Mabomu ya machozi yapigwa wakati Bobi Wine akifanya kampeni Uganda

Mabomu ya machozi yapigwa wakati Bobi Wine akifanya kampeni Uganda

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,603



Mkutano wa Mgombea Urais wa Uganda kupitia Chama cha National Unity Platform(NUP), Robert Kyagulanyi Ssentamu(Bobi Wine) uliokuwa ukifanyika eneo la Bbaale nchini humo umeshindwa kumalizika vyema baada ya askari wa Jeshi la Polisi kurusha mabomu ya machozi kitendo kilichowafanya wafuasi waliojitokeza kulazimika kuondoka. Bobi Wine alipoona hali hiyo ya mabomu ya machozi alianza kuwaambia wananchi waondoke huku akisema yeye atabaki na kuwa wa mwisho kuondoka kwani anataka dunia ione kinachoendelea nchini humo.

Katika sehemu ya maneno yake alimrushia shutma Mkuu wa Operesheni za Polisi Uganda, Frank Mwesigwa akieleza kuwa afisa huyo akishirikiana na Rais Museveni(ambaye ni mgombea Urais pia wa Chama cha NRM) wanafanya vitendo hivyo ili kumkwamisha katika mkutano wake huo ambao alieleza kuwa ulipangwa kufanyika kihalali. "Nataka dunia ione polisi wa Uganda wametumwa na Frank Mwesigwa kuhakikisha sizungumzi na wananchi wa Uganda"
 
Hawa wazee wapuuzi wanataka kuharibu afrika kwa siasa zao za kungangania madaraka wakati wameshindwa kuwaletea wananchi wao maendeleo.
 
Back
Top Bottom