Ni maeneo ya
Kwangulelo baada ya jamaa mmoja mwenye gari alipomuua dereva wa
pikipiki baada ya kupita gari lake ghafla. (pikipiki ilichomekea gari)
Mwendesha bodaboda alisimama pembeni ya barabara na kupiga magoti kuomba
msamaha kuwa alikuwa anajiokoa kugongwa na gari ligine ila jamaa mwenye
gari alichomoa bastola na kumuua hapohapa. Hayo yalijiri juzi
saa 3 usiku na leo ndio mazishi. Cha ajabu yule dereva
pamoja na kuwekwa kituo cha polisi, aliachiwa as if aliua kuku tu. Leo
wakati wanajiandaa kwa mazishi yule aliyeua kaonekana akiendesha gari
lake na ndipo wananchi na madereva wa bodaboda wakaenda nyumbani kwa
yule muuaji na kuchoma nyumba yake na kuharibu kila kitu. Baada ya hayo
kujiri wakawa wanaelekea nyumbani kwa wafiwa na kumbe taarifa
zimeshafika polisi ndipo wakaja kujaribu kutawanya watu... Wananchi
wamekataa wanahoji kisa cha mtu kuua na kuachiwa usiku huohuo. Wakafunga
barabara kuu ya Moshi-Arusha. Polisi walipoanza kupiga mabomu ya
machozi ndipo wananchi wakabeba mawe na kuiweka gari ya polisi kati
kabla hawajaanza kupambana na polisi magari mengine ya FFU yaliyokuwa
mahakamani kwenye kesi ya Lema yakaenda kutoa sapoti na ndio kisa cha
MABOMU. Magari sasa yanatumia barabara ya
Kwangulelo-Kijenge.
Ni maeneo ya Kwangulelo baada ya jamaa mmoja mwenye gari alipomuua dereva wa pikipiki baada ya kupita gari lake ghafla. (pikipiki ilichomekea gari)
Mwendesha bodaboda alisimama pembeni ya barabara na kupiga magoti kuomba msamaha kuwa alikuwa anajiokoa kugongwa na gari ligine ila jamaa mwenye gari alichomoa bastola na kumuua hapohapa. Hayo yalijiri juzi saa 3 usiku na leo ndio mazishi. Cha ajabu yule dereva pamoja na kuwekwa kituo cha polisi, aliachiwa as if aliua kuku tu. Leo wakati wanajiandaa kwa mazishi yule aliyeua kaonekana akiendesha gari lake na ndipo wananchi na madereva wa bodaboda wakaenda nyumbani kwa yule muuaji na kuchoma nyumba yake na kuharibu kila kitu. Baada ya hayo kujiri wakawa wanaelekea nyumbani kwa wafiwa na kumbe taarifa zimeshafika polisi ndipo wakaja kujaribu kutawanya watu... Wananchi wamekataa wanahoji kisa cha mtu kuua na kuachiwa usiku huohuo. Wakafunga barabara kuu ya Moshi-Arusha. Polisi walipoanza kupiga mabomu ya machozi ndipo wananchi wakabeba mawe na kuiweka gari ya polisi kati kabla hawajaanza kupambana na polisi magari mengine ya FFU yaliyokuwa mahakamani kwenye kesi ya Lema yakaenda kutoa sapoti na ndio kisa cha MABOMU. Magari sasa yanatumia barabara ya Kwangulelo-Kijenge.
Huyo aliyeua mwenzake na kuachiwa na polisi ni nani?Ni hata mimi nipo eneo la tukio. Pesa ipo juu ya sheria kwa serikali ya ccm.
Wewe ulikuwepo yote yakijiri au umehadithiwa tu, maana hiki kisa chako kimekaa kipaukwa pakawa, kimepambwa kumfanya mwendesha gari ni Shetani mmoja mbaya sana.
Visa namna hivi huwa siviamni mpaka niipate picha kamili, hii yako siiamini mpaka sasa, sijui baadae.
zomba nakushauri kuendelea kusoma hii thread utakuta watu wengine watakaokanusha au kuikubali taarifa hii. Hata kama sio hapa jaribu kusikiliza radio au hata magazeti. AhsanteWewe ulikuwepo yote yakijiri au umehadithiwa tu, maana hiki kisa chako kimekaa kipaukwa pakawa, kimepambwa kumfanya mwendesha gari ni Shetani mmoja mbaya sana.
Visa namna hivi huwa siviamni mpaka niipate picha kamili, hii yako siiamini mpaka sasa, sijui baadae.
Ndio maisha ya arusha hayo ambako 99% ni chadema.
Ndio maisha ya arusha hayo ambako 99% ni chadema.