Mabasi yabeba mawe badala ya mizigo ili kujenga daraja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabasi yabeba mawe badala ya mizigo ili kujenga daraja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Mabasi yafanyayo safari kati ya Wilaya ya Serengeti na Musoma yameamua kubeba mawe badala ya mizigo ili kutengeneza daraja bovu katika eneo la Daraja Mbili wilayani hapa baada ya daraja hilo kuzidiwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha.
  Kutokana na hali hiyo, wanafunzi wa Sekondari ya Ikorongo kata ya Kebanchabancha ambao wamekuwa wakitegemea usafiri wa mabasi hayo yaliyokuwa yakiwachukua bila kulipa nauli wamekuwa katika adha kubwa ya kukosa usafiri.
  Mwandishi wa habari hizi ambaye alikuwa miongoni mwa abiria wa gari hilo alishuhudia wanafunzi hao wakitakiwa kushuka katika kijiji cha Rung’abure na kutakiwa kujaza mawe kwenye mabuti ya basi la Zuberi linalomilikiwa na Ngoreme, ili yasaidie kujaza kwenye daraja hilo ambalo kwa kipindi kirefu limekuwa bovu.
  ”Wanafunzi wote mnatakiwa kuteremka mkabebe mawe maana huo ndio mchango wenu,jamani abiria hapa tunalazimika kubeba shehena ya mawe ili kujaza pale Daraja Mbili eneo la Nyarukongo maana hatuwezi kupita hivi hivi hapo, hakuna ujanja hii ndiyo serikali ya awamu ya nne maisha bora kwa kila Mtanzania,” alisikika akisema msaidizi wa dereva.
  Pamoja na wanafunzi hao kugeuka wajenzi, baadhi ya abiria wakiongozwa na diwani wa kata ya Nyamatare Chacha Nyasagaw alilazimika kujitosa katika kazi hiyo ili kujaza haraka mabuti yote.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
Loading...