mwali wetu
YNNAH mie naja na kibao cha zamani kidooogo cha Issa Matona Kimasomaso!
Anakwambia................
"Ukiitwa na bwana wajibu kumuitika
Ukiitwa ewe bibi uitike bwana rabeka
Umsikize mumeo bibi kwa kila analotaka"
"Anapokuja mumeo nyumbani hujambo muulizane,
Umpokee mkoba mama kilo ndani ukione,
Ujihadhari na shoga wasije wakunyang'anye,
'Subalkheri' njiani wengine si wanaume,
Leo umepata wako
YNNAH mahawara na wakome"
Hayati Issa Matona ukimsikiza na sauti yake wallah lazima utikise kichwa
"unapolekwa kwako unapofika nyumbani,
ukacheze na mumeo mama umpumbaze chumbani,
Wakija ndugu zako wakaribishe nyumbani,
Wakija mawifi zako mama uinuke kitandani,
Wanapokuja wakwezo uwaweke ukumbini,
Wakaja shemeji zako mama uwaweke barazani,
Wakija mashoga zako,,,,,,,,,,,,,sema nao dirishani,
Wakikuaga kwaheri mama uwambie karibuni,
Ufunge mlango wako urejee kitandani,
"Ukisikia hodi mama ushungi uwe kichwani,
Huenda akawa mumeo usimkere moyoni,
Kama ndiye sema "bwana pita" kwa sauti ya puani,
Mkandekande mabega mume kachoka kazini,
Huku ukichekacheka na macho yawe laini"
"Muwazuie waume wasirande majiani,
Muwafunge kwa vitanzi muwafiche maziwani,
Akija akikutoka humpati asilani,
Atapikiwa mkate na mchuzi bakulini,
Atafukizwa na udi na asumini kitandani,
Atakupita na Honda useme "yule sio bwana fulani"
Utatamani ahera dada nawe ungali mzima"
leo sina chumvichumvi nyingi ni hayo tuuuu.........waapiiii baikokoooo