Mabomu yalipuka Shinyanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu yalipuka Shinyanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bornvilla, Feb 28, 2011.

 1. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mabomu yamelipuka katika maeneo ya kizumbi lakini hayakusababisha maafa.Mabomu hayo yaleta hofu kwa wakazi wa mjini Shinyanga. Source:kidau.blogspot.com
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ni kambi ya jeshi??
   
 3. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nini tena? Ni mabomu kwel?
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Taarifa yako haihamasishi mjadala iko juujuu sana. Hakuna jina la kambi, siku mabomu yalipolipuka na mengineyo yanayoweza kuibeba taarifa yako kutoka taarifa tetesi kwenda taarifa ya kweli.
   
 5. W

  We can JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kipindi cha magazetini leo asubuhi wamesema ni Kambi ya Jeshi-KIZUMBI.
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,115
  Trophy Points: 280
  Gazeti gani hilo?
   
 7. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkubwa, Is this the best you can do????.... I think you could do better than that?? Taarifa yako ni fupi zaidi ya mno. Hebu tuletee taarifa iliyokamilika angalau kidogo.
   
 8. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Mabomu yamelipuka kwenye kambi ya Jeshi iitwayo kizumbi ambayo iko nje kidogo ya mji wa Shinyanga ila hakuna madhara yaliyotokea. Ki ukweli kambi hiyo haiko close sana na makazi ya watu kama ile ya gongo la mboto labda masoja waamue kuyavurumisha wenyewe mbali. Poleni Shinyanga kwetu loh!
   
 9. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka pale kizumbi kuna kambi ya jeshi, poleni sana waathirika. Sasa sijui next ni wapi
   
 10. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mhh Kuna maandamano Shinyanga leo ya Chadema naona maandalizi yameanza...
   
 11. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ahaaaaa!! Hao jamaa wameanza kweli mipango yao ya uchakachuaji maandamano ya CHADEMA. Maana presha yao imewapanda ile mbaya.
   
 12. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Hiyo kambi ni Kizumbi kweli au Old Shinyanga? Tuleteeni habari zaidi tafadhali
   
 13. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,848
  Likes Received: 2,775
  Trophy Points: 280
  Shinyanga mama kuna kambi hizo mbili: Moja inaitwa Old Shinyanga na nyingine inaitwa Kizumbi. Bahati nzuri hizi kambi ziko mbali kidogo na makazi ya watu. Ingawa Old Shinyanga iko karibu, lakini maghala ya silaha yako mbali na mji mdogo wa Old Shinyanga. Kizumbi nayo ndo iko porini mbali kutoka barabara ya Mwanza - Tabora.
   
 14. s

  seniorita JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kama kweli basi hali hhii ya kushikitisha sana nchi hii; hope hayahusiani na wimbi la CDM maandamano
   
 15. Kahema

  Kahema JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2011
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  si walisema hayalipuki tena au? mhhu. mara ya kwanza walisema tukalale mabondeni mara tujiandae kulala angani. yetu macho.
   
 16. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mbona jamaa ametoa maelezo vizuri kwenye hiyo link yake ya K I D A U
  someni kwanza ndo muulize!
   
 17. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  soma vizuri K I D A U kabla ya kuanza kuporomosha lawama!
   
 18. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  duh! mkuu sioni uhusiano hata kidogo wa haya mambo mawili!!!!
   
 19. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #19
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  WAKATI kumbukumbu ya milipuko ya mabomu katika kambi ya JWTZ ya Gongo la Mboto ikiwa bado hazijafutika katika fikra za wakazi wa jiji la Dar es Salaam, mabomu mengine ya jeshi yamelipuka katika kambi ya Kizumbi mkoani Shinyanga.Lakini tofauti na milipuko ya GongolaMboto, yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 20, na wengine 400 kujeruhiwa, milipuko ya Kizumbi, hayakuleta madhara yoyote.

  Milipuko ya Gongo la Mboto iliyotokea usiku wa Februari 16 mwaka huu, pia imesababisha mamia ya wananchi, kukosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao, kuharibiwa.

  Habari za awali zilisema mabomu ya Kizumbi, yalilipuliwa kwa makusudi kwa lengo la kuyateketeza baada ya kuthibitika kuwa muda wake, umepita.

  Ingawa mabomu hayo hayakuleta athari, yamesababisha taharuki kubwa, kama iliyowakuta wananchi wa Gongo la Mboto ambao wengi wao walikimbia na kwenda katika maeneo wasiyoyajua, ili kusalimisha maisha yao.

  Habari zilisema kulipuliwa kwa mabomu katika kambi ya Kizumbi, kulianza Ijumaa iliyopita na kwamba milipuko hiyo, imesababisha hofu kubwa miongoni mwa wananchi.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana, zilisema hofu hiyo imewakumba zaidi wakazi wa mji wa Shinyanga.

  Kwa mujibu wa habari hizo, ulipuaji wa mabomu katika kambi hiyo iliyoko nje kidogo ya mji huo, jana uliingia katika siku yake ya tatu.

  Mmoja wa wananchi mwenye makazi yake karibu na kambi hiyo, Masumbuko Masunga (36), alisema milipuko hiyo imesababisha watu wengi kukimbia makazi yao.


  Alisema hatua hiyo imetokana na hofu ya kupoteza maisha kama ilivyowahi kutokea kwa wakazi wa Mbagala na Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani, alithibitisha kutokea kwa milipuko hiyo, lakini aliwataka wananchi, wasiwe na wasiwasi kwa sababu mabomu hayo yanalipuliwa wanajeshi wenyewe.

  Kamanda Diwani alisema kabla ya kuanza kwa kazi ya kulipua mabomu hayo, JWTZ ilitoa taarifa kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga na wa watu wa vijiji vyote vinavyozunguka kambi.

  Kwa mujibu wa kamanda huyu, kazi ya kuteketeza mabomu hayo, inatarajiwa kukamilika leo.

  Hata hivyo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha JWTZ, Luteni Kanali Kapambala Mgawe, aliliambia gazeti hili jana kuwa hana taarifa kuhusu ulipuaji wa mabomu hayo.

  Alisema "nilisikia taarifa hiyo tangu jana (juzi) lakini, hazikuwa rasmi na baadaye nikajua kuwa hazikuwa na ukweli wowote," alisema Mgawe.

  "Sisi tunafanya kazi saa 24, taarifa hizo nimezisikia tangu jana sidhani kama zina ukweli wowote. Mabomu ya Gongo la Mboto nilipata taarifa baada ya dakika 10 tu tangu mabomu yaanze kulipuka, lakini hayo unayonieleza sijapata taarifa yoyote. Labda mabomu hayo yawe yanalipuka sasa hivi," alisisitiza.

  Ofisa huyo wa JWTZ alisema hajapata taarifa zozote kuhusu kulipuka kwa mabomu.
  "Sidhani kama kuna kitu kama hicho, ngoja tuangalie, haiwezekani tukio kama hilo litokee msemaji wa jeshi nisiwe na taarifa," alisisitiza.

  Kamanda Diwani alisema tangu kuanza kwa kazi ya kuyateketeza mabomu hayo, hakuna taarifa yoyote inayohusu athari au madhara kwa wananchi na mali zao.
  Tathmini Gongo laMboto vurugu tupu


  DOSARI zimeanza kujitokeza katika tathmini ya mali iliyoharibiwa kwa milipuko ya mabomu iliyotokea kambi ya JWTZ Gongo la Mboto, baada ya wathamini kukataa kutambua mali zilizoteketea kabisa.

  Habari zilisema wathamini hao wanataka waonyeshwe mabaki ya mali zilizosalia na si kuelezwa kuhusu mali zilizotekea kabisa, jambo ambalo limezua mtafaruku baina yao na waathirika.

  Msimamo huo, juzi ulisababisha kuzuka kwa vurugu zilizoambatana na kutupiana maneno kati ya wananchi na kikundi wathamini wanaoendesha shughuli hiyo.

  Mwandishi wa habari hizi aliyetembelea Gongo la Mbobo juzi, aliwakuta wasimamizi hao wakizozana na waamiliki wa nyumba waliotaka mali zao zitambuliwe na kufanyiwa tathmini, lakini wathimini wakagoma.

  "Msituonyeshe mali ambazo hazipo,tunataka kuandika mali zinazoonekana tu, zile ambazo hazionekani hatuhusiki nazo kabisa ndivyo tulivyoogizwa,"alisema mmoja wa wathamini hao, kutoka Ofisi ya Waziri (Mkuu Kitengo cha Maafa).

  Ofisa huyo ametambuliwa kwa jina moja la Christopher.
  Kauli hiyo iliibua hasira za wakazi ambao walianza kurushiana naye maneno huku wakisema huo ni usanii waliokuwa wakiutegemea kutoka katika serikalini.

  Mkazi wa Gongo la Mboto aliyejitambulisha kwa jina moja la Agnes alisema hawana imani kabisa kuhusu mpango wa kuthamini mali kwa sababu haki haitendeki."Tulijua watatusaidia lakini kumbe wanatumia lugha chafu kwetu kama vile wanaongea na maadui zao,"alisema.

  Violet Sambiwa alisema lugha ya matusi inayotumiwa na wathamini hao si nzuri na kwamba wanapaswa kuwasikiliza waathirika na kutekeleza haja zao.

  Gazeti hili lilipotaka kuzungumza na mmoja wa wathamani hao, aligoma na kusisitiza kuwa asingependa kupigwa picha."Nyie mnaojiita waandishi hebu nipatieni vitambulisho vyenu ndio muanze kupiga picha hapa la sivyo mwondoke,"alisema.

  Pamoja na kumpa vitambulisho, ofisa huyo aliendelea kugoma kuzungumza na waandishi na badala yake, aliwafukuza akisema kwa mujibu wa taratibu zao, hawatakiwi kupigwa picha wakiwa kazini.


  Serikali yashauriwa kurejesha mafunzo ya JKT
  SERIKALI imeshauriwa kurejesha sheria ya lazima ya mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kuwasaidia wananchi kupata mbinu za kujihami na majanga.

  Ushauri huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Radio Sauti ya Qurani, Shamim Khan.

  Khan ambaye aliwahi kuwa mbunge na waziri, alitoa ushauri huo wakati kamati hiyo ilipotembelea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto na kutoa misaada mbalimbali kwao.

  Alisema maafa yanakuwa makubwa kwa sababu wananchi wengi hawajui namna ya kujihami na majanga na badala yake wanakimbia hovyo.

  Khan alishauri JWTZ kutoa mafunzo ya namna ya kujihami na majanga ya namna hiyo kupitia vituo vya televisheni na radio ili wananchi waelewe.

  Habari hii imeandaliwa na John Dotto, Shija Felician, Shinyanga na Fidelis Butahe, Hussein Issa na Said Powa

  Mwananchi
   
 20. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  dada Regina, old shy kuna kambi 3 za jeshi ila hakuna ghala la silaha hata moja, ni mizinga, vifaru na zana nyingne nzito nzito. mabomu yote ya zana hizo huifadhiwa Kizumbi, shinyanga mjini. Nimeishi old shinyanga kwa miaka 15 ktk kambi ya jeshi, naijua story yote usiogope old shinyanga is safe!!
   
Loading...