Kupika mihogo ya nazi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Mahitaji;
  • Tui la nanzi (Tui zito na tui maji) tui maji ni mchujo wa pili wa nazi
  • Nyanya 2
  • kitunguu
  • mfuta ya kula kiasi
  • Mihogo uliomenywa na kukatwa vipande vidogo vidogo
  • Chumvi
Weka mihogo kwenye sufuria ioshe, kisha kaanga kitunguu mpaka kiwe rangi ya kahawaia, tia nyanya iliyokatwakatwa kaanga hadi iive.

Weka mihogo kisha weka tui maji size mpaka itakapoziba mihogo yako na chumvi utaacha vichemke mpaka utaona inaanza kukaukia na mihogo inaiva vizuri.

Tui maji likishabakia kidooogo na mihogo yetu ikishaiva, unaweka tui lako zito na kuacha vichemkie tu kidogo mpaka liive na kwa uzito unaotaka mwenyewe.

Ukiona uzito wa rojo imetosha upendavyo unaipua tayari kwa kula. Muhogo raha yake uupate na samaki wa kukaanga, au uduvi👌🏻

Ukitaka kuchanganya uduvi kwenye muhogo wako basi unauosha vizuri alafu unauweka kabla ya kutia bubu yaan likishaanza tui maji kukauka kauka unauweka unaacha uchemkie halafu unaweka tui bubu.

1679731020037.jpeg
 
pia

menya mihogo yako
kata vipande vidogo vidogo huku ukiutoa ule mzizi wa katikati
ioshe vizuri kisha iweke katika sufuria unayotaka kupikia
kuna nazi chuja tui bubu pembeni lile tui la pili lichujie kwenye mihogo
hapa hakikisha tui lipo level moja na mihogo sio tui pwaa katia kitunguu maji kiasi kisha bandika jikoni
maji yakianza kukauka mimia tui lako bubu acha lichemke kiasi liive kisha tegua,

badala ya kuweka kitunguu waweza miminia duvi humo sio lazma samaki wa kukaanga hata wa kuchemsha na mbirimbi, embe au limao na chumvi vikaukie mtegua utakula had uvimbiwe


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom