Machache kuhusu Malkia Elizabeth wa pili

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Malkia Elizabeth wa pili amefariki Sept.8, 2022.

Anaitwa Elizabeth Alexander Marry (Malkia Elizabeth II wa pili ),alirithi madaraka kutoka kwa Baba yake ,Mfalme George wa sita 1952 (Prince Albert,Duke) . Mfalme George VI wa sita hakuwa na Mtoto wa kiume ,kama laiti angelikuwa na Mtoto wa kiume basi mtoto huyo wa kiume angerithi kiti cha ufalme.

Mfalme George aliyetawala kuanzia Desemba 11 ,1936 hadi Februari 6 ,1952 alizaa watoto wawili tuu wote wa kike ,mmoja ni Elizabeth ambaye ndiyo wa kwanza na wapili ni Margaret.

Mfalme George alipofariki 1952 ,Mtoto wake wa Kwanza Elizabeth akaridhi mamlaka hivyo kuitwa Malkia Elizabeth II wa pili tangu 1952 hadi 2022 , vyema kujua huyu ni Malkia Elizabeth wa pili ni tofauti na Malkia Elizabeth I wa Kwanza .

Malkia Elizabeth I wa kwanza alikuwa Malkia wa Uingereza na Ireland kutoka 1558 hadi 1603, mwisho wa watawala wa Tudor .

Huyu aliyefariki ni Malkia Elizabeth wa pili alitawala kutoka Februari 6,1952 hadi kifo chake Sept.8 ,2022 ,ndiyo maana tangu tunazaliwa hadi sasa tulikuwa tunasikia tuu Malkia Elizabeth ,Malkia Elizabeth.

Malkia Elizabeth aliolewa na Prince Philip ,sheria inakataza mume kuwa na nafasi ya ufalme sababu nafasi yao ni ya kurithi ndani ya udugu wa damu tangu miaka na miaka.

Kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth ,mtoto wake mkubwa Charles ndiye sasa amechukua nafasi na kiti hivyo anaitwa Mfalme Charles wa III tatu (King Charles III).

Mfalme Charles ana miaka 73 ,ndiye mtoto mkubwa wa Malkia Elizabeth kati ya watoto wake 4 ,aliyezaa na hayati mume wake Prince Philip ambaye alifariki mwaka uliopita 2021.

Hivyo jina Sasa sio tena Malkia ,kama tulivyozoea sasa ni Mfalme Charles wa watatu (III).

Mungu amlaze panapostahili Malkia Elizabeth.


Kwanini anaitwa Mfalme Charles wa tatu (III) ?.
au kwa maana nyingine nini maana ya malkia wa kwanza au Malkia wa pili , Mfalme wa pili au Mfalme wa sita ?.

Hii ni namna na njia ya kutofautisha majina ya wafalme au Malkia ambao wamewahi kutawala lakini majina yao yana fanana.

Sababu katika utawala wa Tudor ,huko Uingereza kabla ya utawala wa Stuart Dynasty kulikuwa na King Henry wa Saba (vii) alitawala kuanzia 1485-1509 ,alafu kukawa tena King Henry wa 8 (viii) aliyefuata akatawala 1509 -1547) .

Baada ya Malkia Elizabeth wa kwanza kufa 1603 utawala ukahama kutoka Tudor hadi Stuart Dynasty ambapo aliyefuata alikuwa ni binamu wa Queen Elizabeth wa kwanza aliitwa King James wa kwanza sababu Queen hakuzaa.

Huyu King James wa kwanza aliongoza kibabe akijiita God's Lieutenant (Divine right of King). Mwaka 1625 King James wa kwanza akafa .

Lakini baadaye katika utawala alitokea Mfalme Mwingine anaitwa James huyu aliitwa King James wa pili (II) ambaye alipinduliwa mwaka 1688 (Glorious Revolution).

Baada ya king James wa Kwanza kufa 1625, Mfalme aliyefuata ni Charles wa 1 (King Charles I ) 1625-1645 , huyu Charles alipinduliwa (Puritan Revolution/First English Revolution) 1645.Ukaingia uongozi wa Oliver Cromwell.

Mwaka 1658 Oliver Cromwell alifariki , Uingereza wakaamua kumuita mtoto mkubwa wa Charles wa kwanza ,aliyeitwa Charles alikimbilia ufaransa akaitwa kuja kutawala huyu aliitwa Mfalme Charles wa pili alitawala kuanzia 1660-1685 .

Huyu mtoto mkubwa wa Malkia Elizabeth ,anaitwa Charles huyu sasa ni Mfalme Charles wa tatu baada ya yule Mfalme charles wa pili wa 1660 hadi 1685 .

Ukumbuke hata huyu Malkia Elizabeth wa pili aliyefariki baada ya kutawala kuanzia 1952 hadi 2022 aliitwa Malkia Elizabeth wa pili sababu hapo nyuma kuliwahi kuwa na Malkia Elizabeth mwingine aliyeitwa Malkia Elizabeth wa kwanza , aliyetawala kipindi Cha Tudor Monarch kuanzia 1558-1603.

Abdul Nondo.
IMG_20220908_230154_829.jpg
 
Nani anapokea rambi rambi ya msiba wa malkia Elizabeth? Tujitahidi kuchangia, wasije wakashindwa kusafirisha na kuzika mwili wa mpendwa wao.wana JF.
 
Back
Top Bottom