Mabasi ya mikoani yanayotembea usiku yawekewe Askari kipindi hiki cha sikukuu

Madukwaa

Member
Nov 13, 2023
17
14
Napenda kulishauri Jeshi la Polisi/Usalama barabarani, tunapoelekea katika msimu wa sikukuu kwa mabasi ya mikoani hasa yanayotembea usiku kuwekewa ulinzi wa maaskari ndani ya mabasi.

Hii ni kwaajili ya usalama wa abiria hasa wanaosafiri usiku.
 
Sawa Ila Askari Ni Wachache Kuliko Idadi Ya Bus
Labda Ungetaja Maeneo
Siyo mabasi yote, yale tu yanayotembea usiku, Mfn: kuna mabasi yanatoka stand saa 1 jioni pia saa 3 usiku.
Dar tu mza
Arusha tu mza n. k
 
Siyo mabasi yote, yale tu yanayotembea usiku, Mfn: kuna mabasi yanatoka stand saa 1 jioni pia saa 3 usiku.
Dar tu mza
Arusha tu mza n. k
Mmmmm askari wanatakiwa kwenye doria ....sio kila bus sijui kama unaelewa unachokitaka ? Doria barabarani usiku ndio suala la msingi sio vinginevyo
 
Askari huyo unaposafiri naye anahitaji kula, anahitaji maji kunywa, anahitaji accommodation.

Unapozungumzia suala la kiulinzi usiku unamaanisha Bunduki, otherwise akiwa askari pekee bila bunduki naye ni pambo tu mnatekwa na mnaibiwa wote. Sasa basi, kama ni bunduki lazima wawe askari wawili, kwa maana huwa hawakaagi bunduki moja, lazima wawili wasaidiane. Hii inamaanisha gharama mara mbili, je kampuni za mabasi zinaweza kumudu gharama hizo??
 
Back
Top Bottom