Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,186
- 10,922
Mamia ya raia wa Israel wameendelea kuandamana karibu na makazi ya raisi wa nchi hiyo wakitaka vitu viwili.Kwanza ndugu zao waliotekwa warudishwe na Benjamin Netanyahu aondoke madarakani kwa kuitumbukiza nchi hiyo kwenye machafuko.
Hayo yakitokea kumekuwa na ukimbizi mkubwa wa ndani ya nchi ambapo wakazi wote wanaokaa mipakani ama wameondoka kuelekea katikati ya nchi au wamepata amri ya kuhama kwa hofu ya kutokea mapigano karibu na makazi yao.Hali hiyo imeonekana kuwaathiri zaidi wakazi wa kaskazini ambako mapigano kati ya Israel na kundi la Hizbolah ymekuwa yakiongezeka muda baada ya muda.
Umoja wa wenye mahoteli wanalalamika kupelekewa wateja wasiowatka waliojaza hoteli zoo.