Mabillion kuwajibu upinzani!

Leo nimeharibu siku yangu nimepita maeneo ya Hazina pale nikamsikia Afisa mmoja akizungumza na mwenzake kwa uchungu sana. Vitu muhimu nilivyo vi-note ni kama ifuatavyo.

1. Kila wizara imelazimishwa ifanye maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, wakati serikali ipo katika hali ngumu sana kifedha.
2. Wizara zoote hazikubajeti pesa kwa ajiri ya shughuli hii
3. Kila wizara imeamuliwa iangalie katika vifungu vyake itatoa wapi pesa na shughuli za kifungu husika zisimame mpaka bajeti ya mwakani
4. Mpaka sasa kwa wastani kila wizara inatumia zaidi ya Billion mbili kwa shughuli za kuadhimisha Miaka 50 ya uhuru
5. Inasemekana viongozi wa CCM wamekasirika kuambiwa kwamba hawajafanya lolote tokea tupate uhuru.

Naumia sana nikijiuliza: Hivi jumla tuna wizara na Taasisi ngapi za Serikali? Mpaka hili zoezi la kujisafisha liishe jumla itatumika bei gani? katika kipindi hiki ambacho uchumi unadorora ni kwanini hizo pesa zisielekezwe katika maeneo yatakayo punguza makali? kama vile kuongeza ruzuku kwa wazalishaji na wasafirishaji bidhaa nje ya nchi.

Kwanini wataalamu wetu Serikalini wanaendeshwa kiasi hiki na wana siasa? Hivi CCM wanaona ni sawa kusheherekea miaka 50 ya uhuru huku ukienda madukani unakutana mpaka na maziwa freshi, mboga za majani na matunda kutoka nje ya nchi?

AAAAAAAAAGR!!

Hiki kichwa cha habari kipo sawa ila kinashindwa kusaport habari yaani ni mpaka usome habari yote ndo utaiunga ni heading otherwise hii ni issue nyeti na muhimu sana. Yule jamaa alyetusaidia kuiba barua ya kina jairo naomba na hii atusaidie
 
Wasiomuelewa mleta hoja ndiyo wale wale, wao ni wanaufaika wa hayo mamilioni yanayozungumziwa na kazi yenyewe ndiyo hii wanayoifanya, kutetea ufisadi kwa nguvu zao zooooooooooooooooote.
 
Back
Top Bottom