Mabibo, Dar es Salaam: Zaidi ya nyumba 200 zabomolewa zilizochini ya umeme mkubwa jijini DSM

Hakuna aliyewapa ruhusa wewe!! Mi nakwambia nimekaa mabibo zaidi ya miaka 25 iliyopita, walikuja wenyewe tu, na pale palikuwa jalala kubwa tu, wakajimegea maeneo kimya kimya basi! Ila wenyeji tulikuwa tunawacheka tu
Unataka kusema imekula kwaoo

Ova
 
Yale yale, waondoke kabla ya majanga, kwanza TANESCO anaweza kushtakiwa na hao hao kama akiwaacha waendelee na maisha pale! Wajuzi wa "Tort Law" wanaweza kufafanuwa zaidi, watolewe kwa manufaa ya umma, ama sivyo ulaji kwa squatters..
 
umeme(17).jpg

Zaidi ya nyumba miambili zimebomolewa zilizopo karibu na umeme mkubwa wa TANESCO katika eneo la Mabibo hadi bonde la Msimbazi na kuziacha familia bila ya makazi hali iiliyosababisha vitendo vya wizi na uharibifu wa mali zikiwemo samani, Magodoro pamoja na vifaa mbalimbali.

ITV imefika katika tukio hilo la bomoabomoa na kukuta watu wakiangaika kuokoa baadhi ya mali huku wengine wakiwa na nyuso za kukata tamaa baada ya mali zao kufunikwa matofali, wengine wakilalamikia vitendo vya wizi unaofanywa na baadhi ya vijana katika eneo hilo.

Wakati hao wakilalamikia upotevu wa mali zao ITV imeshuhudia baadhi ya wananchi wakiangaika kubomoa wenyewe nyumba zao kwa lengo la kuokoa mabati na vifaa vingine vya ujenzi, huku wengine wakihamisha vitanda, magodoro ambapo wakizungumza na waandishi wa habari wamesema licha ya kuwekewa alama ya x kwenye hizo nyumba lakini kesi ili kuwa mahakamani hivyo wangepewa taarifa ili waweze kuondoa mali zao.

ITV imemtafuta msemaji wa shirika la umeme nchini ili kuzungumzia swala hilo ambapo ametoa taarifa kuwa yuko katika kikao, ambapo kumbukumbu zinaonyesha kuwa nyumba hizo ziliwekwa alama ya x muda mrefu na wakazi hao walitakiwa kubomoa nyumba wenyewe na kuondoka katika maeneo hayo hatarishi yanaliyo chini ya umeme mkubwa wa TANESCO ambayo kwa mujibu wa sheria yanamilikiwa na shirika la umeme nchini TANESCO, jambo ambalo walipinga na kuamua kwenda mahakamani.


ITV
 
Ok lazima watu waishi kama mashetani ndani ya hii miaka kadhaa.
 
Ni kwa usalama wao..
Ila lazima walidharau kabla ombi la wao kuambiwa wahame.. wakifikiri ni awamu zilizopita..
 
Chadema 2020 tunatengenezewa njia rahis ya kuchukua dolla.


$wissme
 
Chadema 2020 tunatengenezewa njia rahis ya kuchukua dolla.


$wissme
ndio maana CCM itatawala milele kama hizi ndio akili za upinzani,yaani mpigiwe kura kisa mtaruhusu watu waishi sehemu hatarishi,nimesikitishwa sana kuona nchi hii bado ina watu wana uwezo mdogo kiasi hiki kichwani,poor you!
 
Duu kama namuona vile mama mwenye nyumba wangu wa yamani yamani anavyolia lia daa mungu mpe nguvu ya kumtafuta dalali wa vyymba vya uwani
 
Back
Top Bottom