"Mabro" mnalia lia sana mnatufundisha nini?

"Mabro" mnalia lia sana mnatufundisha nini?

Wrevta

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2023
Posts
1,442
Reaction score
1,733
Kazi na iendelee! JF humu haipiti week bila ya kusoma uzi wa "bro" akilia lia kuhusu kuumizwa na mke wake au mchumba ambaye anatarajia kumuoa.

Hii ni red light kwa wadogo zenu ambao nasi tunakuja huko huko mlipo. Mnapolia lia mnaleta picha gani? Hivi hamjui ya kuwa nyie ni barua na wasomaji ni sisi wadogo zenu?

Yaani mpaka unajiuliza, huyu "bro" ana kamasi au ubongo? Ukijilinganisha naye kwenye mizani unaona kabisa kuwa unampiga gap parefu mno. Hana akili kabisa (sorry for this but its a reality).

Unasema moyoni, huyu angekuwa "bro" wangu ningevizia usiku njiani na vijana wenzangu tupige mitama na viboko kabisa. Yaani unaona kabisa kichwani hakuna kitu, ila kwa kuwa ni "bro" unaamua tu kuipitia thread kimya kimya.

Mnatuumiza mno wadogo zenu, sijui mnaleta picha gani kwetu.
Wapo "mabroo" wengi ila sitowataja nawahifadhi... ila jueni tu kuwa mnatusononesha sana wadogo zenu.

Kama nyie mnalia lia sisi tujifunze nini?
Unakuta mara mwingine analalamika amegundua watoto siyo wake, mara huyu analalamika ananyimwa tendo na mkewe, mara huyu anachunwa na mke wake, mara huyu katapeliwa mali nk

Kama mdogo nitashindwa kuvumilia huku mbeleni, sitopita kimya kimya nitakuwa natoa shit... mnakera sana "mabroo".

Hawa wafuatao najivunia mno kuwafahamu, nimejifunza vingi kwao, nao ni;
Robert Heriel Mtibeli DeepPond Mshana Jr Countrywide na wengine wengi sana ambao sitowataja kutokana na wingi wao...

All in all

"Mabroo" mnatuangusha mno! Sijui tuanze kuwachapa makofi...
 
Kazi na iendelee! JF humu haipiti week bila ya kusoma uzi wa "bro" akilia lia kuhusu kuumizwa na mke wake au mchumba ambaye anatarajia kumuoa.

Hii ni red light kwa wadogo zenu ambao nasi tunakuja huko huko mlipo. Mnapolia lia mnaleta picha gani? Hivi hamjui ya
Mabroo zako wenyewe ndiyo hao wanaolia hata wakipewa 'Dislike' kwenye comment, hapo unategemea nini?
 
Ni kwa sababu maandiko ya sisi wenye amani na furaha kwenye ndoa hatuyaandiki mara nyingi. Sijajua kama mimi ni bro ama baba yako mdogo.

Huku kunatawala nyuzi za wanaoomba ushauri wa kutendwa ama magumi wanayoyapitia.

Nyuzi za furaha huwa hazipo ama zipo kwa uchache kwa sababu kunakuwa hakuna ulazima wa kushare.

Lakini tupo sana. Hao wanaolia, wanatafuta suluhu. Wapo wengine wanakufa nayo moyoni.

Usiwakebehi.
 
Sawa mzee wangu. I am 25, huenda ukawa ni baba yangu kiumri.
 
Sasa hata akituma uzi wa kulia c unajifunza pia au!!
Ukianza haya mambo ndo utafahamu vizuri
 
Ndo shida za kuanza mapenzi ukubwani mtu yupo 27+eti ndo ana fall in love sijui alkua wapi enzi za u teenager wake
Kwani mtu akianza mapenzi akiwa na 27 inahesabika kaanza mapenzi ukubwani?
 
Back
Top Bottom