Mabasi ya Al-Saedy Dar- Iringa: uhuni, dharau na kunyanyasa abiria vimekithiri

MtamuMix

Senior Member
Feb 10, 2018
119
138
Kampuni ya mabasi ya Al-Saedy yanayofanya safari zake Dar-Iringa wanafanya uhuni na dharau kwa abiria bila kufikiri madhara yake.
Abiria wanakatiwa tiketi gari ya saa moja na nusu, mnafika stend ratiba inabadilishwa mnaondoka saa tatu.
Nyingine ratiba inaonyesha kuondoka saa tatu, wao wanaondoka saa mbili na nusu.

Abiria wanaachwa kwa kisingizio cha kwamba ulitakiwa kuripoti nusu saa kabla ya safari. Leo, juni 28 gari la saa3 limeondoka saa mbili dk 40 juu ya alama. Mbaya zaidi abiria aliyefika saa mbili dk 42 anajibiwa kwa kejeli na dharau kwa nini hukufika saa mbili na nusu.
Huu uhuni hauvumiliki, sijui trafic police wanaokagua wanafanya nini? Au nao ni sehemu ya huu uhuni...

Sawa, tunawaachia kampuni yenu, tunahamia rasmi makampuni mengine. Ila mjue kabla yenu yalikuwepo makampuni makubwa ila leo wako juu ya mawe.

Wasalaam,
Mimi muathirika.
 
Wanasema anaringa kwakuwa yeye Ana scania ambazo kwa hyo route hakuna wa kumkamata njiani
 
Siungi mkono hizo kauli za hao wahudumu kwa wateja wao. Ila linapokuja suala la kuwahi vituoni, na sisi abiria tujitahidi kuwa 'panctual'.

Abiria unatakiwa ufike kituoni nusu saa kabla ya muda wa basi kuondoka ili kuondokana na hiyo sintofahamu.

Nina imani ni wewe mtoa mada tu uliyeachwa kwa bahati mbaya kwenye hiyo safari. Pole sana kwa usumbufu ulioupata.
 
Acha kuharibu biashara za wenzio kwa uzembe wako binafsi..au wewe utakua mmoja wa wenye mabasi ushaona mwenzio anapata passenger's ukaamua umharibie apoteze wateja, waswahili ndivyo tulivyo ukiona mwenzio anapata unaumia.

Kama nikweli one of the passengers ulieathirika basi hamia pekeyako, ila usiseme "Tunahamia rasmi makampuni mengine"
 
Back
Top Bottom