Nimewahi kusikia hawa watu huwa wanatumika hata baada ya kustaafu,na ukumbuke ni amri.Je haitupi wasiwasi na UWT uliogeuka kuwa UWC(Usalama Wa CCM) ukawa na mikono kwenye vyama vya upinzani kupitia watu kama Marando?NCCR palitokea mgogoro kikadhoofu sana,naomba mwenye taarifa za utendaji wake,kama alihusika na migogoro au la,na kivipi kwa wakati akiwa NCCR pia kilichomtoa huko ni nini.Nina wasiwasi naye saana.
jiulize kwanini dokta na chadema walimsimamisha uongozi..unasema kafulia alikuwa alikuwa mamluki ? Unaweza ukaelezea zaidi.
Mwanamayu you are missing the point, mtu kuwa usalama wa taifa si kwamba wote ni wasaliti wa taifa kuna usalama wa taifa huku wana mapenzi makubwa na taifa lao zaidi ya wewe usiye usalama wa taifa.Marando amesema mwenyewe kuwa alikuwa mwajiliwa wa usalama wa taifa, sasa ni vipi aliacha kazi hiyo? Alifukuzwa? Kwa nini alifukuzwa? Alistaafu? Na alikuwa na wadhifa gani wakati anatoka huko? Je, si bado mmoja wao?
Heshima kwako PAS,
Mkuu sina hakika sana kama Marando kapewa assigment ya kuisambatratisha CHADEMA,mara nyingi watu wa system wanatumia hali ya mambo ya wakati husika kufanikisha mipango yao.Mfano CHADEMA wakati huu wana vita ya chini chini ya kugombea nafasi ya kiongozi wa upinzani bungeni Zitto Kabwe naibu katibu mkuu na Mwenyekiti Freeman Mbowe wanaweza kusababisha yaliyotokea NCCR Mageuzi yajirudie tena.Rejea tena bandiko langu kazi kubwa ya UWT kipindi hiki ni kusambaratisha upinzani Marando yuko tena kwenye chama kinachoitia hofu CCM akifanikiwa tena anaweza kufananishwa na yule kachero mashuhuri sana nchini Israel Bwana Eli Cohen.
:smile: Usistaajabu yaliyotokea NCCR utakapoona ya CHADEMA:smile-big:Marando amesema mwenyewe kuwa alikuwa mwajiliwa wa usalama wa taifa, sasa ni vipi aliacha kazi hiyo? Alifukuzwa? Kwa nini alifukuzwa? Alistaafu? Na alikuwa na wadhifa gani wakati anatoka huko? Je, si bado mmoja wao?
huyo baba ni mfanyakazi wao na huko alipo yuko kazini!!!
Mkuu Andrewk,
Ni kweli ukitazama mfumo wa tawala nyingi dunia eg Uk na Austria kiongozi wa upinzani bungeni pia ndiye kiongozi wa chama.Jiulize unadhani yanayoendelea ni bahati mbaya !.
Pamoja sana Mkuu
Tatizo hapa jamvini ni ubishi tu ubishi tu - MN Marando bado ni mwajiriwa wa TISS - kama unakataa kajinyonge UFE!
Du..Maswali mazito kwelikweli haya!..pia nina wasiwasi baadhi yake yanamhitaji yeye mwenyewe ayajibu kwa usahihi, vinginevyo utalishwa sumu hapa!
Tatizo mnabwabwaja bila kuwa na fact. Lini ulimwona Marando akimsifia Kiongozi yeyote wa Serikali au Ufisadi. Hvi kati ya Mrema na Marando nani alivuruga chama cha mwenzake?
NCCR walimpokea Mrema akiwepo Marando aliyempisha ili awe mwenyekiti lakini baadaye alianzisha migogoro
Pamoja sana Mkuu
Tatizo hapa jamvini ni ubishi tu ubishi tu - MN Marando bado ni mwajiriwa wa TISS - kama unakataa kajinyonge UFE!
Tatizo mnabwabwaja bila kuwa na fact. (1)Lini ulimwona Marando akimsifia Kiongozi yeyote wa Serikali au Ufisadi. Hvi kati ya Mrema na Marando nani alivuruga chama cha mwenzake?
NCCR walimpokea Mrema akiwepo Marando aliyempisha ili awe mwenyekiti lakini baadaye alianzisha migogoro isiyokwisha kwa kutaka kuendesha chama kibabe na siyo kikatiba hvo akakitibua chama cha NCCR. Baadaye alipotoka Mrema NCCR iliyumba lakini ilikuwa imetulia tofauti na TLP alikokwenda Mrema isiyokwisha mgogoro.
Wapinzani pia wana matatizo yao. Walimtuhumu Marando kuwa ni kibaraka wa ccm pale alipowashinda ubunge wa Afrk Mashariki. Marando anajua kujieleza na alikuwepo bungeni hivo kufahamiana na wabunge wengi. Wakati wagombea wengine wa nafasi ya upinzani kwenye bunge hilo walijipambanua kama wapinzani zaidi Marando aliwazidi kete kwa kujieleza vizuri zaidi na kujipambanua kama mtanzania bila kubagua wabunge wa CCM wakampa kura na akashinda huo ubunge.
Hapa tunajiita great thinkers lakini kwani kwa hili la Marando mmechemsha. (2)Hivi Kazi anayofanya Marando ya uwakili bado kuna haja ya kutafuta vijisenti kwenye Usalama wa taifa?
Mwachani Marando enyi vijana wa Dot com make wazoefu tunamfahamu ni mpambanaji aliyewafungua watanzania macho enzi za kuanzisha mageuzi.
Marando amesema mwenyewe kuwa alikuwa mwajiliwa wa usalama wa taifa, sasa ni vipi aliacha kazi hiyo? Alifukuzwa? Kwa nini alifukuzwa? Alistaafu? Na alikuwa na wadhifa gani wakati anatoka huko? Je, si bado mmoja wao?