Wana Jf, habari zenu. Niko katika pilikapilika za kutafuta chuo cha certificate kwa ajili ya mdogo angu. Sasa nikawa nimefika Tengeru Arusha ili kuchek uwezekano. Baada ya kufika Tengeru nikaambiwa vyo vya cheti ambavyo ni matawi ya Tengeru ni Mabughai, Ruaha na Uyole. Nimejaribu kutafuta kwenye tovuti za chuo lakin bado sijaona taarifa za muhimu zinazofafanua vyuo hivyo. Hivyo bas, naombeni kwa yeyote mwenye kujua vyuo hivyo anihabarishe tafadhal. Pia ushauri wa kipi chuo bora kati ya hivyo. Mchango wenu ni wa muhimu sana wana JF. ASANTENI