwani hamna namna wanaweza kubadilika. Vipi kasema atahamia wapi?

Kasema ni bora kuwa mwanaharakati kuliko kuwa under kafulila au rungwe..!Inavyoonekana NCCR hakujatulia na nadhani another second collapse is on the way...!
 
Kasema ni bora kuwa mwanaharakati kuliko kuwa under kafulila au rungwe..!Inavyoonekana NCCR hakujatulia na nadhani another second collapse is on the way...!
Kwani ilinyanyuka lini najuta walinipotezea muda enzi za Mrema 1995 UDSM.
 
[/QUOTE] Mh.Agripina Buyogera (Mb Kasulu vijijin) amesema yupo tayari kurudisha kadi ya NCCR endapo David kafulila atakuwa mwnyekiti wa NCCR Taifa .Kauli kama hii ilitolewa na Moses Machali wa NCCR mda mfupi kabla ya Jemus Mbatia Kupewa siku 21 za kutakiwa kujieleza kama yeye si kibaraka wa CCM.

Mpaka leo, Mkoa wa Kigoma, Mbeya, Zanzibar, Dodoma, wametoa msimamo kuunga mkono hatua ya kung'olewa Jemus Mbatia kwa makosa ya kuunga mkono CCM.

Kauli ya Agripina na Moses ni maneno yaleyale ambapo inaonekana yametengenezwa na CCM ili kuua Upinzani kupitia kwa Jemus Mbatia.
Agripina Buyogra ameongeza kuwa alimwacha Mume wake na kuungana na Jemus Mbatia katika harakati za siasa ambapo harakati hizo zimezaa matunda ya yeye na wenzake kuwa wabuge!!

Hivi Mbatia aliacha kufanya harakati jimbo la kawe ambako yeye aligombea akaenda kumunadi Mwanamke Agripina??.Inakuwaje Agripina na Halima Mdee ambao wote ni wanawake wapate Ubunge halafu Jemus Mbatia ashindwe na kufungua kesi???

Hivi kumusaidia mtu katika kampeni ni sambababu ya kumkuandamza asiwe na mawazo mbadala???
Mbona Lowassa anasema ndiye alimuweka Jk madarakani lakini Leo Kikwete huyohuyo anataka Lowassa ajivue gamba???

Ni kwa nini utaratibu wa kumupata Mwenyekiti Taifa utawaliwe na vitisho vya kutaka kurejesha kadi??
Hivi krejesha kadi ni kwa faida ya nani??

Wakati wabunge wa Chadema wanatok nje , Kafulila na Mkosamali walitoka nje kuunga CDM lakini Agripina na Moses hawa kutoka nje kutii maagizo ya Mbatia ambaye aliwataka waunge mkono CCM!!!
Je, ninani amewalaumu??

Hivi unaweza kumwacha Mume wako ukaenda kwenye kampeni badala ya kuambatana naye???
Sasa kama ulimwacha Mume wako Mbatia alizibaje Pengo hilo la Mume wako??
BI aGRIPINA umetudhalilisha wananchi kwani tegemeo letu ni kwa Wabunge wote wa Upinzani sasa kama wewe hutake kuwawaheshimu waliokuchagua kwasababu ya Jemus Mbatia ni bora ukaomba ushauri kwa Mume wako akushauli vizuri maana hata CCM ambao unawatumikia hawajasema kuacha Ubunge kwa sababu ya kuondolewa Rostam Aziz na makundi mengineya Mfisadi mabayo yanatakiwa kujivua gamba.

[/QUOTE]
King king, hii si mara yako ya kwanza kukishambulia chama cha NCCR-Mageuzi. Ushindwe, pamoja na wote waliokutuma (kama wapo). Kama unamtaka mbunge wetu awe na heshima, jifunze wewe heshima kwanza kwa kuandika majina ya watu kwa usahihi, na kuachana na chama ambacho hakikuhusu. Kama unataka undani wa NCCR-Mageuzi njoo ujiunge, sio kukaa pembeni na kufanya kazi ya kiibilisi; fitina na hiana kwa nyumba usiyolala.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom