Mabibo hostel waua mtuhumiwa wa mwizi.

mi nafikiri wamekremu zaidi kuua lazima wapige mawe ilikuwa issue ndogo kumnywesha ule uchafu wa maji ya chooni nyuma ya lile hall
ashiki unamnywesha kikombe kizima unamwachia..sisi tulimkamata mwizi wakataka kumpiga nikawambia tutumie mbinu mbadala jamani
tukaenda nyuma ya nyumba ya mtu ikatafutwa ndoo na kikombe jamaa akalazimishwa kunywa akachiwa asbh wanamkuta yuko kala baruti njia ya kimara kuita shika saa nyingi..so vijana wangu sikunyingine msionekane wauwaji bali waamuliaji mpeni maji ya tanki la chooni kikombe kimoja kinamtosha
anyway

Goodjob

duuuh ndo naisikia leo loh!
 
kuua ni dhambi na against the law haijalishi amefanya nini! wangempeleka tu polisi apate adhabu yake huko ingawa hata magereza yetu yamejaa tufikirie njia mbadala sio kuua na je mna uhakika mia kwa mia ni mwizi coz kuna mke alishamwita mme wake mwizi mitaa ya stendi kidogo afe kisa walikuwa na maugomvi yao tu
 
Nikikumbuka kile kisa kilichomtokea jamaa pale IFM kwa kupokea kichapo baada ya kusingiziwa kuwa ni mwizi... kumbe alikuwa ametoka kwenye chumba cha Msichana wake,alipigwa bila hatia na hali hiyo ilipelekea kifo chake baadaye...Kabla ya kuchukua za kumpiga mtu (Mob Justice) tuweni makini...
 
Hivi bado watu hawajashtuka tu kuwa hao auxillary police ni washiriki wazuri na hao wezi? Na wanawajua fika..........hata wa pale UDSM. Tena Mlimani siku hizi ndo hapafai kabisa wanafunzi wanapokonywa laptops kama hakuna ulizi, majumbani walimu wanavunjiwa wanaibiwa, mpaka magari yanachukuliwa mchana kweupe.
 
Nikikumbuka kile kisa kilichomtokea jamaa pale IFM kwa kupokea kichapo baada ya kusingiziwa kuwa ni mwizi... kumbe alikuwa ametoka kwenye chumba cha Msichana wake,alipigwa bila hatia na hali hiyo ilipelekea kifo chake baadaye...Kabla ya kuchukua za kumpiga mtu (Mob Justice) tuweni makini...
Kuna mwingine aliuliwaga zamani kidogo maeneo ya geti maji engineering Mlimani kwa kushukiwa mwizi. Tena yeye si kuwa aliuliwa baada ya tukio la wizi la hasha. Ni kwamba kulikuwa na udokozi mdogo mdogo kama nakumbuka vizuri wa vifaa vya ujenzi, wakahangaika kutega mitego hawakufanikiwa. Siku ya tukio kijana wa watu katoka kwenye maghorofa ya maji pale kumsalimia dada yake akakatiza engineering ili atokezee Cafteria ya zamani; katoto si kakaropoka ......yule mwizi ni yule......... ikawa mwisho wa maisha ya yule kaka. !!
 
polisi imejaa rushwa, ukimpeleka polisi ataachiwa tu. kuiba hawaachi, kuua nidhambi na kinyume cha sheria. kwa hali hii jibu ni moja tu, serikali iangalie na upya sera zake, vijana wengi hawajielewi, waelimishwe waweze jitegemea, la sivyo tutaelekea pabaya sana
 
ndugu,ukikamata mwizi na akikuambia maisha magumu mpe kibarua afyeke nyasi kuzunguka nyumba yako, akimaliza atengeneze bustani ya maua na aoshe tuk tuk yako ili umpe kipato halali. hapo ndo utajua kuwa shida yake sio kipato halali,anataka mteremko. sina huruma na mwizi hata kidogo,awe wa mume/mke wa mtu, ama mali! wao wanaona maisha yako ni marahisi sana bila kufikiria nguvu uliyotumia kufika hapo ulipo! mwizi ni mvivu,la sivyo angeiba mara moja akapata mtaji wa kuuza mboga za majani kwa tenga!<br><br>
Hukumu hii wanapewa vibaka, wanaoiba weusi kwa wazungu hela nyingiiii wanapeta. <br>
Siwatetei wezi ila jamani mtaani maisha magumu. Nilishamkamata mwizi nikamweka chini nikaongea naye kwa kina kisha nikamuacha aende zake.
 
Back
Top Bottom