Mabomu ya Polisi yatanda Ubungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu ya Polisi yatanda Ubungo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkeshaji, Apr 3, 2012.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wanabodi,
  Asubuhi hii FFU wamewatawanya wamachinga katika maeneo ya Ubungo mataa, Ubungo maji, stendi ya mkoa na wale wanaofanya biashara katika maeneo ya gridi ya taifa.

  Mojawapo ya maeneo ambayo yameathirika ambayo nimeyashuhudia ni ile baa ya Standard ambayo ipo karibu na stendi ya mkoa. Baa hiyo imevunjwa katika eneo lake la mbele ikiwa ni hatua za utekelezwaji wa oparesheni hiyo.

  Kuna magari ya FFU na askari kanzu yasiyopungua 30 ambayo yametanda maeneo hayo ya Ubungo. Pamoja nayo yapo mawashawasha mawili ambayo yanasubiri kufanya kazi pale itakapohitajika.

  Kwa ujumla hali bado ni shwari na machinga wengi wameingia mitini kwa sasa japo kuna kajikundi kadogo ambacho bado kanajibizana na askari pale maeneo ya mataa. Kajikundi hako kana mabango mawili ambayo yanasomeka:
  "Haya ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania?"
  "Nyie mnasaini posho mnakula, siye tunakufa na njaa".

  Oparesheni hii inafuatia matangazo yaliyokuwa yanatolewa na Tanesco, Tanroads na Manispaa ya Kinondoni ya kuwaondoa watu wanaofanya shughuli katika maeneo ya gridi ya taifa, chini ya njia za umeme na katika hifadhi ya barabara.
  Kwa mujibu wa Tanesco, Tanroads na Manispaa ya Kinondoni ilitakiwa wafanyabiashara hao wawe wameondoka katika maeneo hayo kufikia tarehe 01.04.2012 la sivyo wangeondolewa kwa nguvu.

  NB:
  Kwa wale akina Tomaso: Sikuweza kupata picha kwa sababu kamchina kangu hakana uwezo wa kuchukua picha.
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  na vile wana hasira za arumeru basi vijana wote ni adui
   
 3. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Sioni tatizo kuwaondoa ila sasa wangeweka mipango wawapeleke sehemu ambayo watafanyia hizo kazi ili wawe wanalipa hata ushuru...tatizo wanawafukuza lakini waende wapi? na hii ni shida ya hii nchi hakuna mipango kila mtu anajiwazia yeye tu...

  Lile eneo litakua na usalama zaidi hao machinga wakiondolewa mana kwanza asilimia kubwa ni vibaka wanaiba wanajichanganya pale.
   
 4. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli mpango huu ni mzuri kwa usalama wa hawa wafanyabiashara, matumiaji na taasisi zinazomiliki maeneo hayo na maendeleo yetu. Mpango huu pia utatusaidia ktk zoezi la mipango miji.

  Lakin tatizo langu ni nguvu na mbinu inayotumika. Hv serikali haijui kuwa wafanyabiashara hawa wanategemea biashara hizi kuishi wao na familia zao? Hivi haijui kuwa kwa kufanya hivi ni sawa na kukiuka haki zao za kuishi? Kwa nini wasingeandaa mpango wa kuwahamishia sehemu nyingine au kuwawekea mazingira bora zaidi ya kufanya biashara?
   
 5. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono serikali kuondoa hao vibaka sintasahau mwaka 2008 yaliyonikuta hapo.
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Polisi wa Tanzania katika kazi wanazopenda kuzifanya, na huzifanya kwa ufanisi mkubwa sana ni hii ya kuwapiga wamachinga.

  Utashangaa wamejaza mabomu ya machozi, risasi za moto na magari ya washawasha kama vile wanakwenda vitani. Pamoja na hasira za kugaragazwa Arumeru, serikali ina hasira za wanaubungo kuikataa ccm na wanatambua kwamba vijana wanazidi kuikataa.

  Well, ni wazo zuri kuwaondoa katika hayo maeneo hatarishi lakini wamewaandalia maeneo ya kuwahamishia? kwani magufuli na tanesco hawajui kwamba hao watu wako hapo ili kujitafutia rizki zao!? kwanini wasiwaandalie mahali muafaka pa kufanyia biashara kabla ya kutumia maguvu kuwahamisha?
   
 7. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,843
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 180
  Nadhan ni Muhimu Kwa hili Zoezi Kufanyika sasa kwani ilikuwa Hadi Inatia Aibu!! Naomba liwe Endelevu!! Na planning for new areas for business nayo iwe endelevu!! Kulocate maeneo ya hawa wafanyabiashara shida ni nini? Tanesco wahamishwe then Tunajenga soko Pale!! Watu wanataka kupata huduma karibia na bus stops / Railway stops na Halmashauri Husika wanaweza kupata Mapato!! Akina Jerry wameishiwa Mbinu hadi wamebaki kuangalia Mabango tu!! Shame on them!!
   
 8. N

  NALO LITAPITA JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 294
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Sina tatizo na kuwaondoa ila basi wawapatie eneo la kufanya biasaende wapihara zao.unapo wafukuza w
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Msitegemee ccm kuungwa mkono, kila kukicha wanatengeneza uadui na raia, hawayaoni makosa yao, kwa mfano, serikali ya ccm kuiweka gridi ya taifa pale ilipo ni location mbaya, ni rahisi sana kuhujumiwa akitokea mhujumu, kwa mujibu wa master plan ya mipango miji, stand ya mabasi inasomeka ilipaswa kuwa maeneo ya tabata, kuna eneo kubwa sana lilitengwa kwa ajili hiyo, wamemegeana maeneo na kiua plan hiyo, wakajibana pale ubungo terminal iliyokuwa ya uda, hostel za chuo kikuu kuzijenga mabibo ni kosa jingine la wazi kwa serikali ya ccm, wangezijenga kwenye eneo la chuo kikuu mlimani kwani pana eneo kubwa sana, badala yake kuna biashara ya kiuwekezaji, mlimani city. location ilipo upcountry bus terminal ukijumlisha movement ya wanachuo kwenda na kurudi main campus kunafanya kuwepo watu wengi eneo la grid ya taifa na ndipo wamachinga kwa nature ya biashara zao inawavuta kuwatega wateja wapitao ama kwenda hostel, majumbani ama bus terminal. serikali haiyaoni makosa yake, inayaona makosa iliyoyazalisha na kuyashughulikia kikatili sana. waondoe pale bus terminal ili kuepusha kizaaza siku grid ama mtambo wa kufua umeme kwa gesi ukipata hitilafu kubwa.
  Serikali ya ccm ni adui wa wananchi.
   
 10. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  unapofikiria kuwaandalia maeneo utambue nature ya biashara ya kimachinga, usije kuishia kujenga machinga complex kwa mamia ya mamilioni halafu likawa makazi mazuri ya popo.
   
 11. j

  jmnamba Senior Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi niandikapo hapa nasikiliza clouds fm kuwa ubungo terminal maeneo ya nje pale askari wa ffu vs machingas kuondolea eneo lile. Foleni nayo ndio usisema, hayo ndio yaliyojiri muda huu!
   
 12. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,960
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Napongeza jiji na jeshi la polisi.

  Sheria za nchi ni lazima zilindwe kwa gharama yoyote.
   
 13. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni sawa kabisa.
  Huwezi amini pale kuna watu walikuwa wanapiga hela ya nguvu na hawalipi kodi zaidi ya pesa hiyo kuingia kwenye mikono ya wajanja. Kwa mfano hivi karibuni kuna watu walifikia hadi hatua ya kupigana na mmoja aliwahi kupigwa shoka mguuni kwa kugombania kituo. Yaani kuna watu ambao sio serikali, ndio wanadai wao wanamiliki kile kituo cha daladala, na ndio wanaochukua ushuru wa biashara za pale. Na pesa hiyo haiingiii serikalini bali mikononi mwa watu.

  Kuna watu pale huwa wanaweka majenereta na wanawaunganishia watu umeme nyakati za jioni. Kila balbu moja huwa inalipiwa sh. 500. Na jenereta linaweza kuwa linalisha balbu hadi 50. Hiyo ni hela ambayo haina kodi.
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Naamini ilikuwa muhimu zaidi kuiondoa pale grid ya taifa ya umeme, simbion na power plant ya gas ya songas. yale maeneo ni ya makazi na yana watu wengi sana. tuangalie mbali siyo chini ya transforma tu.
   
 15. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Serikali corrupt zinafukuzana mabarabarani na wananchi, haitozi kodi, celtel ilipouzwa kwa airtel serikali kwa makusudi haikulipwa kodi yake stahiki ya bilions of shilings, tunafikiria kodi ya balbu hamsini, kodi ni muhimu lakini iliyo nono imepaswa kuwa kipaumbele.
   
 16. c

  collezione JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  1) Cha kwanza Ajira hamna, huo ndo ujira wao...
  2) Waende wapi wakafanye biashara?? Mmewatengea maeneo mapya,
  Ambayo yatakidhi maslahi yao ya kibiashara? Msije mkawatupa chanika. Wakati mnajua uko wateja hamna.(Poor plan)

  Huwezi tokomeza tatizo. Bila kutokomeza chanzo cha hilo tatizo...
  "Ni sawa na kupiga dawa ya mbu chumbani, wakati milango na madirisha iko wazi."

  My take: ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. Acha JK aruke na ndege kila siku. Wakati watu wanahangaika na maisha magumu.
   
 17. a

  abousalimu Member

  #17
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi hii tabu kwelikweli. Hakuna mipango madhubuti ya kuwasaidia wadanganyika. Lkn inabidi hawa watawala waelewe kuwa solution siyo kupiga na kufukuza!
   
 18. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Tanesco ndio wanapaswa kuweka mitambo yao pembeni ya mji sio mjini
   
 19. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wawaondoe tu na wawapeleke MACHINGA COMPLEX haina watu
   
 20. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Safi na kule Mbagala rangi tatu tusaidieni jamani hakupitiki sababu ya wamachinga na biashara barabarani, lo!!
   
Loading...