Mabiringanya ya nazi

farkhina

Platinum Member
Mar 14, 2012
14,568
16,906
Wengi wetu tumezoea nyanya chungu za nazi,biringanya pia likipikwa na nazi huwa na ladha nzuri pia.

Mahitaji:

Biringanya kata dogo dogo wek katika maji ya baridi (hii husaidia biringani kutobadilika rangi sana na kua jeusi)

1.Nyanya

2.Kitunguu saumu na maji kiasi vitwange na chumvi.

3.Tui la nazi zito/bubu.

4.Tui jepesi.

Namna ya kutaarisha:

1.Weka biringanya lako katika sufuria

2.Katika nyanya nyembamba na weka saumu na kitunguu maji kilichotwangwa.

3.Mimina tui jepesi lifikie nusu ya wingi wa mabiringanya (ili lisivurugike) chemsha hadi kukaribia kuwiva.

4.Weka tui bubu na subiri kidogo then epua.

5.Weka mezani tayari kwa kuliwa.

6.Zuri kulia na wali,chapati au upendavyo.
 

Attachments

  • 1422157475552.jpg
    1422157475552.jpg
    35.1 KB · Views: 475
  • 1422157499520.jpg
    1422157499520.jpg
    73.9 KB · Views: 484
Wacha siku nijaribu. ..hili hua nafanya la kukaanga tu ndo nalopenda

Kuna mtu siku na nunua hilo biringani nkamwambia nalipika kwa nazi hili akanishangaa ati hajawahi kuskia siku nkalipika hili nkamualika alikula akalipenda aliposhiba nkamuuliza unajua umekula nini? Akajibu hata sikujua naona kitu kitamu tu lol nkamwambia biringanya akashangaa
 
Biringanya la nazi tamu sana, ni kama nyanya chungu vile. Unakoleza nazi hadi linatoka kifuta.
farkhina kama utaweza lipike likiwa halijamenywa, linakua tasty zaidi.
 
Last edited by a moderator:
biringanyi napenda , hii ya kuunga kwa nazi sjawahi onja, ngoja njaribu. Imenivutia Mashaallah
 
Mmh mie hata liungwe na ukwaju nitakula basi tu tena nakula nimelikuta kwa watu mi sijawahi nunua kwangu nikapika teh

Mie nna hilo tatizo kwenye Kabeji (Sijui kama nimepatia jina) tangu mdogo kabisa sielewani nayo kabisa, japo sasa hivi najitahidi kuzipenda na nnaona maendeleo yanaridhisha!!!!!
 
Mie nna hilo tatizo kwenye Kabeji (Sijui kama nimepatia jina) tangu mdogo kabisa sielewani nayo kabisa, japo sasa hivi najitahidi kuzipenda na nnaona maendeleo yanaridhisha!!!!!
Mie ni biringani, cabbage na kisamvu hizi mboga hapana kwakweli, tena mara mia na cabbage siku hizi ndo nakula kula zamani nlikua sigusi kabisa
 
Mie ni biringani, cabbage na kisamvu hizi mboga hapana kwakweli, tena mara mia na cabbage siku hizi ndo nakula kula zamani nlikua sigusi kabisa
mwalimu unakosa mengi hasa kwenye kisamvu...kisamvu cha nazi tena kichanganywe na vijimbaazi kwa mbaaaali..lol ntakula mpaka kijungu kilicchopikiwa kipasuke. jitahidi utazoea kidogo kidogo. mie kunde na magimbi mhhh nala tu ila hayapandi katu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom