Mabillion kuwajibu upinzani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabillion kuwajibu upinzani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mvaa Tai, Nov 7, 2011.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Leo nimeharibu siku yangu nimepita maeneo ya Hazina pale nikamsikia Afisa mmoja akizungumza na mwenzake kwa uchungu sana. Vitu muhimu nilivyo vi-note ni kama ifuatavyo.

  1. Kila wizara imelazimishwa ifanye maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, wakati serikali ipo katika hali ngumu sana kifedha.
  2. Wizara zoote hazikubajeti pesa kwa ajiri ya shughuli hii
  3. Kila wizara imeamuliwa iangalie katika vifungu vyake itatoa wapi pesa na shughuli za kifungu husika zisimame mpaka bajeti ya mwakani
  4. Mpaka sasa kwa wastani kila wizara inatumia zaidi ya Billion mbili kwa shughuli za kuadhimisha Miaka 50 ya uhuru
  5. Inasemekana viongozi wa CCM wamekasirika kuambiwa kwamba hawajafanya lolote tokea tupate uhuru.

  Naumia sana nikijiuliza: Hivi jumla tuna wizara na Taasisi ngapi za Serikali? Mpaka hili zoezi la kujisafisha liishe jumla itatumika bei gani? katika kipindi hiki ambacho uchumi unadorora ni kwanini hizo pesa zisielekezwe katika maeneo yatakayo punguza makali? kama vile kuongeza ruzuku kwa wazalishaji na wasafirishaji bidhaa nje ya nchi.

  Kwanini wataalamu wetu Serikalini wanaendeshwa kiasi hiki na wana siasa? Hivi CCM wanaona ni sawa kusheherekea miaka 50 ya uhuru huku ukienda madukani unakutana mpaka na maziwa freshi, mboga za majani na matunda kutoka nje ya nchi?

  AAAAAAAAAGR!!
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mkuu hujaamka nazo kweli ? Nimesoma sijaelewa kitu kimoja , ujumbe uko clear kichwa cha habari mbona kimekaa kilevi levi ?
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Duh! kweli jumatatu huwa ni ya 'blue' ..... mkuu kunywa siku za Ijumaa na Jumamosi, kwa Jumapili madhara yake ndiyo haya. Tena wewe si wa bia za kawaida bali konyagi poli.
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180

  Halafu tunamlaumu Jairo, haka kanchi kameshakufa kanatembea kwa kudra za mwenyezi Mungu. Hapo wajanja wanakamua tena mshiko, si wameruhusiwa kufanya hivyo. Nchi ya kukurupuka hii, yaani mwaka jana wakati wanabajeti hawakujua kuna maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru?
   
 5. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,164
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280


  Hapo penye RED, TOOTHpick Toka CHINA. Kwa nini Shilingi isiporomoke. Mmekalia politics mkijua ndio zinazowapa ulaji.
   
 6. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  nenda soko la ubungo, mwenge, buguruni jioni ni sandals za kichina ambazo zinaharibika baada ya wiki, TZ nourmer!!
   
 7. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viongozi legelege watatengeneza Serikali legelege hiki ndicho tukionacho
   
 8. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Kipaumbele cha mafisadi wa ccm na serikali yao ni maonesho tu. hata kama 90% ya vinavyooneshwa ni vya uongo
   
 9. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jamani mbona anaeleweka vizuri sana??? Nyie msioelewa ndiyo mmeamka nazo!!! Ahsante sana Mkuu kwa kutuletea nyeti hizi!!! Wapinzani wapige kelele nyingi sana bungeni na majukwaani kupinga ubadhirifu huu!!
   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  mi nilishasema humu mwakani mwez wa pili nchi itakuwa haina pesa kabisa..
   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Lunyungu naamini uwezo wako wa kufikiri ni mkubwa tuu hebu jaribu kusoma point namba5 alafu oanisha na kichwa cha habari usipoelewa ni-PM kwa ufafanuzi zaidi
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  serikali ya kisela hata mambo yake huenda kisela sela tu
   
 13. L

  Lua JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ndiko tulikofikia kwa sasa!
   
 14. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Msishangae, Upeo wa ccm umefikia kikomo. Dawa ni siku ya uhuru tufanye maandamano makubwa nchi nzima kupinga ubadhirifu wa fedha zetu kulazimisha kusherehekea kisicho sheherekeka. Tunataka fedha zetu zitumike kwenye maendeleo siyo anasa. Polisi watakuwa bize na hawataweza kuzuia maandamano yote. Mwisho wa siku kitumbua kitaingia mchanga na Ujumbe utafika kwa hao wageni watakaokuja.
   
 15. m

  mang'ang'a JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Mtoa mada kaeleweka vizuri tu, nafikiri hawa wanaompinga ki wale TASK FORCE wa mafisadi wa kitengo cha vuruga JF msg sisi tumeielewa bana
   
 16. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  mkuu mbona iko wazi? vipi maandalizi ya miaka 50 yanaeneleaje?of cource tunakivunia AMANI na UVUMILIVU!
   
 17. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #17
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Maadhimisho yanafanyika kila mkoa na wilaya ambapo mabanda hujengwa, kupambwa na kwekewa watumishi humo kufanya maonyesho. Nahisi hii linaongezea kwenye bilioni ulizozitaja kwa kila wizara. Du Kama kupanga ni kuchagua hapa tumeingizwa "vichakani"
   
 18. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #18
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  hili suala la kuwaita hawa jamaa wajanja kunafanya waonekane wana akili wakati wana resources zote lakini hawezi hata kupanga wazitumieje!
  'Wajanja' ni akina Bill Gates, Steve Jobs, Masoud Kipanya na wajasiriamali wengine wanaoweza kuplan na kusimamia miradi yao lakini hawa ni wajinga na wezi.
   
 19. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #19
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Me nimemuelewa nazan walioamka nazo ndo hawajamuelewa
   
 20. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,968
  Trophy Points: 280
  hata mie naungana nawe hii ina chenga na sijaamka nazo maana hata coka huwa sinywi. Nilitegemea mabililioni yametengwa kuwajibu wapinzani kuhusu jambo fulani.
   
Loading...