Mabere Nyaucho Marando katupwa wapi?

Mabere Nyaucho Marando katupwa wapi?

Ni muda umepita toka huyu kamanda atoweke katika vyombo vya habari na siasa za Tanzania.

Hata ushiriki wake katika siasa za 2015 kuelekea uchaguzi ulikuwa hafifu.

Je amekumbwa na maswahibu gani.? Je ameachana na siasa.? Je siyo tena mmojawapo wa mwanasheria wa chadema.? Maana hata ushiriki wake katika kesi za chama hauonekani.

Pole huyu bwana nasikia ni taahira siku hizi na ndiyo maana nafasi yake ilishachukuliwa na Tundu.
 
Ni muda umepita toka huyu kamanda atoweke katika vyombo vya habari na siasa za Tanzania.

Hata ushiriki wake katika siasa za 2015 kuelekea uchaguzi ulikuwa hafifu.

Je amekumbwa na maswahibu gani.? Je ameachana na siasa.? Je siyo tena mmojawapo wa mwanasheria wa chadema.? Maana hata ushiriki wake katika kesi za chama hauonekani.

Marando ambaye ni mwanaharakati wa siasa za vyama vingi na gwiji wa sheria nchini, aliugua ghafla mwaka jana akiwa nyumbani kwake na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili usiku wa kuamkia Septemba 4.

Baada ya kupatiwa matibabu katika wodi maalum aliyokuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, hali yake ilionekana kuzidi kuwa mbaya na hivyo familia yake kulazimika kumpeleka India kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, uongozi wa Muhimbili katika kipindi hicho haukuweka wazi ugonjwa uliokuwa ukimsumbua Marando. Taarifa za kuaminika ni kwamba, Marando alitibiwa nchini India na kurejea kwa ajili ya kuendelea na mazoezi madogomadogo ya kumsaidia kuimarisha afya yake.

Kwa mujibu wa watu wa karibu yake hali ya Marando imeimarika na ingawa hajaanza kazi rasmi, amekuwa akitoa misaada ya kitaaluma kila anapohitajika, hasa kwa baadhi ya wanasiasa kutoka Chadema.

Mmoja wa viongozi wakuu wa Chadema ambaye hakupenda kutajwa jina lake kwa sababu si msemaji wa familia ya Marando, alisema hali ya kiongozi huyo kwa sasa ni nzuri tofauti na ilivyokuwa mwaka jana.

"Kwa kweli Marando mwaka jana aliumwa sana (lakini) tunashukuru Mungu kwamba madaktari wamejitahidi kwa hali na mali wakampatia matibabu mazuri na hatimaye afya yake kwa sasa ni nzuri," alisema kiongozi huyo.

"Viongozi (wa Chadema) wamekuwa wakienda kumtembelea mara kwa mara."

Mwanasheria mkongwe huyo amekuwa akitegemewa katika kusimamia masuala mbalimbali ya kisheria ya Chadema, na kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana aliahidi kutangaza matokeo kadri ambavyo angekuwa akiyakusanya kutoka kwa mawakala wa chama hicho.

Matangazo hayo yangekuwa kinyume na Sheria ya Uchaguzi na huenda Jeshi la Polisi lingelazimika kumtia nguvuni, lakini aligumua muda mfupi kabla ya tarehe ya tukio hilo kubwa la kidemokrasia la kila baada ya miaka mitano nchini, hata hivyo.

Alipotakiwa kueleza ni lini hasa pengine Chadema inataraji Marando atakuwa amerudi kwenye shughuli zake za kila siku, kiongozi huyo alisema, "Nakushauri uonane na familia yake (maana) ndo wanaweza kukueleza vizuri zaidi."

Nipashe iliwasiliana na mke wa Marando ambaye alisema hawezi kuzungumza kwa niaba ya mume wake na kushauri kuvuta subira mpaka pale Marando mwenyewe atakapoamua kuonana na mwandishi yeyote wa habari.

"Mimi siwezi kuzungumza kwa niaba ya mume wangu, na naomba usininukuu," alisema mkewe huyo nyumbani kwa Marando.

"Subirini atatoka mwenyewe kuzungumza na nyie mpaka mtaridhika."

Marando ni miongoni mwa wanasiasa wa kwanza wa upinzani nchini baada ya kuwa mmoja wa waanzilishi wa jukwaa la NCCR na kisha chama cha NCCR-Mageuzi muda mfupi tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Chanzo: Nipashe
 
Huyo alikuwa ni NATIONAL SECURITY.....Labda kapangiwa majukumu mengine....
 
Yupo anafanya kazi akimaliza ataleta majibu tuliza mzuka
 
Wadau naomba wenye taarifa za kina juu ya Mzee wetu Mabere Nyaucho Marando, maana kapotea kwa muda mrefu kwenye ulimwengu wa siasa. Hivi yuko wapi? Na mbona yuko kimya hivi?
 
Counter Intelligence Officer yupo labda afya imeyumba kidogo
 
Wadau naomba wenye taarifa za kina juu ya Mzee wetu Mabere Nyaucho Marando, maana kapotea kwa muda mrefu kwenye ulimwengu wa siasa. Hivi yuko wapi? Na mbona yuko kimya hivi?
Yupo sana ila afya yake iliyumba
 
Yupo ndugu, juzi alionekana CDM makao makuu akisaini ktk kitabu cha msiba wa Ndesapesa.
 
Yupo mkuu anajaribu kumfundisha maadili "Baba Wema"
 
Toka alivyoahidi kutangaza matokeo ya urais kabla ya tume,akamixiwa..akaanza kuumwa mpk kesho.Jamaa zake wa zamani walimpa kitu ngumu!!
 
Poleni na majukumu familia ya JF. Niende kwenye swali hapo juu. Huyu mtu alikuwa mwanasiasa na wakili pia. Cha ajabu kapotea ghafla na sijasikia tukio linalomhusu hadi akatoweka. Najiuliza yupo wapi? Anafanya nini? Je kapatwa na nini Mbna kmya sana?
 
Back
Top Bottom