Nyanda za Juu Kusini: Uwekezaji kwenye Kusafirisha abiria (Niliyojionea)

Dumbuya

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
593
870
Habari Wanajamvi...Heri ya Mwaka Mpya !

Nipende kuleta kwenu mtiririko wa matukio na hali halisi niliyoshuhudia katika kuelezea sekta ya usafirishaji (abiria) nyanda za juu kusini (Iringa,Njombe,Ruvuma na Mbeya).Kutokana na uchangiaji wa moja kwa moja wa sekta hii kwenye uchumi na uhitaji wa maboresho ambayo kimsingi yanasimamiwa na siasa basi uzi huu nina imani upo jukwaa sawa na utachagizwa kuleta maboresho katika upande huu wa Tanzania.

Safari : Dar - Kyela

Ubungo
: Safari inaanza taratibu nikiwa ndani ya basi la semi luxury ambayo kwa route hii ya Dar - Kyela nauli ni Tsh.40,000/-(ambayo ni daraja la juu kwa safari hii). Hali ya basi lile ni ya kawaida sana hasa ukizingatia vitambaa na siti vinaonekana dhahiri havijafanyiwa usafi wa uhakika (kufuliwa) kwa muda mrefu. Tv ilikuwa imewashwa kama sehemu ya kuwaliwaza wasafiri lakini sauti haisikiki vizuri kutokana na uchakavu wa madirisha (rubber) hivyo kupelekea kelele zinazotokana na mtikisio wa gari kufika kabla ya sauti ya TV.Nilifika kwenye siti yangu na nashukuru kwani mikanda ilikuwepo na ilifanya kazi sawia.

Tulipofika Kibamba matone ya mvua yalianza kudondoka na kupelekea abiria wengi kufunga madirisha yaliyokuwa wazi.Hapa harufu mbalimbali zilianza kusogelea pua zetu lakini pia kuliamsha janga lingine ambalo lilituacha midomo wazi.Kupitia kwenye carrier maji yalianza kuingia ndani na matone kudondokea kwenye siti (hasa za dirishani)...Hiii iliamsha tafrani kwa abiria aliyekuwa analowa na maji yale...Mzee yule ilibidi abadilishiwe siti ndo akatulia. Siti yake ilikuja kukaliwa na abiria aliyepanda Kibaha ambapo mvua ilikuwa umetulia.

Safari iliendelea na mwendo mzuri na dereva alijitahidi kuzingatia alama za barabarani hasa speed...

Mbuyuni (Chakula) - Iringa: Kufika hapa abiria tuiingizwa hotelini ambako tulipewa dk.10 za maliwato pamoja na kupata chakula.Kwa jicho la haraka hoteli ile ina aina mbili za chakula bufeet (wali nyama) na chipsi + nyama,pamoja na duka moja linalouza vinywaji, biskuti na vitu vingine vidogodogo.

Sehemu kubwa ya eneo hili inaonekana kutengwa na kutokuwa na shughuli.Kwa biashara ya kulisha wasafiri hakika ni wazi kuwa hoteli hii na nyinginezo za aina hii ambazo zinafuatana zina ukosefu wa ubunifu au upungufu wa mitaji kuweza kutoa huduma bora kwa uhakika.Maliwato yake yalikuwa okay japo usafi wanajitahidi japo bado ni changamoto hasa ukizingatia uwepo wa maji kwenye sakafu na hali ya ukungu kwenye marumaru.

Comfort Hotel - Tukiwa tunaitafuta Ilula..tulipita eneo maarufu kwa wengi nalo ni kitonga lakini kabla ya hapo kuna hoteli moja iliyokuwa mfano wa kuigwa kwa standard ya vyakula na ubora wa huduma,uwepo wa aina mbalimbali za viburudisho (refreshments) kwa ajili ya wasafiri mf.Televisheni za taarifa za habari/Magazeti,Uwepo wa PA system kwa mabasi yanaoingia na kutoka,Huduma za malazi n.k.Nilisikitika nikiona tunapita magofu,vichaka na nusu pori...Nini kiliwakuta watu hawa ?? Hakika hatuwezi yajua yote lakini uwekezaji wao ulikuwa kivutio katika safari ambacho kilitazamiwa na wengi tangu wanapoanza safari.

Kuchimba Dawa - Kwa miaka ya katikati kulikuwa na utaratibu wa mabasi haya kusimama na kuchimba dawa maeneo ya wazi lakini kutokana na kero mbalimbali,Serikali iliweka sheria kudhibiti hili.Kibiashara na kiuchumi wengi tulitarajia vituo hivi hasa maeneo ya karibu kungekuwepo na ubunifu wa kutengeneza huduma za maliwato ambazo zingekidhi viwango na kutoa ajira. Maeneo yote hayo yamebaki na mapango ambayo yameanza au yataanguka muda si mrefu.

Vibao vya Barabarani - Kwa kweli niwashukuru Celtel (iliyokuwa) na Pepsi kwa kuweka vibao vya kuonesha umbali wa maeneo mbalimbali pamoja na mabango maarufu ya "Karibu Mkoa/Wilaya hii" kwani vibao hivi pamoja na kutangaza kampuni zao pia vimekuwa vikitoa taarifa za muhimu hasa umbali kwa wasafiri.Sasa vibao hivi vimechoka..Makampuni wanaojua umuhimu wa kutangaza upcountry business karibuni mjitangaze kwa njia hii nzuri.Ikiwezekana pia zitumike na Serikali za mikoa kama sehemu ya kutangaza vivutio katika wilaya/mkoa husika kwani naamini kila mkoa una megi ya kujivunia kwa Tanzania hii.

Jeshi la Polisi - Hakika nipende kuwapongeza kwa Surveillance nzuri mnayoifanya huku barabarani kwani kila ambapo tulivuka wilaya..checkpoint askari aliingia ndani ya basi na kutusalimia pamoja na kuuliza mwendo wa dereva pia kukagua usalama wa abiria.Kwenye hili Kongole. Lakini pia Uhamiaji hawakuwa nyuma katika kufanya ukaguzi kuhakikisha kila kitu kipo ndani ya sheria.

Hitimisho - Kutokana na kuwa msafiri wa maeneo mbalimbali nimesikitika kuwa ukanda huu ambao zamani ulikuwa juu kwa biashara na ulisifika kwa viwango hivi sasa umekuwa ukidorora maeneo yote.Naonea ukanda huu wivu nikiona mabadiliko aliyoyafanya Shabiby kule kwenye route ya Dodoma na mabasi kadhaa katika route ya Dar - Arusha.

Fursa iliyopo huku ni kubwa hasa ukizingatia tabia na haiba ya wenyeji wa ukanda huu (marafiki zangu Wanyakyusa)...Nina uhakika hata nauli ikiwa Tshs.50,000/- basi hilo litajaa iwapo tu kukiwa na usimamizi na abiria kuhakikishiwa huduma ubora na usafiri salama.

Nachelea kuwaalika kina Shabiby/ ukanda huu LAKINI ni muhimu kuwa na mwekezaji serious atakayerudisha hadhi na kukuza myororo wa thamani (hoteli na maduka) huku akitoa ajira muhimu kwa vijana na wakazi wa maeneo haya.Viongozi tunaomba mchagize katika hili ikiwemo kuwalinda hawa wafanyabiashara wazaliwa/wa nje ili wawe na mazingira rahisi pindi wanapoamua kuleta mitaji yao.

Tanzania yetu..Fahari Yetu !!!

Asanteni.
 
Wakinga mazindiko yao yalieksipaya ndiyo chanzo cha njia hiyo kupwaya, siku hizi wako Dar es Sslaam kwenye biashara ya maduka ya jumla na rejareja.
 
Wakinga mazindiko yao yalieksipaya ndiyo chanzo cha njia hiyo kupwaya, siku hizi wako DSR kwenye biashara ya maduka ya jumla na rejareja.
Waliokuwa wanafanya vizuri siyo wote wakinga mbona...Tumefeli wapi njia hii ??
 
Ila route ya kwetu Dar - Songea, ma bus yako vizuri mno na huduma zake ni bora, ila shida ni sehemu ya chakula (hoteli) comfort, na mafinga mmmh tatizo.
 
Jaribu kupanda saibaba ya saa saba mchana DAR - ARUSHA mkuu, ni kimeo kuliko hata hili la Dar- kyela. kwa upande wa hotel ni kweli kabisa hii njia haina hotel kabisa mkuu hilo halipingiki japo nimeona kilimanjaro anajenga yake naamini itakuwa nzuri...
 
jaribu kupanda saibaba ya saa saba mchana DAR - ARUSHA mkuu, ni kimeo kuliko hata hili la Dar- kyela. kwa upande wa hotel ni kweli kabisa hii njia haina hotel kabisa mkuu hilo halipingiki japo nimeona kilimanjaro anajenga yake naamini itakuwa nzuri...
Hoteli zinachagiza mnoooo...Nawajua ndugu zangu wengi waliokuwa wanapanda Dar Express kwa sababu ya Hoteli ya Highway tu !!
 
Hiyo route hoteli hakuna kabisa zilizopo kwakweli hawazingatii usafi ,

Mpaka unajiuliza hivi uchafu ni sehemu ya mtaji wa biashara.
 
Hiyo route hoteli hakuna kabisa zilizopo kwakweli hawazingatii usafi ,

Mpaka unajiuliza hivi uchafu ni sehemu ya mtaji wa biashara.
Wanaanzaga vizuri halafu hakuna muendelezo.Vyakula wanauza ghali na hakuna usafi/ubora unaoridhisha...
 
Wanaanzaga vizuri halafu hakuna muendelezo.Vyakula wanauza ghali na hakuna usafi/ubora unaoridhisha...
Unakuta nyama imekakamaa kama biskuti aisee, vyakula navyo haviliki, havina ubora kabisa.
 
Zainab (ujio wake wa pili), Scandnavia waliondoka na uzuri wa na ubora wa mabasi pande hiyo...

Waliofuata wote wanajaribu jaribu tu
 
Waliokuwa wanafanya vizuri siyo wote wakinga mbona...Tumefeli wapi njia hii ??
Wakinga matajiri wamehamia Dar wanafanya biashara za mahotel maduka ya jumla na uagizaji bidhaa China na Thailand
 
Hata ukifika huku mbeya napo uchafu naona ni fashion, maana hata chips na wapishi wa mtaani wanauza chakula kichafu Sasa sijui nitabia za wahudumu?
 
Mkuu wewe umeona mabasi tu.

Hakuna uwekezaji wowote toka awamu ya Kikwete hadi hii ya Magufuli katika mikoa tajwa(miaka 20 tunaenda).

Tatizo lazima lisemwe wazi.

Hii ni kutokana na kutaka kumpunguzia umaarufu hasa Mwandosya aliyediriki kugombea urais.

Ukiacha barabara ambazo tusiwe wanafiki zimetengenezwa hasa Mafinga-Igawa, uwekezaji mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini ni kama hakuna.

Mkoani Mbeya barabara bado ni mbovu sana Igawa Tunduma ni mbya na inamaliza maisha ya watu kila siku.#Huko Mawilayani hasa Mbeya kuna kasi ndogo sana ya mendeleo ya kimsingi, barabara.
 
Back
Top Bottom