Mabere Marando na utetezi wa Manji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabere Marando na utetezi wa Manji

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by BIN BOR, Feb 17, 2011.

 1. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huyu Manji ni fisadi na wengi tunajua hilo. Huyu Manji anatetewa na Mabere Marando aliye mwanasheria wa CDM. Chadema inakemea ufisadi. Sasa uadilifu wa Mabere uko wapi, au pesa mbele maadili nyuma? Naamini Dr. Slaa ataisoma hii. Tusifumbiane macho pale tunapokwenda vibaya.
   
 2. smati

  smati Senior Member

  #2
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Marando yupi?? Yupo marando mwanasheria na marando mwanasiasa. hata kama ni yuleyule lakini ni watu wawili tofauti.
   
 3. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kikwete rais na Kikwete mkwere ni watu wawili tofauti? Ndio maana nikasema uadilifu nyuma, pesa mbele......
   
 4. M

  MushyNoel Senior Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mara ya kwanza nilishangaa. lakini cha kuelewa ni kwamba Mengi katika matangazo aliyoyatoa kupitia ITV alimwita manji fisadi papa na alipokwenda mahakamani wakili wa Mengi ( Michael Ngalo ) akawasilisha nyaraka za makampuni ya manji yaliyokwapua fedha kutoka Kagoda .Manji akitumia kampuni yake ya Quality Finance.

  Sasa sheria ya makampuni inamtambua mmiliki wa biashara na kampuni yake kama watu wawili tofauti.hivyo basi Mengi kumwita manji fisadi papa halafu akaenda mahakamani kutumia nyaraka za kampuni ya manji kuna walakini kisheria.Hivyo Marando anamtetea manji kama personal na sio makampuni yake yaliyofanya ufisadi.
   
 5. T

  TechMaro Senior Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hili jambo limekuwa likinisumbua kwa muda mrefu sana.... I am starting to suspect hii opposition tuliyo nayo kusema kweli. Tusikute ni kukosekana kwa opportunities upande mwingine ndo watu wakahamia upinzani, huku mioyo yao bado haijabadilika.
  Leo hii, Mabere Marando ndo anaongoza kukataa nyaraka eti lazima ziwe zimethibitishwa na ofisi husika.... This is very wrong especially as ni mtu wa upinzani na wakati wa kampeni alijionyesha yeye ni hodari wa kuwataja mafisadi hadharani...
   
 6. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Marando yuko kazini na ana familia inayomtegemea kupata mlo.Sasa sidhani yeye ingekuwa rahisi kuacha tenda ya kazi ambayo kasomea miaka yote hio kisa mambo ya siasa.

  Kama wakina Mengi wana ushahidi wa kutosha watashinda kesi kama hawana inamana wameshindwa kesi na Marando katimiza wajibu wake kama wakili na atakuwa kalipwa hela halali za kazi aliofanya.
   
 7. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kama ni kuendekeza njaa basi Rostam akiwa na kesi Marando anaweza kumtetea?
   
 8. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo kesho si ajabu ukasikia Marando mwanasheria wa CCM, eti kwa sababu ana familia. Obama ni mwanasheria na kampuni yake haitoi utetezi kwa shauri lolote lenye maslahi ya kuwajenga republicans na hata wao hawa-consult kampuni hiyo kwa sababu hizo hizo. Kwa maneno mengine unataka kusema hata katika Chadema Marando alifuata mshahara na si itikadi. Na alikuwa mgombea wa uspika. Sina chuki na Marando lakini hapa kuna suala uadilifu na kama ningeandika kichwa cha habari ningesema kiongozi wa CDM atetea fisadi wa CCM. Kama ni familia, hata Nyerere alikuwa nayo wakati anaacha ualimu na kufanya siasa. CHADEMA INAPAMBANA NA MAFISADI NA SIO KUWAPAMBA.
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, hiyo ndio hypocrisy ya baadhi ya wanasiasa wasiosimamia morals wanazoziamini... binafsi nafahamu kila lawyer ana moral conducts zake na mabere kwa kuwa chadema na kutetea manji ni contradictory

  he needs to uphold CDM standards by not represent Manji
   
 10. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160

  Kwahio Marando angekuwa daktari na Manji anaumwa mngemlaumu kumtibu Manji kwa vile atalipwa kwa hela za ufisadi?


  Kama Mengi ana ushahidi wa kutosha atashinda haijalishi nani anamtetea Manji.


  Mbona nyie bado mnatumia mtandao wa vodacom? hamjui kama mnawalisha mafisadi? sasa kwanini yeye asifanye kazi yake?
   
 11. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Marando alichofanya ni wrong. Kubali kataa. Chadema wanabidi wawe makini la sio watakuwa hawana credibility wakiimba wimbo wa ufisadi.
  Imagine angeshinda uspika? Speaker Marando amtetea Manji. No way!!
   
 12. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160

  Tatizo tumekaa tunapoteza mda kuwaita mafisadi bila kuchukua hatua yoyote.Mafisadi wanaendelea na maisha yao bila wasi wasi. Wenye ushahidi wanaweza kuwapeleka mahakamani hatuwezi kuendelea miaka nenda tunapiga kelele na kusimamisha maisha ya watu wengine kisa hao mafisadi.

  Hawa mafisadi wote ni wafanya biashara kwanini sisi wananchi tusigomee biashara zao kama tunamsimamo lakini tuko tayari kumyooshea kidole MARANDO kwa kufanya kazi yake ya uwakili hili apate pato?


  Au huoni kwa sisi wananchi kuendelea kununua bidhaa za mtu yoyote anayetuhumiwa kwa ufisadi ni kuendelea kuwatajirisha?
   
 13. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Itawezekanaje kwa daktari bingwa wa macho kupasua moyo? Tafuta mfano mwingine.
   
 14. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unaanza ku-justfy ule usemi....if you can't fight them, join them???
  Marando amechemsa na ni ameshaanza kuwa a big liability for Chadema. Marando ni kansa na soon ataiangamiza Chadema for his selfishness. Kubali kataa lakini huo ndio ukweli
   
 15. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Na sisi wananchi pia tuna makosa kuendelea kutumia/kununua bidhaa za hawa mafisadi , tuache kuwategemea wanasiasa tu kwenye kila kitu na sisi pia tunaitaji kuchangia pale inapowezekana.


  Marando wakili na hio ndio kesi ilimfuata. Kwanini mengi hakumuajili Marando hili wamshitaki Manji kama alikuwa na ushahidi wote?

  Kazi ya uakili unaweza kuwa kwenye upande wowote utaokufuata mwanzo kwa vile ndio njia yako uliochagua ya kukuingizia kipato.
   
 16. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nipe sababu za msingi na uthibitisho unaoonyesha kwamba manji ni fisadi au na wewe umesikia tu kwa watu!subiri kesi iishe mahakamani iwapo mahakama itathibitisha kuwa manji ni fisadi ndipo utoe hizo lawama kwa marando!!mimi naona hapo umechanganya siasa na kazi halisi ya mtu malando akiwa kama mwananchi wa kawaida watoto wake wanahitaji kuvaa,kula na elimu so sioni sababu ya wewe kumzuia kufanya kazi kwa kuwa unakua kama umeshamhukumu manji kama fisadi kitu ambacho si kweli kesi bado haijaisha!
   
 17. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kama ana njaa ya kulisha familia yake ni haki kumtetea Rostam akiwa na kesi tena ya ufisadi?
   
 18. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kesi ya Mramba na Yona ikimfuata aichukue kwa sababu ya kuingiza kipato?
   
 19. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kivipi sasa? mfano wangu umelenga ajira kwamba mtu hutakiwi kuchagua unayemuhudumia.

  Kesi hii ni MANJI VS MENGI na sio MANJI VS CHADEMA, kama ingekuwa MANJI VS CHADEMA hapo ndio tungemshangaa Marando kwa kuendana kinyume na chama chake. Nyinyi mmeichukulia kesi kisiasa na ndio maaana mnamshangaa MARANDO lakini hii kesi ni ya watu binafasi wawili na imetokea kwamba upande mmoja umemuajili MARANDO kuwa wakili wake.
   
 20. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ikija kesi ya ROSTAM v/s SLAA Marando achukue kesi?
   
Loading...