Mabomu ya Polisi yatanda Ubungo

Tanesco ndio wanapaswa kuweka mitambo yao pembeni ya mji sio mjini
Hivi miaka 30 iliyopita maeneo kama Ubungo na Mwenge au hata Sinza ya leo palikuwaje?
Hata watu wa Wazo wanataka kiwanda cha saruji kihame kwani kinapulizia vumbi kwenye nyumba zao!
 
Kama Waliojenga mabondeni wamepewa viwanja bure na maji na umeme umepelekwa kwenye maeneno yao,
Kwanini wamachinga wasitafutiwe suluhisho?.......

Kumbuka watanzania tunaishi hand to mouth,......wengi wetu, so watu wengi wanategemea kununua nyanya moja na kitunguu na robo unga wakati wametoka kibaruani.....Now, watu wa namna hiyo hawawezi kwenda sokoni, wanahitaji sehemu ya kununua mahitaji yao while on route to majumbani mwao........Sasa serikali inatakiwa iwe creative hapo kuweka sehemu za machingaz kwenye strategic areas!!!
 
Napongeza jiji na jeshi la polisi.

Sheria za nchi ni lazima zilindwe kwa gharama yoyote.

Mimi naamini hili ni zoezi la zimamoto tu,siku chache zijazo hali itarudi vilevile...
Kwa mnaokumbuka,miaka ya nyuma pale Manzese Darajani hadi Migombani,wachuuzi na wamachinga walivunjiwa sehemu zao za biashara lakini angalia leo hii hali imerudi vile vile!
hata hapo ubungo,hii si mara ya kwanza watu kutimuliwa imefanyika sana.

Serikali inabidi ijitambue kwa kuweka na kusimamia sheria,la sivyo itakua inaharibu fikra na ufahamu wa wananchi wakidhani wanaonewa pindi wanqboadhibiwa kwa ukiukwaji wa sheria.
Imefika wakati Watanzania tufunguke na tuachane na habari ya kushurutishwa. Sheria zinawekwa ili zifuatwe. Ifike mahali watu inapaswa kuheshimu maeneo husika kulingana na hadhi.Kama ni stendi basi na iwe stand na si vinginevyo.
 
ukipingangana an hii operation hata kama wewe ni mwanachadema basi utakuwa ni mpumbavu..tunataka jiji liwe safi lipangwe vizuri...kazi za kufanya zipo nyingi sio lazima kila mtu awe machinga
 
mpango huo ni mwema kwani yale ni maeneo hatarishi, tatizo ni kwa serikali yetu kuwaachia kufanya biashara pale mpaka sasa, wangewatoa wale wachache waanzilishi yasingetokea hayo, na basi wawatafutie mahala pa kufanyia hizo biashara zao la sinyo watageuka kuwa wezi na makahaba hapa mjini.
 
Napongeza jiji na jeshi la polisi.

Sheria za nchi ni lazima zilindwe kwa gharama yoyote.

Sheria za nchi zinalindwa kwa Wamachinga na walalahoi wengine tu? Je mbona nchi ina mijizi na mijambazi tena imejazana serikalini,lakini sheria za nchi hazitumiki?. Nyie Magamba! Time will tell. You have done our lives a misarable,time will come when we will do yours
 
Acha tu sisi wachelewaji wa kazin tumefika saa 3 kasoro kutokana na foleni na kufungwa kwa barabara,ila inapaswa waondoke pale maana ni sehemu hatarishi kwa maisha yao na pia kuna vibaka sana pale kutokana na msongamano wa wafanyabiashara
 
Wanabodi,
Asubuhi hii FFU wamewatawanya wamachinga katika maeneo ya Ubungo mataa, Ubungo maji, stendi ya mkoa na wale wanaofanya biashara katika maeneo ya gridi ya taifa.

Mojawapo ya maeneo ambayo yameathirika ambayo nimeyashuhudia ni ile baa ya Standard ambayo ipo karibu na stendi ya mkoa. Baa hiyo imevunjwa katika eneo lake la mbele ikiwa ni hatua za utekelezwaji wa oparesheni hiyo.

Kuna magari ya FFU na askari kanzu yasiyopungua 30 ambayo yametanda maeneo hayo ya Ubungo. Pamoja nayo yapo mawashawasha mawili ambayo yanasubiri kufanya kazi pale itakapohitajika.

Kwa ujumla hali bado ni shwari na machinga wengi wameingia mitini kwa sasa japo kuna kajikundi kadogo ambacho bado kanajibizana na askari pale maeneo ya mataa. Kajikundi hako kana mabango mawili ambayo yanasomeka:
"Haya ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania?"
"Nyie mnasaini posho mnakula, siye tunakufa na njaa".

Oparesheni hii inafuatia matangazo yaliyokuwa yanatolewa na Tanesco, Tanroads na Manispaa ya Kinondoni ya kuwaondoa watu wanaofanya shughuli katika maeneo ya gridi ya taifa, chini ya njia za umeme na katika hifadhi ya barabara.
Kwa mujibu wa Tanesco, Tanroads na Manispaa ya Kinondoni ilitakiwa wafanyabiashara hao wawe wameondoka katika maeneo hayo kufikia tarehe 01.04.2012 la sivyo wangeondolewa kwa nguvu.

NB:
Kwa wale akina Tomaso: Sikuweza kupata picha kwa sababu kamchina kangu hakana uwezo wa kuchukua picha.

Safi na kule Mbagala rangi tatu tusaidieni jamani hakupitiki sababu ya wamachinga na biashara barabarani, lo!!
 
unapofikiria kuwaandalia maeneo utambue nature ya biashara ya kimachinga, usije kuishia kujenga machinga complex kwa mamia ya mamilioni halafu likawa makazi mazuri ya popo.

Mkuu.. Machinga Complex ni kipimo kizuri cha upungufu wa akili wa viongozi wetu.. Nilisema toka wakati wanaanza matayarisho kwamba kama nia ni hiyo wanayoisema basi itakuwa ni hasara.. Nadhani kulikuwa na personal interests ndo maana wakalazimisha..
Hili la ubungo kwangu mie naona Serikali kabla ya kutoa deadline wangewatafutia eneo mbadala ambalo liko ndani ya biashara.. Au wangeweza hata kununua eneo toka kwa raia na kulitenga kwa ajili ya wamachinga.. Kuwafukuza bila ya kujua wataenda wapi ni kuwaonea na kuwalazimisha kuingia katika vitendo vya uhalifu.. Serikali makini icingewaacha wajazane pale ndo waje kuwaondoa..
 
Sina matatizo kabisa na wazo na hatua za kuifanya miji yetu iwe safi na salama.

HATA hivyo akili yangu inagota ninapoona miongoni mwa wanaofanya hizo shughuli ni vijana walio na elimu ya kidato cha nne, sita na stadi za kutosha kujiajiri endapo wangewezeshwa. Kuna wizara ya Mama Nagu ya Uwekezaji na Uwezeshaji ... sijui ina mikakati gani inayotekelezeka kuhusu vijana hawa.

Katika hili, hawa vijana (Serikali inawaita Wamachinga ... naomba niwaite Wajasiriamali) wananyimwa haki yao ya msingi ya kuishi kwa kufanya kazi ambapo Serikali inawajibika kuwatengenezea mazingira muafaka ya wao kujiajiri.
 
Japo CCM na serikali yake wana matatizo lakini kwa hili la kuwatoa wafanyabiashara sehemu za Road reserve na maeneo sensitive kama hapo kwenye Grid ya Taifa ni jambo la kuungwa mkono

Kama hapo ubungo ilikuwa ni shughuli hasa kama unatembea kwa mguu ilikuwa ni kazi kukatisha hayo maeneo na kama una gari na limepata hitilafu hata sehemu ya kuweka gari pembeni ilikuwa hakuna

lakini Serikali iangalie hili swala la ajira kwa upana wake
maana unaweza kukutana na kijana mwenye nguvu zake anazurura hapo ubungo masaa kumi na mbili akiuza key holders na nail cutters, kwa kijana kama huyu kuna future gani hapo?

Swala la kilimo linachukuliwa kimasihara masihara tu, lakini kilimo cha kisasa ndio sekta ambayo ingeweza kumeza namba kubwa ya watu wasiokuwa na ujuzi katika kazi zinazohitaji utaalamu (nililiona Zimbabwe miaka ya nyuma)
 
Polisi wa Tanzania katika kazi wanazopenda kuzifanya, na huzifanya kwa ufanisi mkubwa sana ni hii ya kuwapiga wamachinga.

Utashangaa wamejaza mabomu ya machozi, risasi za moto na magari ya washawasha kama vile wanakwenda vitani. Pamoja na hasira za kugaragazwa Arumeru, serikali ina hasira za wanaubungo kuikataa ccm na wanatambua kwamba vijana wanazidi kuikataa.

Well, ni wazo zuri kuwaondoa katika hayo maeneo hatarishi lakini wamewaandalia maeneo ya kuwahamishia? kwani magufuli na tanesco hawajui kwamba hao watu wako hapo ili kujitafutia rizki zao!? kwanini wasiwaandalie mahali muafaka pa kufanyia biashara kabla ya kutumia maguvu kuwahamisha?

Tatizo la kukariri kwamba dola ni matumiza ya nguvu, kwani wakiwaambia wateue uongozi wa wamachinga then wajadiliane nao baada ya hapo wafikiee sulhisho kwa manufaa ya pande zote mbli hao watu wangeondoka tena bila gharama kubwa kiasi hiki. Sasa hao FFU watalinda hapo milele? hAO CHINGA Leo kesho na keshokutwa hawatakuwepo lakini polisi wakitoka watarudi tena. lk hide n seek game
 
serikali isiyo na vipaumbela huwa ina deal na mambo ya kipumbafu pumbafu kama haya....
 
Naamini ilikuwa muhimu zaidi kuiondoa pale grid ya taifa ya umeme, simbion na power plant ya gas ya songas. yale maeneo ni ya makazi na yana watu wengi sana. tuangalie mbali siyo chini ya transforma tu.
Kwa kweli hili eneo limegeuka kwua hatari sana. Inashangaza kwua mamlaka zimechukua muda mrefu sana kuwaondoa watu pale. KIla ninapopita, hasa nyakati za jioni siachi kusali kuwa lolote baya lisitokee, maana likitokea, maafa yatakayopatikana hayatasimulika kirahisi
 
Yaani huruma tunawaonea na serikali ndio imeshaamua!
Sasa sijui mwisho wake upo wapi! Mbinu mbadala ilitakiwa ifanyike ili wakitolea hapo wajue atlist wanahamishiwa wapi.
 
Back
Top Bottom