Mabasi ya Mbeya yanakimbia sana

Hvi likichomoka jabali hko juu itakuwaje aisee
Hio ni sehemu ya bonde kuu la ufa la afrika mashariki.
Mawe huwa yanaporomoka na kuziba hiyo njia hasa msimu wa mvua.
Hata hivyo huo mlima ulichongwa na kampuni moja ya ujenzi ili barabara ikae vizuri kama inavyoonekana sasa.
Kabla haijachongwa hiyo njia ilikuwa mbaya sana na gari ilitumia muda mrefu kupanda au kushuka huo mlima.
 
Looo mkuu nilipita hapo usingizi wote ulikata nikaana kukaa kama abiri wa kwenye boda boda.
 
Hakuna safari hua naifurahia kama Kampala- Mwanza. Picha hua linaanza saa 5 usiku ndani ya zhong tong mpya la Friends au Isamilo. Ni mwendo wa 100-120 barabarani mko wenyewe tu chuma inakata lami tu
 
Watuondolee hivyo vi speed governor vinatumalizia ladha.
Watuache tu Mbeya tuwe tunafika saa saba
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Umenikumbusha enzi za miaka ya 1998 hadi 2000 kulikuwa na basi la masia, lilikuwa inafika Tunduma saa 9:00 mchana kutoka Dar... Chini ya dereva mahiri Deo Kapelege, aisee ilikuwa balaa
Lilikuwa linapita Iyunga saa 8:20 ilikuwa ni roho mkononi
 
Hekima sa tisa jioni siku tuko ubungo mataa pale licha ya foleni,na ilitoka tunduma nilidandia uyole.yule dereva kimbaumbau hivi ye anapiga fegi tu na gia hewani balaa sikupata hata lepe la usingizi njia nzima machine inapepea tu pale mafinga ndo aliua
 
Ni kweli kabisa, miaka ya 99 bus kama la Embakassy lilikuwa linaingia stand Mnazi mmoja saa 12:45 jioni kutoka Mbeya, na hilo ndio lilionekana kuwa slow kuliko yote!

Lilikuwa likiitwa FISI. Ndilo lilikuwa la mwisho kuingia Mbeya au Dsm.. Lenyewe lilikuwa likijichukulia abiria wote wa mwishomwisho.
 
Ni kweli kabisa, miaka ya 99 bus kama la Embakassy lilikuwa linaingia stand Mnazi mmoja saa 12:45 jioni kutoka Mbeya, na hilo ndio lilionekana kuwa slow kuliko yote!
Huko mbali 2008 tu hapo natoka songea nakuja dar, kibaha tumeingia saa 12 iv jua linawaka mpaka 2.30 iv nipo, so kwa sasa safari hazina raha masaa kibao barabarani
 
Bujibuji umenikumbusha hii nikiwa home SIMIKE nikisikia makelele tu kona ya META najua TAWAQAL hiyo imetoka DAR.

Mwaka 98 nilipanda TAWAQUAL ya Kaburu tulitoka Ubungo- Majisaa 12.15 asubuhi. Ndani ya basi kulikuwa na mzee mmoja anahubiri neno alipandia Morogoro, ngoma wakati inakata kona za IYOVU mzee aliacha kuhubiri akaenda kumchungulia dereva, alirudi kimya na INJILI ikaishia pale. Saa 5 hivi tuko Iringa pale Ipogoro. TRAFIKI akatuhoji safari ikoje wahuni wakajibu "poa". Kumbuka hapo kuna basi iliingia mtoni mazima huko Tanga.
Tuliingia Mbeya saa 9 hivi. Nikaulizwa umekuja na JENEZA (Mwamahapa- M Sleeping Coach)? Nikawajibu hapana, hiyo ngoma ilitua nusu saa kabla yetu.
 
Sijui haya magari yaliundwa vipi.

Maana kwenye kona yalikuwa yanalala kama yanadondoka kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…