Mabinti wahitimu wa vyuo Amkeni

Habari za muda huu wana jamvi


Naandika uzi huu nikiwa kwenye daladala nikirejea nyumbani kutoka kwenye "mihangaiko" ya Kila siku
Ndani ya daladala nmekaa karibu na wakina mama wawili wakipare(nimesikia wakiongea kipare). Hawa kina mama wanaelezana kuhusu tabia mbaya za mabinti zao waliohitimu vyuo ambao umri unaenda na hawajapata kazi Wala hawajachumbiwa.

Kinachowauma zaidi ni tabia ya Hawa "mabinti" kushinda ndani na kutizama movie muda wote badala ya kutoka nje watembee tembee huwenda wakakutana na "ngekewa".

Namnukuu mmoja akisema "Yani Bora wa kwako hata kanisani anaenda, Mimi huyu wangu hatoki hata kwenda dukani hataki, hana hata marafiki akatembee huko anaweza akapata mume njiani lipo lipo tu"

Wadogo zangu wa kike jitahidini kutembea tembea mama zenu wanataka muolewe mtazeekea ndani.
Nipe namba za hao mabinti...
 
Ushauri murua. Kwa kuwa wamehitimu vyuo na wanadoda nyumbani bora wachangamkie fursa ya kuolewa chapchapu wapate watoto huku wakiendelea kutafuta ajira tayari wakiwa ndani ya ndoa, watakuwa wamepunguza stress upande mmoja huku wakijishughulisha na ujasiriamali/kilimo. Ila waolewe na wanaume ambao wataheshimu taaluma zao na watawapenda kwa dhati
Nakazia ujumbe wako mkuu
 
Wangejua wenzao kwa miaka mitatu/minne chuo walishaolewa nakuachika mara 3 + michepuko juu hata wasingesema.

Hao ni wanandoa wastaafu. Ni akina Shusho Jr.

Kwa tabia ninazoziona vyuoni, nitakuwa wa mwisho kushawishika kuoa graduate, japo wapo wachache sana waliotulia.
 
Back
Top Bottom