Mabao trafiki Dar yavuna milioni 870/- kwa siku 12

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Mabao trafiki Dar yavuna milioni 870/- kwa siku 12
www.ippmedia.com/sw/habari/mabao-trafiki-dar-yavuna-milioni-870-kwa-siku-12

Takwimu hizo zinatokana na taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, kwamba operesheni zilizoendeshwa na kikosi cha usalama barabarani katika kanda hiyo ndizo zilizowagharimu wahusika faini za kiasi hicho cha fedha, kati yake wakiwa ni madereva wenye magari, pikipiki za kawaida na za magurudumu matatu, maarufu kama bajaji.

Kamanda Sirro aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa faini zitokanazo na makosa hayo ni za kuanzia Novemba 21 hadi juzi.

“Idadi ya magari yaliyokamatwa ni 9,817, pikipiki 708, daladala 3,268, magari mengine (binafsi na malori) 6,548. Kwa ujumla makosa tuliyokamata ni 29,289. Wapo pia madereva wa bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa helmet (kofia ngumu) na kupakia mishkaki (abiria zaidi ya mmoja),” alisema.

Aliongeza kuwa ukaguzi wa magari na utoaji wa stika unaendelea katika vituo vya Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na hivyo akawataka wananchi wenye vyombo vya moto kupeleka magari yao kwenye vituo vya polisi ili yakaguliwe.

Wiki mbili zilizopita, kikosi hicho cha usalama barabarani jijini Dar es Salaam kilikusanya zaidi ya Sh. milioni 400 katika operesheni hiyo endelevu iliyodumu kwa wiki moja.
 
Hivi kweli jeshi la Polisi linafurahia kukusanya pesa kwa makosa ya watu tena makosa yanayo husiana na usalama barabarani!! Hii ni hatari naona wako obsessed na pesa tuu.
 
kha! hilo nalo ni swala LA kujivunia. baada tujivunie Ku export bidhaa tunajisifia kukomoa wananchi
Ndiyo vyanzo vyetu tulivyonavyo, sasa tufanyeje na hali ya kuwa hao hao wananchi wanataka elimu bure, madawa hospitalini n.k.
 
Ni lazima wapongezwe ni hatua nzuri sana cha muhimu watengeneze utalatibu mzuri wa kulipia hizo ticket,
Serikali ya marekani chanzo chake kikubwa cha mapato ni kodi
 
Kumbe vyanzo vya mapato vipo?nasikia zinakuja ndege zingine 2 mwezi wa kwanza na 1 mwezi wa pili....
 
Yani trafic wamekuwa watu wa hovyo sana siku hizi..kubambika kosa hawaoni tabu...dhambi kubwa sana hiyo ya dhuluma...hii pesa ni dhuluma tupu..na hakika ina laana kuna ms.....e mmoja alitaka nimbambikia kosa ila mwenyew aliona aibu baada ya kumshinda ...hela halali ndio ya kujivunia hii hela traffic asilimia 50 ni ya wizi....
 
Mabao trafiki Dar yavuna milioni 870/- kwa siku 12
www.ippmedia.com/sw/habari/mabao-trafiki-dar-yavuna-milioni-870-kwa-siku-12

Takwimu hizo zinatokana na taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, kwamba operesheni zilizoendeshwa na kikosi cha usalama barabarani katika kanda hiyo ndizo zilizowagharimu wahusika faini za kiasi hicho cha fedha, kati yake wakiwa ni madereva wenye magari, pikipiki za kawaida na za magurudumu matatu, maarufu kama bajaji.

Kamanda Sirro aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa faini zitokanazo na makosa hayo ni za kuanzia Novemba 21 hadi juzi.

“Idadi ya magari yaliyokamatwa ni 9,817, pikipiki 708, daladala 3,268, magari mengine (binafsi na malori) 6,548. Kwa ujumla makosa tuliyokamata ni 29,289. Wapo pia madereva wa bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa helmet (kofia ngumu) na kupakia mishkaki (abiria zaidi ya mmoja),” alisema.

Aliongeza kuwa ukaguzi wa magari na utoaji wa stika unaendelea katika vituo vya Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na hivyo akawataka wananchi wenye vyombo vya moto kupeleka magari yao kwenye vituo vya polisi ili yakaguliwe.

Wiki mbili zilizopita, kikosi hicho cha usalama barabarani jijini Dar es Salaam kilikusanya zaidi ya Sh. milioni 400 katika operesheni hiyo endelevu iliyodumu kwa wiki moja.
Kwa haraka inaonekana ni sifa lakini hatulioni tatizo linalojengeka hapa! Siku hizi hakuna kitu tena kinaitwa minor offence, ambalo ni kosa la kuonywa tuu unapigwa notification
Minor offences haziepukiki barabarani lakini ndio hivyo tena
 
Minor offence haingii mfuko wa PRA Mkuu, hiyo ni ya kusafishia buti mkuu na kupata staftahi.

Kwa haraka inaonekana ni sifa lakini hatulioni tatizo linalojengeka hapa! Siku hizi hakuna kitu tena kinaitwa minor offence, ambalo ni kosa la kuonywa tuu unapigwa notification
Minor offences haziepukiki barabarani lakini ndio hivyo tena
 
Fuata sheria uone kama utabambikiwa Kesi. Kwa anayeendesha gari Dar anaelewa kero ya kuchomekewa kwenye foleni. Juzi kati kuna dada alinichomekea mpaka nikaona aibu. Yule dada alikuwa hafananii na kile kitendo. So, Iam fully supportive kwa traffic kupenalize watu tufuate sheria. In any society kodi ndo suluhisho kwa Watu wakorofi. In fact hata ajali za kizembe kizembe zimepungua. Wange extend kodi kwa madereva WA daladala wazembe, wachafu nk. Bila mijeredi punda haendi.
 
Tii sheria bila shuruti. Dar kuna magari mangapi? Kati ya magari yote wamekamata 9000 tu, ni asilimia ndogo sana. Madereva wa Dar wengi wanafanya makosa ya kizembe sana ila siku hizi wameanza kuheshimu sheria.
 
Hivi kweli jeshi la Polisi linafurahia kukusanya pesa kwa makosa ya watu tena makosa yanayo husiana na usalama barabarani!! Hii ni hatari naona wako obsessed na pesa tuu.
Makosa mengi sio ya kihatarisha maisha ni yale kama huna reflective triangle,huna fire extinguisher,umesimama juu ya zebra crossing etc
 
  • Thanks
Reactions: BAK
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom