Machali kujiuzulu ubunge?

Machali kujiuzulu ubunge?

Binafsi, nachukua fursa hii kumpongeza Mh. MACHALI kwa msimamo wake wa kuapa kujiuzuru ubunge na uanachama wa NCCR iwapo Kafulila atakuwa mwenekiti wa chama hicho, unajua watu wengi hamjui kafulila na tabia zake mbaya, wala huyu hana uzalendo hata kidogo

ni mr.misifa yaani hupenda kusema tu ili aonekane amesema lakini ukija katika suala la utekelezaji wa mipango yake ni ziro kabisa. Nawashauri kumuona kafulila sawa na matapeli wa kisiasa,si mfano wa kuigwa. Kwa upande wa machali aka JEMBE yaani mtu anayependa kusema ukweli daima aungwe mkono, huyu jamaa siyo mbabaishaji hata kidogo ni mtu anayependa kufuatilia mambo kuliko Kafulila, hebu anza tu kufuatilia sifa zao kitaaluma utabaini kuwa Kafulila alitoroka hata chuo,elimu yake mnaijua?muulizeni muone kama atawaambia labda anaweza akawaambia kwa sababu nimechokoza hilo,ni mbabaishaji tu na ndiyo maana anawakimbia hata watu wake jimboni,

hana uwezo wa kujadiliana ni mnafiki wa kupita kiasi.Zipo taarifa kuwa yeye na Hashimu Rungwe wamepata fedha za CCM ili kuhakikisha mbatia nang'oka kwenye uenyekiti eti kwa sababu mbatia kashitaki Benki ya moja inayotetewa na kampuni moja ya kiwakili ya watu wa CCM. Wasiyeyushe hoja, wahojini wamepata wapi hela za kununua wajumbe wa NEC ya nccr?

Aidha siku moja Mh. MACHALI alipata kudai kuwa tayari kafulila alikuwa amemwomba washirikiane kumng'oa Mbatia lakini kwa kuwa machali ni ANALYST wa mambo kitaaluma huwa hakurupuki, alimshauri kafulila haraka ya nini kutaka Mbatia aondoke kwa vurugu?una ajenda gani,Oooh!mimi nataka niwe m/kiti(kafulila huyo)halafu wanasiasa wengi watahamia kwetu na tutajenga chama na kwa hiyo kuna watu wengi wanatuunga mkono wakiwemo akina hashimu Rungwe nk. Kwa hiyo wewe niunge mkono.

MACHALI AKAMJIBU "SIWEZI KUWA CHIMBUKO LA VURUGU ZISIZOKUWA NA FACTS. Nenda katafute hoja nyingine na ukipata sababu za kutosha ndiyo uje", Kiukweli Machali anapaswa kuungwa mkono kwa msimamo wake, hatupaswi kumbeza kama anavyofanya Kafulila kwa kusema kuwa Machali ni mwoga na eti apambane akiwa humohumo nccr.

Kusema hivyo ina maana tunabariki wana ccm na wale wote waliowahi kuwa ccm warejee ccm wakendeleze kupambana humohumo ccm. Wazo la Kafulila limefulia kweli kama jina lake lilivyo, anataka kutushawishi na sisi wana harakati kuwa ccm siyo tatizo, Kimsingi KAFULILA awapelekee ndugu zake hiyo hoja ya kutaka, KAMANDA machali abaki nccr wakati kafulila au Rungwe akiwa mwenyekiti. NAKUBALIANA NA DR. SLAA KUMUITA kafulila SISIMIZI, hakika anfikiria kisisimizi sisimizi.

Ndio maana aliwahi kumsifia KIKWETE Kuwa ndiye Rais bora aliyewahi kuujali mkoa wa kigoma, anamsifia kikwete kwa mema yapi kwa wana kigoma. Kafulila CCM kwelikweli tena CCM "A",halafu huyu jamaa ndiye anayetaka kuwa Mwenyekiti wa NCCR, amefulia kwelikweli na hii ni aibu hata kwa wale wote wanaomfagilia kafulila huku wakijua kuwa ni mtu wa kuzungumza tu huku akiwa siyo mtendaji. Anafagilia CCM Kama hajui ccm NDIYE MCHAWI wa sis kuwa masikini katika hii miaka 50 ya uhuru.

Machali amenena sawasawa kuwa Kafulila na wafuasi wake wakifanikiwa kuingia kwa fujo kabla ya muda kufika ajiuzuru, hakika bravooooooooooooo kwa machali na hii itatoa mwanga na kuwakumbusha watu kuwa ni ujinga na upumbavu kukubali kufanya kazi chini ya mtu ambaye unajua kuwa hafai hata kidogo katika tasisi moja kama kafulila, Inawezekana ni kafulila kaandika hii post hapa JF na kujificha ili aone kama watu tutagilia, hatufagilii ujinga sisi, tunamshauri kafulila arudishe akili zake nyuma akatafakari juu ya yeye kuwa Bw. MITAFARUKU kila anapokwenda alipokuwa CHADEMA vurugu, NCCR vurugu.

Ametumwaa na ccm kuuua upinzani,hafai hata kuwa mkuu wa familia.
Jina lako lipo tofauti na unayosema, sisi wapiga kura tunataka wabunge wapinzani waongezeke halafu wewew unashauli wapungue!!!!

Huoni kuwa wakipungua NCCR itapoteza ruzuku na jimbo litakwenda CCM na Mbatia atapoteza nafasi ya Mwenyekiti!!!
Ndiyo maana nikasema tuwe wakweli kutoa Mawazo sio kukurupuka watu wanatufuatilia afya zetuni ili kupima uwezo wetu!!!???
 
Hivi Mbatia akiondoka akapata cheo Hashimu Rungwe kuna nini???
Kwa nini tuwe na Umimi , Ndio maana CCM wanatutawala!!!
 
Hivi Mbatia akiondoka akapata cheo Hashimu Rungwe kuna nini???
Kwa nini tuwe na Umimi , Ndio maana CCM wanatutawala!!!
 
Hivi unamaanisha NCCR imekuwa inaendeshwa kwa fedha za CCM, Kwanini Hashimu Rungwe achukue Fedha CCM na sio CHADEMA???
Naamini wewe uliye jisajiri sasa hivi humu JF umelenga kumutetea hasa MBATIA , inawezekana Chuki ya Mbatia inatokana na hisia kuwa Hashimu Rungwe kachukua Fedha CCM kama Mbatia anavyo Chukua !!!
Mimi najua Mbatia Kaka mda Mrefu sana anaendesha NCCR bila yeye kuwa na biashara yoyote lakini matumizi ni makubwa !!!!

Angekuwa mtumishi wa serikali alipaswa kutangaza mali!!!
Angalia wakati wa uchaguzi alijenga ofisi za NCCR kila tawi eneo lote Kawe!!!

Sasa Hashimu Rungwe anabiashara lakini Mbatia hana biashara!!!

Moja ya Malalamiko ya Mh Agripina ni kwamba Mbatia amewasaidia sana kifedha lakini hakuhoji hizo pesa Mbatia alikuwa anatoa wapi wakati NCCR haina ruzuku??
Misaada kama hiyo ndiyo imetupeleka pabaya na David Cameroon ameanza kutoa masharti Mabaya!!!
Nawaomba NCCR kwa kuwa Mbatia ndiye aliyekuwa na Mkataba na CCM kupokea fedha muondoeni ili kuepuka mashart ya CCM!!!

Angalia suala la Mswaada linawashinda baada ya Mbatia kwataka Agripina na Moses kuambatana na CCM Mbungeni wakati Mkosamali na Kafulila wanaunga mkono CHADEMA!!!

Mbatia ni Munafiki anasema hataki kwenda Ikulu kumuona JK wakati anapata fedha za kuua Chadema kwa mlango wa nyuma!!!


Kama kweli Mbatia anapinga mswaada kama CDM kwa nini yeye kama Myenyekiti haungani na MBOWE kama kafulila alivyofanya ???
 
[h=2]6 DECEMBER 2011[/h][h=3]
[/h]

Na Pendo Mtibuche, Dodoma

JINAMIZI la kutaka kumtimua Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, limechukua sura mpya baada ya
Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama hicho, Bw. Moses Machari, kusema kuwa kama harakati za kumuondoa zitafanikiwa, wanaoendesha harakati hizo za usaliti dhidi ya mwenyekiti wao wakifanikiwa yuko tayari kujiuzulu ubunge na kuwa mwanaharakati.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, mbunge huyo alisema mgogoro huo uliodumu sasa ndani ya chama chao unatokana na uroho wa madaraka kwa baadhi ya viongozi wanaotaka nafasi ya Bw. Mbatia na si vinginevyo.

Alisema hivi sasa imefikia wakati baadhi ya viongozi kutumia fedha zao kurubuni baadhi ya viongozi wa chama hicho ili wapite mikoani kufanya shinikizo la kumkataa Bw. Mbatia na kutoa tuhuma ambazo si sahihi.

"Jambo hili nalipinga kwa nguvu zote, si sahihi baadhi ya viongozi ndani ya chama chetu tukaanza kusalitiana kwa kutumia fedha walizonazo kutaka kuondoa viongozi kwa malengo yao binafsi, hili likitokea mimi nitajiuzulu ubunge na kuwa mwanaharakati wa kawaida tu," alisema mbunge huyo.

Alisema chanzo cha vurugu zote ndani ya chama hicho ni kutokana na viongozi kuhusika kupigania madaraka kwa masilahi yao binafsi na kutaka kukivuruga.

Aliwatuhumu viongozi hao aliowataja kuwa ni wasaliti kwa Bw. Mbatia na kueleza kuwa baadhi ya madai yao si sahihi ikiwemo ya matumizi mabaya ya ruzuku ya chama hicho ya sh. milioni 130 kwa mwezi na kwamba ni uzushi na hoja ya kukosa kugombea na kukosa ubunge kwa mwenyekiti huyo haina msingi kwa kuwa hata yeye aliwahi kukosa.

Alisema chama hicho kinapata ruzuku ya sh.milioni 12 kwa mwezi na siyo milioni 130 kama inavyodaiwa na wabaya wake hao wanaonyemelea nafasi yake na kuwataka wanaotaka kuthibitisha hicho kwenda katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Bw. John Tendwa.

Alisema watu hao ndiyo wanaoeneza uvumi kuwa Bw. Mbatia ni wakala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwataka wajitokeze hadharani kuthibitisha hayo madai ili watumie katiba ya chama chao kukomesha hayo kama yapo.

Akizungumzia vikao vilivyoendeshwa na viongozi wa chama hicho Mkoa wa Dodoma ulioripotiwa kuvunjika na baadhi ya vyombo vya habari baada ya hoja hiyo ya Bw. Mbatia kuingizwa alisema viongozi hao wanatumiwa na baadhi ya kundi hilo linalompinga Bw. Mbatia kutekeleza hayo wanayotaka.

Alisema kutokana na hali hiyo wanawaomba wanachama wao kusimama imara na kulaani vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi na wanachama wanaopita huku na kule kueneza uongo dhidi ya mwenyekiti wao.

Kwa upande wake Kamishna wa chama hicho Mkoa wa Dodoma, Bw. Mohamed Kabutari, ambaye ni miongoni mwa watu wanaotuhumiwa kupewa fedha kwa ajili ya kueneza kile kinachodaiwa kuwa ni maovu ya mwenyekiti wao kwa lengo la kumkataa alisema yeye anamkataa Bw. Mbatia kwa madai kuwa ni azimio.

Alisema yeye kama Mjumbe wa Halmashauri ya chama hicho taifa, katika mkutano wa Halmashauri Kuu uliofanyika Dar es Salaam Novemba 5, mwaka huu kilichohusisha wajumbe 28 wote waliazimia kutokuwa na imani na mwenyekiti wao hivyo suala hilo si kwamba yeye kama kamishna wa chama hicho Mkoa wa Dodoma anamkataa.

Akizungumzia madai ya Bw. Machari kuwa wapo viongozi na wanachama wanaopewa fedha ili kumkataa Bw. Mbatia alisema hayo ni maneno ya kitoto na kukanusha mpango wowote wa kumpendekeza mtu yeyote kuwa mwenyekiti kama inavyodaiwa kuwa wapo baadhi ya watu majina tunayo.

Alisema hata kama mbunge huyo atajiuzulu nafasi yake ya ubunge, chama hicho hakiwezi kuyumba na kudai kuwa yeye hana ugomvi wowote na baadhi ya viongozi wenzake wa chama hicho mkoani Dodoma.

Alisema katika kikao chao walichokifanya mjini Dodoma kwa kuhusisha wenyeviti wa majimbo sita ya Mkoa wa Dodoma yaani Kibakwe, Bahi, Mtera, Kondoa Kusini, Kondoa Kaskazini na Kongwa walizungumzia mambo mbalimbali ya chama chao.Hata hivyo kikao hicho kilidaiwa kuvunjika baada ya hoja ya kutaka wamkatae Bw. Mbatia kuwasilishwa.



 
Kumbe kuna wabunge ndani ya NCCR Mageuzi ambao wanampenda Mwenyekiti James Mbatia?
 
Back
Top Bottom