BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,013
Mabao trafiki Dar yavuna milioni 870/- kwa siku 12
www.ippmedia.com/sw/habari/mabao-trafiki-dar-yavuna-milioni-870-kwa-siku-12
Takwimu hizo zinatokana na taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, kwamba operesheni zilizoendeshwa na kikosi cha usalama barabarani katika kanda hiyo ndizo zilizowagharimu wahusika faini za kiasi hicho cha fedha, kati yake wakiwa ni madereva wenye magari, pikipiki za kawaida na za magurudumu matatu, maarufu kama bajaji.
Kamanda Sirro aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa faini zitokanazo na makosa hayo ni za kuanzia Novemba 21 hadi juzi.
“Idadi ya magari yaliyokamatwa ni 9,817, pikipiki 708, daladala 3,268, magari mengine (binafsi na malori) 6,548. Kwa ujumla makosa tuliyokamata ni 29,289. Wapo pia madereva wa bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa helmet (kofia ngumu) na kupakia mishkaki (abiria zaidi ya mmoja),” alisema.
Aliongeza kuwa ukaguzi wa magari na utoaji wa stika unaendelea katika vituo vya Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na hivyo akawataka wananchi wenye vyombo vya moto kupeleka magari yao kwenye vituo vya polisi ili yakaguliwe.
Wiki mbili zilizopita, kikosi hicho cha usalama barabarani jijini Dar es Salaam kilikusanya zaidi ya Sh. milioni 400 katika operesheni hiyo endelevu iliyodumu kwa wiki moja.