Mabeberu wameanza fyokofyoko DR Congo

Mabeberu wameanza fyokofyoko DR Congo

AVRAM

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
616
Reaction score
889
Vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti kuwa taarifa zilizovuja kutoka matokeo kamili ya uchaguzi wa Desemba 30 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zinaonyesha kuwa mgombea aliyetangazwa katika nafasi ya pili, Martin Fayulu, alikuwa ndiye mshindi wa wazi.

Taarifa hizo zimetolewa na gazeti la Uingereza la Financial Times, na vyombo vya habari vya nchini Ufaransa, ikiwemo Radio ya Kimataifa ya Nchi hiyo RFI, na kituo cha televisheni cha TV5.

Chanzo: DW: HABARI.
IMG-20190116-WA0029.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku dunia ikisubiri kwa tahadhari uamuzi wa mahakama ya kikatiba juu ya ni nani mshindi wa kura za urais huko Kongo, kumeibuka data zilizovujishwa kutoka ndani ya database ya tume ya uchaguzi inayohusisha asilimia 86 ya kura zote zilizopigwa. Data hizi ambazo zimechambuliwa na kuripotiwa na gazeti la financial times zinaonyesha kuwa mgombea Martin Fayulu alishinda uchaguzi wa December 2018 kwa asilimia 59.4 (59.4%), akifuatiwa kwa mbali na Felix Tshisekedi aliyepata asilimia 19 (19%)- Congo voting data reveal huge fraud in poll to replace Kabila. Pamoja na juhudi za Kabila kujaribu kuendesha uchaguzi kwa kuzuia usimamizi wa uchaguzi kwa vyombo kutoka nje, yaonekana wazi kuwa kuna wazalendo waliowezesha kukushanya hizo taarifa sahihi na kuzivujisha.

Taarifa hizi mpya, zinakaribiana sana na zile zilizotolewa na kanisa katoliki zilizokusanywa kwenye vituo zaidi ya elfu 40 zilizoonyesha kuwa Bw. Fayulu alishinda kura za urais kwa zaidi ya asilimia 60. Pamoja na hayo, waratibu wa kampeni ya Bw. Fayulu, wanadai kuweza kukusanya sampuli za matokeo yanayoonyesha ushindi wa zaidi ya asilimia 61. Takwimu hizi, zimeongeza hisia za watu wengi ndani na nje ya Kongo kuwa Kabila aliingia makubaliano ya kushirikiana madaraka na Bw. Tshisekedi, baada ya kudhihirisha kuwa asingeweza kumtangaza mgombea wa chama chake Bw. Shadari aliyeshindwa vibaya mno kwenye uchaguzi huo.

Kutokana na taarifa hizo, dunia imeanza kuimulika Kongo. Jumuiya ya SADC ambayo Kongo ni mwanachama, imeitisha kikao cha dharura kuijadilli huko Addis Ababa, Ethipia - SADC calls for emergency meeting over DRC poll. Pia SADC ambayo kupitia waangalizi wake kwenye huu uchaguzi katika hatua za awali ilitoa maoni kuwa ulienda vizuri na kasoro ndogondogo, imegeuka msimamo wake wa awali na kuitaka tume ya uchaguzi ya Kongo (CENI) ihesabu kura upya African nations call for recount in DRC election. Mataifa yenye ushawishi Kongo, mfano Ubelgiji, Ufaransa na Marekani, wote kuanzia awali waliyatilia shaka matokeo ya uchaguzi, wakisema yalipinduliwa.
 
Hao ma beberu wanataka amani itoweke waendelee kuiba rasilimali za kongo hawana jipya hao.
 
DR Congo isingekuwa na utajiri mkubwa wa madini wazungu wala wasingejiangaisha kumjua Fayulu wala Tshisekedi.

Lakini kila wakichungulia wanaona madini yenye fedha nyingi, lazima wajifanye wana upendo mkubwa.

Jana wakati magaidi wanafanyiza pale Kenya CNN, BBC Al Jazeera na wazungu wengine akili zao zilikuwa BREXIT.
 
Nadhani hujitambui jinsia yako wewe!
Hao "MABEBERU" ndio wamekupatia "Tanganyika" na baadaye Tanzania. Huko Berlin.
Mabeberu hao hao kutokea Ubelgiji mahali alipokwenda kutibiwa kaka TL, ndio wakamuua Patrice Lumumba kwa kutumia acid ili ushahidi usipatike milele.
 
Mabeberu hao hao kutokea Ubelgiji mahali alipokwenda kutibiwa kaka TL, ndio wakamuua Patrice Lumumba kwa kutumia acid ili ushahidi usipatike milele.

Na ni mabeberu hayo hayo yalimpiga risasi TL au ni nani?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom