Mabango ya Mhe. Magufuli Barabarani Yamelipiwa Ushuru Mwaka Mzima?

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,061
Naona maeneo mengi ya nchi mabango yamepamba barabara jambo ambalo limenifanya nijiulize maswali yafuatayo:
1. Je, yalilipiwa ushuru wa muda mrefu licha ya wahusika kutambua kwamba uchaguzi utakuwa wa muda mfupi tu?
2. Je, mabango hayo yaliwekwa bure na kama ndivyo mbona yale ya Lowassa yaliondolewa maeneo mengi ya nchi?
3. Je, ripoti ya CEMOT kwamba CCM walikuwa kinara wa rushwa hususani katika ngazi ya urais. Na ukimya wa vyombo husika kuhusiana na gharama za uchaguzi mkuu 2015 laweza kuwa jipu?
KARIBUNI TUJADILIANE KWA HOJA
 
Hiyo namba 3 ni sahihi kabisa, ktk historia ya Tz hakuna utawala uliokuwa wa magumashi km huuu wa Magu, ndio maana hata mambo yao mengi wanaendesha kimagumashi km utawala wenyewe ulivyopatikana,
 
Magufuli kama ni kinara wa kuhakikisha watu wanalipa kodi, na hili nalo alivalie njuga.
 
January atakuwa aliyalipia, amechota hela ya kutosha kwa muitaliano kupitia mwili wa dadake, so hela haikuwa na uchungu ile unaweza kuta amelipia mpaka kampeni za 2020 yatakaa hapo yakichakaa yanabalishwa tu, chezea pesa ya hongo wewe tena aliehongwa ndio kakupa zawadi.
 
CCM waliiba kura

Alafu wanasema chaguo la mungu. Mwizi anakuwaje chaguo la mungu. Haya umeya jiji la Dar wanataka kutuibia wakati tupo macho wizi kweupe mchana.

Kweli nimeamini magamba wamekubuhu kwa wizi.
 
Naona maeneo mengi ya nchi mabango yamepamba barabara jambo ambalo limenifanya nijiulize maswali yafuatayo:
1. Je, yalilipiwa ushuru wa muda mrefu licha ya wahusika kutambua kwamba uchaguzi utakuwa wa muda mfupi tu?
2. Je, mabango hayo yaliwekwa bure na kama ndivyo mbona yale ya Lowassa yaliondolewa maeneo mengi ya nchi?
3. Je, ripoti ya CEMOT kwamba CCM walikuwa kinara wa rushwa hususani katika ngazi ya urais. Na ukimya wa vyombo husika kuhusiana na gharama za uchaguzi mkuu 2015 laweza kuwa jipu?
KARIBUNI TUJADILIANE KWA HOJA
Yalilipiwa vat? Tunaomba figure kwa aliyokuwa nayo.
 
Hili ni swali la msingi sana. Ni lazima viongozi wa manispaa yaliko mabongo hayo watuonyeshe pesa zilizoingia kutokana na kutundikwa kwa mabango hayo.
 
Back
Top Bottom