Kaizer
Platinum Member
- Sep 16, 2008
- 25,320
- 17,823
Wanawake wanajua wanachotaka ila wengi ni wazito kusema wanataka nini kwa wapenzi wao. Hata wale wepesi wa kusema huwa wengi hawaridhiki na wanachopewa.
Mfano mwanamke anaweza akawa amechoka na shida ya usafiri akataka anunuliwe japo kivitz ila utakuta ni ngumu kumwambia mpenz wake hali ya kuwa anajua mpenz wake ana uwezo wa kumnunulia. Ikitokea njemba ya pembeni amenunua bila kuombwa unakuta anaanza kuhamisha upendo kwa njemba kidogo kidogo.
Mwingine anaweza akapewa kivitz akatamani angepewa range kabisa.
Pia tunapowalalamikia wanaume tunapenda mtuoneshe huruma ila wanaume mnapolalamikiwa mnapenda kutatua tatizo bila kuonesha huruma au kuonesha kuwa unafeel vile mpenzi wako anajifeel.
Mfano, mwanamke anakupigia simu anakwambia anaumwa. Wanaume wengi huuliza unaumwa nini?, umeenda hospitali? Akijibiwa sijaenda utasikia nakupitia hapo au nakutumia mtu aje akuchukue akupeleke hospitali.
Wanawake wengi huwa tunatarajia kauli tofauti kabla ya hiyo ambayo hutupa relief. Mfano "pole mpenzi wangu, au ni uchovu tu, unaumwa sana baby wangu?, jaribu kupumzika kidogo nitakupigia baadae kidogo nione unaendeleaje. Pole mamii yaani hadi na mimi nimekosa raha."
hizo sentesi zinaonesha namna gani ulivyoguswa na tatizo, sio lazima useme kama zilivyo ila katika hatua ya awali onesha namna ulivyoguswa halafu ndio ukimbilie kusolve tatizo.
Ni hayo tu kwa sasa.
good analysiss but what are the LIMITS?