Mabere Nyaucho Marando

Ushushushu wake na jinsi alivyoisambaratisha na kuipoteza nccr mageuzi ndiyo kinachowafanya wanachama wengi wa chadema wamuone huyu jamaa kama kapandikizwa na ccm kuiharibu chadema
 
... Kama ni mashushu mbona aina yake wamo wengi tuu ndani ya vyama, na vyote?? Kama optimist, napenda kuamini pia kwamba wapo mashushu wengi sana wanaojali mustakabali wa Taifa lao vis-a-vis good governance na kwa hiyo siasa safi na uongozi bora pia. Namaanisha kwamba kama inawezekana ku-influence hayo nje ya Chama Cha Mafisadi, basi, kwa nia njema kabisa, wamo kwingineko.
 
Siku alipo tangaza kujiunga chadema, nilitoa angalizo kuwa kama alivyo fanya nccr asije akavuruga chadema. Must be handled him with care.
 
sio kweli alionekana mbaya kwa kuwa Mrema hakuwa na Elimu ya kutosha kuelewana nao akawa anatoamaamuzi mazito bila kuwahusisha wao, Mrema ndio alikuwa shushu mpaka leo bado sio mpinzani kwani kwenye makesi yake yote hakuna la kumkabili ila Mtikila linamkabili Mrema alitumwan na Rais was awam ya ------ kukimaliza chama cha wasomi waliokuwa tishio mdio maana Mwlm JK Nyerere alisema kamwe awezi kuona nchi yake inaliwa na mbwa yeye angali yupo, Baada ya Marando kumsahihisha makundi yalianza na baadaye akasomba kundi lake kuunda TLP ilo kundi lake nalo likameguka kwa nini msimuseme Mrema anayesupport CCM kwa hivi sasa na hali anaona ni chama cha Mafisadi sio wakulima wanyonge, JK aliposema iwapo utaona biashara inakufaa hapa sio maali pake chagua moja lakini leo hii wakulima wamepungua wapo wafanyabiashara wakubwa ambao ni wanyonyaji wa nguvu zetu ten wanamilija wameichonga sana mpaka wanafyonza Viongozi kam yaliyomtokea MH.6
 
katika siasa hakuna rafiki au adui wa kudumu; sioni hatari yoyote na marando.
 
Ushushushu wake na jinsi alivyoisambaratisha na kuipoteza nccr mageuzi ndiyo kinachowafanya wanachama wengi wa chadema wamuone huyu jamaa kama kapandikizwa na ccm kuiharibu chadema

Angeshinda Uspika ungesemaje? Mashushu mbona wako wengi sana akiwemo na mbunge wa Maswa Magharibi? Mbona huyo hatusemi? au kwa vile kashinda ubunge? Tuwahukumu watu kwa matendo yao sio kwa kazi zao.
 
Nakumbuka mwaka 1995 Mwalimu Nyerere alimwita huyo Marando mhuni hata Marando analitamubua hilo!Kwa waliyo karibu na Marando muulizeni atawambia ni kweli Mwalimu alipata kumwita mhuni
 
Suala la Marando tumelijadili sana humu kwenye thread zilizotangulia. Sisi ambao tunamfahamu vizuri Marando tulieleza humu kwamba ni mpiganaji wa kikweli kweli. CCM wamekuwa wakimpakazia kwa miaka mingi kwamba ni shushushu anayepandikizwa kwenye vyama vya siasa. Sisi tulishinda katika mjadala huu.
 
marando ni mwana harakati safi, mpiganaji safi na mpenda maendeleo ya nchi. Yuko chadema kudumisha chama. kule NCCR mrema ndiye alienda kukisambaratisha chama,wala si marando au lamwai. Mrema mpaka sasa anatakiwa kuangaliwa akipata upenyo atavuruga upinzania huko bungeni
 
ni mpiganaji mweledi, mzoefu, ambaye mbinu za CCM kudhoofisha upinzani ilimtumia Mrema kuali Muungano wa chama Cha wasomi , wanasheria na wakulima , baaday ya kufaniliwa kamfuata Msigina katiba Rwekamwa na kumsambaratisha, marando alitoka NCCR mageuzi kimya bila chokocho baada ya kuona CCM-C Mbatia anaanza U-Mrema wake, jama unakumbuka Mzee mzima Dr. Masumb Ramw arirudi sie sie em sasa wamemumaliza kwa kumtelekeza yuko pale Empress Mzee wa watu akiangaika na kesi asizo zishinda kwani wamemaliza ameduwaa Mrando bonge la Mjanja alidumu huko huko, maskni tumepoteza wakili maarufu wa pale mbezi Mzee wa Kiahay Mzee wa Tetea TETe aliyepoteza maisha nay alikuwa Mpiganaji (samhani Nimesahau jinale)
 
nifahamuvo mimi mashushushu haswa wa rika la marando wana uzalendo wa kweli kwa nchi yao hivyo basi kumtilia shaka marando ni kutotambua ukweli halisi!
 
Marando ni mpiganaji mweledi, alikuwa msema kweli hata ndani ya kitendo cha usalama wa taifa. Jambo la msingi ni kwamba CHADEMA wasimwamini kupindukia kiasi maana huwezi jua. Kwa nafasi aliyonayo ndani ya chama hana madhara sana, atawasaidia kuikomaza chama na kufika mbali.
 
NCCR-Mageuzi iliharibiwa na Mrema; Marando alikuwa mwasisi wa NCCR-Mageuzi na hivyo asigeianzisha halafu tena eti atumiwe na CCM kuiua.
 
Back
Top Bottom