Mabomu ya Gongolamboto....Jeshi lilijua???!!!!!!

Mabomu ya Gongolamboto....Jeshi lilijua???!!!!!!

Al Zagawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Posts
2,528
Reaction score
1,621
sijuzulu.....ni maneno ya waziri wa ulinzi akinukuliwa na magazeti.

hakuna atakayejizulu maana katika jeshi hakuna siasa....ni maneno ya ofisa wa jeshi akinukuliwa na magazeti.

poleni kwa maafa makubwa yaliyowakuta......maneno ya mkuu wa kaya, aliongea baada ya mkutano na baraza lake la ulinzi na usalama. hayo ni maneno aliwaambia wanajeshi...hakutaja ni kiasi gani cha damage kwa jeshi ikiwa ni mali au vifo tofauti na mbagala ambapo walau tulijuwa idadi ya wanajeshi waliopoteza maisha.

ukija huku mitaani(time will tell) yapo maneno kuwa jeshi lilijua habari ya tukio hilo na wao walijiandaa mapema kusalimisha mali na uhai wao. Mfano wa stori za mitaani ni hizi mbili ambazo nimezipata ofisini:

1. kijana mmoja anasoma KIU(dady wake ni mjeshi)...alisikika akimwambia mwenzie wawahi kuondoka maeneo ya chuoni kule goms kwa vile siku hiyo kungetokea milipuko ya mabomu eneo hilo...wapo waliobisha lakini kweli ilipodhihiri uongo ulijitenga

2. mama mmoja huko tabata ambaye ni mjeshi alirudi hom mapema akahamisha familia kwa mshangao wa majirani...ilipofika usiku na kizaizai kutokea..wenye akili wakatambua...alaa ndiyo maana alifanya vile...

ni vijimaneno tu...ikiwa vina ukweli basi wakati utaongea laa vitajifia a natural death

nawasilisha!:wink2:
 
Nimeshasikia habari kama hii lakini sijamsikia mtu ambaye ameambiwa na ndugu au jamaa yake mwanajesi zote ninazosikia ni "..kuna jamaa ana ndugu yake mwanajeshi...." na sio "..mimi ndugu yangu mwanajeshi aliniambia..."
Sina hakika kama hizi tetesi ni za kweli unless aje mtu humu aseme wazi kuwa aliambiwa na ndugu yake mwanajeshi kuwa kuna tukio lingetokea.
 
ninaweza kukupa namba za simu za mtu ambaye kaka yake alimjulisha aondoe familia. sema kama uko tayari mkuu.
 
Hata mimi nimeskia hivyo hivyo yawezekana ni kweli
 
mm boss wng aliambiwa ahame tangu saa 10 jioni alipigiwa simu na rafiki yake ambaye ni mjeda!!
 
Back
Top Bottom