Mabilioni Uswiss: Mbunge yeyote anayedai anayafatilia, anaudanganya umma

Pa kuanzia ni kufuatilia historia ya jinsi suala hili lilivyoanza na jinsi wanasiasa walivyojiingiza. Ni kweli kabisa mtu mmoja ambaye si mamlaka husika kuweza rejesha pesa zilizofichwa nje ya nchi. AG alishawahi kuelezea suala hili lakini watu wakampa za kwake hapa JF na kuonekana kwamba si mzalendo.
Hata kama ni kufuatilia mfumo, nao pia hauwezi kubadilishwa nje ya mamlaka husika.
 
Tangu alipoinuka Zitto nakujitangaza kuwa eti anafuatilia kitu kiitwacho mabilioni ya uswisi nilibaki mdomo wazi nikiwasikitikia wale wanaomwamini kwa ulaghai wake,

Kwakuwa ninaakili timamu na ninafahamu vema taratibu za ufuatiliaji wa pesa yoyote iliyo nje ya nchi hasa nikiangalia sheria za nchi yetu na sheria za uswisi, nilibaki kustaajabu tu uzandiki wa kijana huyu wa mwandiga,

Jamani watanzania msiwe wajinga na wapumbavu, kama jamuhuri na vyombo vya dola nchini havijaamua kufuatilia suala hili hata angekuja Yesu na Mtume Mohamed hawataweza kuingia uswisi na wakafanikiwa kurejesha pesa iliyoingia kwa njia haramu nchini humo.

Tuache kudanganyana kuwa Zitto anafatilia mabilioni uswisi. Kodi ya wananchi inatafunwa kwa viini macho kama hivyo.

Zitto na kundi lake wanatambua wazi kuwa hapa tz kuwa watanzania kama Yericko Nyerere wanaijua michezo yao yakipuuzi wanayowafanyia watanzania na mimi kwa moyo safi kabisa huwa sikubali kudanganywa na mtu mhuni kama Zitto,.

Kama serikali husika haitaki fedha zilizolimbikizwa huko ughaibuni zirudishwe nyumbani kwao hilo halitawezekana; mfano unaotolewa wa fedha za Abacha kurudishwa huko Nigeria ni kwa sababu yuke mama waziri wao wa fedha alisimama kidete kufuatilia mpaka baadhi tu ya hizo fedha wakarudishiwa. Hapa Tanzania tulikuwa na zile fedha za RADAR ambazo mahakama ya Uingereza iliamuru zirudishwe ndio hizo zilizorudi lakini VIJISENTI vya wakina Chenge na Idirs Rashid serikali wala haikujishuhulisha kuhakikisha kuwa zile fedha zinarudi!!!! Watawala wanajuana hivyo hawawezi kuumbuana.
 
hata hujitambui ndio maana umeamua kubwabwaja tu bila mpango.nani kakwambia yeye biafsi anafuatilia pesa zirudi kama hutumiki kisiasa kupotosha kwa maslahi yenu binafsi.me najua umemlenga nani katika porojo zako hizo hapo juu.Zitto anadeal na mifumo inayowezesha hao wezi akiwepo mw/kiti wenu kupeleka hizo pesa huko ng'ambo.kuna viongozi wengi ni mafisadi sio ccm pekee hata huko cdm na wameweka mabilioni huko ng'ambo coz ya mifumo mibovu ya kudhibiti pesa sio Tanzania tu bali all over the world so jiangalie sio unatumika tu.kama serikali haitaki kuzifuatilia so what?tuziache?hata hizo billions unazosema unadhani hao wafadhili wamekurupuka tu bila kupata taarifa sahihi kuzihusu?huyo unayemuona hafai anakwenda nchi kwa nchi kuwaambia hao wafadhili jinsi pesa wanazotoa kama msaada na mkopo wanavyogawana mafisadi wachache na kuzilimbikiza ughaibuni....unajua kinachofuata baada ya hapo?ndio hizo shinikizo kutoka kwa wadau wa maendeleo ya Africa.wanazibana serikali za Africa kuweka sera za kusimamia pesa vizuri kwa manufaa ya wananchi.Anachofanya Zitto ni kupuliza kipenga cha mwizi mwizi then wanaibuka watu na kumkimbiza mwizi hadi wamkamate.Tatizo linakuja unapopiga kelele za mwizi ukiwa ndani ya kuni linalonufaika na huo wizi watakuharibia tu kwa namna yoyote ile ikiwemo kukugeuzia kibao kuwa wewe ndio mwizi mwenyewe.I remember siku ya mwaka mpya 2003-2004 enzi hizo nilikuwa nimepanga maeneo ya magomeni mapipa.nilienda kusherehekea kukaribisha mwaka mpya(mwaka pekee ambao sikwenda mkesha kanisani) kwenye ukumbi mmoja huko city center unamilikiwa na mdau flani wa chama cha siasa sasa wakati narudi zangu mida ya kuelekea saa kumi alifajiri nipo pombe vibaya nanesa tu dunia naiona yangu.nimeshushwa na gari karibu na mtaani nikawa napiga zangu step kuelekea home,nikapita kundi la kwanza la vijana wako bize kinoma na stori,nikapita kundi la pili sasa wakati nalifikia kundi la tatu nikahisi hatua za kunyata nyuma yangu.hata sikupata muda wa kugeuka mwanawane ilipita roba ya mbao shingoni.kama hujawahi fanyiwa hivyo usiombe,maana nilipojaribu kukukuruka tu si misumari ikawa inaingia shingoni?ikabidi nitulie tu(niwe mpole) wafanye yao.walisanya kila kitu wakanivua hadi raba zangu kaliii nilikuwa nazipenda sana.hapo lile kundi la tatu wanaangalia mchezo unavyoendelea.....sasa wajamaa walivyomaliza kuchukua vyao(hapo pombe ishakata) wakatawanyika ile nimekurupuka napiga kelele za mwizi mwizi wa kwanza kufika eneo la tukio ni lile kundi la tatu tena fasta,walichohakikisha ni kwamba naacha kupiga hizo kelele like tumekuja kukusaidia tueleze wamekuibia nini?akili ikanicheza nikajiuliza hawa jamaa walikuwa karibu hawajanisaidia sasa wakora wamekimbia ndio wanajitokeza kusaidia,nikajumlisha moja na mbili nikaconclude ni wale wale tu wanataka wajue wamepata ngapi.nikaropoka wamenipora zaidi ya laki mbili(enzi za mkapa laki mbili hela nzuri) simu na blah blah ili wakapambane vizuri mbele ya safari.baada ya kusikia hivyo unadhani kuna aliyebaki?tena cha ajabu walipita njia tofauti na walizoingilia hao walioniibia.nikajua wanafahamu watakutana wapi.but since walikuwa wengi na ilikuwa usiku sikujisumbua hata kuwafuata nikaondoka mdogo mdogo kuelekea home.wewe nakuchukulia upo kwenye kundi la tatu la hao wanaojitokeza kukupoteza usikonsetrate kwa wale waliokuibia ili kupoteza ushahidi wenye nia njema wasijitokeze kusaidia kukamata mwizi.USHINDWEEEEEEEEEE NA ULEGEEEEEEEEE!!!!!
Uzito-phobia unakusumbua
 
Pa kuanzia ni kufuatilia historia ya jinsi suala hili lilivyoanza na jinsi wanasiasa walivyojiingiza. Ni kweli kabisa mtu mmoja ambaye si mamlaka husika kuweza rejesha pesa zilizofichwa nje ya nchi. AG alishawahi kuelezea suala hili lakini watu wakampa za kwake hapa JF na kuonekana kwamba si mzalendo.
Hata kama ni kufuatilia mfumo, nao pia hauwezi kubadilishwa nje ya mamlaka husika.

Hapa tuueleze umma kwamba hii issue inahitaji mageuzi ya kiutawala ndo tuweze kuweka mfumo mzuri wa mihimili kusimamiana vizuri. Mfano bunge likitoa maamuzi serikali iyafatilie
 
kuna vitu nadhani zzk kabwe alikua anapewa tips nzito na serikali/usalama wa taifa ili kumjenga kisiasa, ukweli wamefanikiwa sana katika hilo cause watanzania kwanza hua hatuna kawaida ya kuhoji kitu/vitu, hili la watu kuficha pesa uswisi or else where sio jambo la ajabu kwa nchi zinazoongoza kwa ufisadi, tulimkubali sana zzk though baadhi ya watu walimtaka sana ataje majina, alikataa hadi leo kumbe na yeye hua kuna pesa inatumwa kwake kupita german.

Nakubaliana na mleta uzi, mtu 1 tu hawezi kua na access hiyo hata kidogo vinginevyo iwe kwa miujiza au kujua nani ana tsh/dolla/paund or euro kiasi gani, kuzirudisha tunadanganyana, mtu 1 hawezi, hata pinda akitaka still naamini hawezi!

nakubaliana na wewe mkuu.huyu jamaa huenda alikuwa anajengwa kisiasa ili wanachadema wamkubali iwe rahisi kumpindua mwenyekiti wa sasa na kufanya cdm kuwa ccm d.hapa naona mungu ameingilia kati akafumaniwa akiwa kwenye mchakato.na wahariri wa baadhi ya magazeti watakuwa wanahusika.wanaandika sana pumba zake kwa maandishi makubwa kwenye kurasa za mbele za magazeti yao.wanacdm muwe waangalifu na magazeti mnayosoma.wahariri badilikeni sasa.
 
mtasema sana hamuwezi ziba nyota ya zitto na wewe ni chadema family

Twende polepole mkuu, hivi mtu kama mtu anaweza kufuatilia pesa/uhalifu uliofanywa nje ya nchi? zitto alikuwa "anafuatilia" mabilioni ya uswis kwa rungu la uenyekiti wa poac ama? poac ina meno ya kuvuka mipaka ya nchi kufuatilia uhalifu?
 
Kufuatilia pesa Uswis na kwingineko ni Uzushi ambao unapotosha umma wa watanzania. Ni sinema hiyo kama tu ya jems Bond na zingine
 
mtasema sana hamuwezi ziba nyota ya zitto na wewe ni chadema family

Hakuna anayehangaika kuzima nyota ya mtu hapa, tena ni nyema maana itaibukia kwingine, hivyo asiwe na amani wala asipige kelele kama anavyohangaika sasa.
 
Mkuu,
Kwa kweli mimi sijui kama hao wamo au hawamo. Ni vibaya kutuhumu watu hasa kama hatuna ushahidi wowote.

Watu labda wanachanganya mambo mawili hapa, kuna kuzirudisha pesa zilizofichwa huko na pili ni kuwajua walioficha huko.
Zitto hawezi kufanya la kwanza ila la pili akiwa na mtandao wa wabunge wa nchi zingine hilo linawezekana. Si ajabu hata sasa ana majina ila kuyatoa ndio ngoma nzito.

Lakini hata ukimjua aliyeficha kurudisha ngumu.

Mtanzania ina maana haya majina hapa ni ya kilaghai?

ANGALIA HAPA

Copy kwa Mshombsy
 
Kweli nimeamini maneno ya JK Chadema wanafiki wapo wengi. Wakati Zitto anaanza kazi hii mlikuwa kimya, leo kwa sababu ya maamuzi ya kipuuzi mnajaribu kumchafua. Wenye akili wataelewa anachofanya na wanafki endeleeni na unafiki wenu. Na natumaini kama alivyofanikiwa kufikia kuilazimisha serikali kuja na sheria ya madini mpya hata hili ninaimani atatusaidia kuja na mwafaka mpya hata sheria mpya ya uhamishaji fedha na ukwepaji kodi kimataifa. Zitto endelea kufanya ya taifa achana na wanafiki.
Anyway mkimaliza na Zitto mtuambie freeman Mbowe atatoa lini mkanda wa mauaji ya Arusha ili haki itendeke kwa familia za marehemu.
 
Last edited by a moderator:
Mtanzania; hapa ni kwamba anasema anafuatilia mabilioni ya Uswiss kitu ambacho hawezi kimamlaka.

Swala la kuwataja anaweza ndio kupitia Bungeni na alipokuwa Tabora wiki 3 zimepita alisema kikao kijacho cha bunge. List haiwezi kupatikana kwa mtandao wake na wabunge wa nje; list inaweza kupatikana toka serikali yetu na ninakuhakikishia hiyo list wanayo tayari serikali ni mtu tu anahitajika kuichomoa kwa siri.

Tatizo tunaaminishwa na mtandao wa kimataifa kitu ambacho ni kibaya. Hao wabunge mnaowasema hawajapitisha sheria nchini mwao kufanya wateja wa nje wote wakiweka hela kwenye mabenki iwe automatic kuitaharifu nchi mteja anakotoka, sasa leo mnasema mtandao wa kimataifa wa wabunge.

Hao wabunge wanaangalia maslahi ya nchi zao na si wabunge wa dunia. Hawawakilishi dunia.
 
Last edited by a moderator:
Jaman kabla zitto hajatuambia nan alyetuambia..nyote wanafk tu,nyote mnamuogopa zto face to face..mkubal zto watanzania wamkubal,na natangaza waz#yeriko nakuchukia bas tu
 
Jaman kabla zitto hajatuambia nan alyetuambia..nyote wanafk tu,nyote mnamuogopa zto face to face..mkubal zto watanzania wamkubal,na natangaza waz#yeriko nakuchukia bas tu

Ni report ya benki kuu ya uswiss ndo ilitoa orodha ya jumla ya pesa toka kila nchi wateja wanakotoka bila kutaja majina. Sisi ndo ikaanza ya kufuatilia kila mtu anadai anazifuatilia
 
Kweli nimeamini maneno ya JK Chadema wanafiki wapo wengi. Wakati Zitto anaanza kazi hii mlikuwa kimya, leo kwa sababu ya maamuzi ya kipuuzi mnajaribu kumchafua. Wenye akili wataelewa anachofanya na wanafki endeleeni na unafiki wenu. Na natumaini kama alivyofanikiwa kufikia kuilazimisha serikali kuja na sheria ya madini mpya hata hili ninaimani atatusaidia kuja na mwafaka mpya hata sheria mpya ya uhamishaji fedha na ukwepaji kodi kimataifa. Zitto endelea kufanya ya taifa achana na wanafiki.
Anyway mkimaliza na Zitto mtuambie freeman Mbowe atatoa lini mkanda wa mauaji ya Arusha ili haki itendeke kwa familia za marehemu.

Mimi nikiwa na akili zangu timamu kabisa, sikukaa kimya bali nilimueleza wazi Zitto kuwa anawalaghai watanzania nakujaribu kujijenga mwenyewe kisiasa kwenye suala la mabilioni huko uswisi.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja tusubirie maoni ya Zitto atasemaje!

Back
Top Bottom