mabibi na mabwana karibuni kwenye kitchen party ya YNNAH!!!!!

mabibi na mabwana karibuni kwenye kitchen party ya YNNAH!!!!!

amu

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2012
Posts
16,171
Reaction score
31,358
Asalam aleykum jamanii!!!
Bwana yesu Asifiwe!!!
Mashaalaah mmependeza!!! Watu mpo ng'aring!ari eeeee mmependeza kwa kweli!!
Embu dj @FixedPoint tuwekee ule wimbo wa marehemu Omary Kopa kitchen party tuburudike wakati tunasubiri mdumange all the way from Tanga wanaandaa vyombo wakisaidiana na baikoko.
Hapo mbele mnaona kuna majlis ndogo imezungukwa na makungwi wetu waliokuwa na kazi nzito naaam!!na bado kazi inaeendelea ikiongozwa na dj mwenyewe @FixedPoint Mamndenyi gfsonwin AshaDii snowhite mwaJ kungwiii mwenyewe matashtiti Madame B mama chumvichumvi Paloma all the way from chuga Cantalisia wamependeza kwa kweli na sare zao aaaa make ups zimetulia jamani!!Hongereni kwa kweli kwa kazi kubwa itakayoendelea na mliyoifanya.
Karibuni uwanja ni wenu kule pembeni kuna mabomba ya bia yaa ukweee ni kujibinyia tu moja limetoka tbl jingine limetoka mabibo wine na wale #team juice kuna mabomba yao ya azam juice,chilly will bavaria.
Karibuni tuserebuke huku tukimsubiri mwali kuingia ukumbini.
 
Last edited by a moderator:
dj Fixed Point embu punguza mziki kidogo naambiwa mwali yupo tayari makungwi wanatoka na kwenda kumchukua na kumuingiza ukumbini,wakati makungwi wanajiandaa naomba tusimame wote kumkaribisha malkia wetu wa leo jamani mbona wengine hamna vinywaji?? Heaven on Earth vipi mama hii ni shughuli vip service hapa embu kajibinyie unachotaka usuuze koo
 
Last edited by a moderator:
naam mwali keshaingia YNNAH mtoo jicho jicho,shingo shingo jamani wenye wivu wajinyongeeeeee!bila kuchelewesha mda namkaribisha Arabela atungulie shughuli yetu kwa duah
 
Last edited by a moderator:
naam mwali keshaingia YNNAH mtoo jicho jicho,shingo shingo jamani wenye wivu wajinyongeeeeee!bila kuchelewesha mda namkaribisha Arabela atungulie shughuli yetu kwa dua'h
 
Last edited by a moderator:
bridal-skincare-tips-for-radant-skin-01.jpg



hongera YNNAH weeee hongera namimi hongereee weeee hongera

na mie Paloma mamaa ya chumvi chumvi ndo namuingiza ukumbini!
namtaka mama yeke harusi naye aje hapa uwanjani!
bibi na dada harusi nao nawataka ukumbini!

kungwi na somo wa harusi mko jamani!?

njoni tumfunde mwali asije fedheheka ndoani!!!
 
Last edited by a moderator:
amu nishatia timu mie........

shughuli watu na watu ndi sie
 
Last edited by a moderator:
wii Paloma naona hauko nyuma..kijacho wetu lazima awe mcharuko

maana katembezwa sehem zote na mama ake
 
Last edited by a moderator:
Sare ya kitchen party ni rangi gani vileee😕😕😕
 
wii Paloma naona hauko nyuma..kijacho wetu lazima awe mcharuko

maana katembezwa sehem zote na mama ake

mie tena................sasa leo naenda kitchen party na ambyulensi.....vikianza tu aaaanh taratiiiibu najisogeza leba rum!
Lady doctor naye yumo atasaidia.

Sijui sansharie yupwapi naona bado anapaka mekap!
 
Last edited by a moderator:
naam mwali keshaingia YNNAH mtoo jicho jicho,shingo shingo jamani wenye wivu wajinyongeeeeee!bila kuchelewesha mda namkaribisha Arabela atungulie shughuli yetu kwa duah
Alfatihaaaa..amin.jaman mola aipe baraka shughuli yetu
 
Last edited by a moderator:
dj babu weeee hebu pumu tupumuweeeeee twamtaka mamie mwari aingie!
ha haaa, yaani leo nimekamatwa kweli, yaani huko kwenye taarabu ni sifuri....
bora mdogo wangu umekuja uwe unaniambia nitafute wimbo gani wa nani.......
 
naona makungwi mnaongezeka haya ukumbi wenu tena YNNAH ni mwiko mkubwa sana tena mizimu itakasirika kupikia mwiko afu usiuoshe tena wengine wadada wa .com wanapangusa mwiko na toilet paper jamani mwali usitutie aibu mwiko mwenzake kitambaa cheupe na maji
narudisha mic kwako Fixed Point snowhite Paloma Heaven on Earth
 
Last edited by a moderator:
mwali wetu YNNAH mie naja na kibao cha zamani kidooogo cha Issa Matona Kimasomaso!
Anakwambia................


"Ukiitwa na bwana wajibu kumuitika
Ukiitwa ewe bibi uitike bwana rabeka
Umsikize mumeo bibi kwa kila analotaka"


"Anapokuja mumeo nyumbani hujambo muulizane,
Umpokee mkoba mama kilo ndani ukione,
Ujihadhari na shoga wasije wakunyang'anye,
'Subalkheri' njiani wengine si wanaume,
Leo umepata wako YNNAH mahawara na wakome"

Hayati Issa Matona ukimsikiza na sauti yake wallah lazima utikise kichwa

"unapopelekwa kwako YNNAH unapofika nyumbani,
ukacheze na mumeo mama umpumbaze chumbani,
Wakija ndugu zako wakaribishe nyumbani,
Wakija mawifi zako mama uinuke kitandani,
Wanapokuja wakwezo uwaweke ukumbini,
Wakaja shemeji zako mama uwaweke barazani,
Wakija mashoga zako,,,,,,,,,,,,,sema nao dirishani,
Wakikuaga kwaheri mama uwambie karibuni,
Ufunge mlango wako urejee kitandani,

yani napata burudani hapa jamaniiii............

"Ukiisikia hodi mama ushungi uwe kichwani,
Huenda akawa mumeo usimkere moyoni,
Kama ndiye sema "bwana pita" kwa sauti ya puani,
Mkandekande mabega mume kachoka kazini,
Huku ukichekacheka na macho yawe laini"

Hapa akakukanya bibie ila ndo wanasema kumlinda patina ni sawa na kulinda bahari! Mweee

"Muwazuie waume wasirande majiani,
Muwafunge kwa vitanzi muwafiche maziwani,
Akija akikutoka humpati asilani,
Atapikiwa mkate na mchuzi bakulini,
Atafukizwa na udi na asumini kitandani,
Atakupita na Honda useme "yule sio bwana fulani"
Utatamani ahera dada nawe ungali mzima"

leo sina chumvichumvi nyingi ni hayo tuuuu.........waapiiii baikokoooo
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom