Mabalozi mia moja wa CCM Monduli, wahamia CHADEMA

Mabalozi mia moja wa CCM Monduli, wahamia CHADEMA

ketwas

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
212
Reaction score
36
UCHAGUZI 2015: Viongozi CCM Monduli wakiwemo M/kiti Swalehe Ramadhani, Katibu Anna Ernest watangaza kujiunga Chadema leo. Wasema CCM imekiuka kanuni za uchaguzi
Time: 2015-08-13 18:49:16

monduli13.jpg

Mabalozi wa mashina miamoja na kumi wa CCM mwenyekiti katibu kata wajumbe wa kamati ya siasa ya kata pamoja na wenyeviti wa mitaa minne katika kata ya Monduli mjini mkoa Arusha wamehama CCM na kuhamia Chadema.

Tukio ilo limetokea Monduli mjini leo majira ya saa sita mchana wakati viongozi hao walipo kusanyika na kutoa kauli ya kuhama CCM na kuhamia Chadema huku wakieleza sababu zinazo wafanya kufikia maamuzi hayo.

attachment.php

Kwa upande wao wenyeviti wa serikali za mitaa wajumbe wa nyumba kumi na katibu wa CCM kata ya Monduli Anna Erinest wameitaka jamii itambue kuwa hayo ni maamuzi yao binafsi na hayahusiki na shinikizo la mtu yoyote kama inavyo daiwa na baadhi ya watu kila wanaohama udaiwa wameshinikizwa.

Watu wanalinganisha kipindi hiki na kipindi cha Mrema 1995.Ni tofauti sana,kipindi cha Mrema Mwalimu Jk alimpigia debe Mkapa na kama ujuavyo watanzania walikuwa wanamsikia sana Mwalimu,pia Mrema hakufuatwa na viongozi na wanachama wengi wa Ccm maana wengi walimwonea aibu Mwalimu.Ila kipindi hiki cha EL ni tofauti sana,wengi watamfuata (hasa kampeni ikianza)njia za mawasiliano (social media )ni nyingi sana na pia Media Coverage ni kubwa sana kwa EL
 
Aliyekua meya wamanispaa ya Bukoba ndgu Anatory Amani amejiunga na CHADEMA rasmi. Aliyekua waziri wa zamani wa nishati na madini Nazir Karamagi amejiunga na CUF

2. Aliyekuwa mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM, Keko, Peter Mtisi pamoja na makada 100 wa CCM wamejiunga CHADEMA.

3. Mbuge wa Sikonge Said Nkumba avaa gwanda naye.... ukombozi unaendelea
 
Mwaka huu ni zamu ya vijana kuleta mabadiliko kuwa na sisi tunaweza tukiamua
 
Kweli watanzania wamechoshwa na CCM, halafu bado CCM inawaahidi watanzania vitu ambavyo havitatokea kamwe. Kwani walikuwa wapi wasiyafanye ndio wanakumbuka shuka wakati kumekucha? Tutamchagua LOWASSA WA UKAWA ifikapo october kesho kutwa,kwani haya maisha magumu yamesababishwa na SISIEM.
 
Aliyekua meya wamanispaa ya Bukoba ndgu Anatory Amani amejiunga na CHADEMA rasmi. Aliyekua waziri wa zamani wa nishati na madini Nazir Karamagi amejiunga na CUF

2. Aliyekuwa mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM, Keko, Peter Mtisi pamoja na makada 100 wa CCM wamejiunga CHADEMA.

3. Mbuge wa Sikonge Said Nkumba avaa gwanda naye.... ukombozi unaendelea

Huku Arusha CCM+TANESCO tukutane october, CCM wanawatumia TANESCO kufanya hujuma ya kugawa umeme ila tukutane October
 
nawashauri wakina nape na mtoto wa mzee polepole na mtoto wa mzee makonda waanze shikamooo lowasa kama wenzao walivyoanza shikamooo mbowe
 
Aliyekua meya wamanispaa ya Bukoba ndgu Anatory Amani amejiunga na CHADEMA rasmi. Aliyekua waziri wa zamani wa nishati na madini Nazir Karamagi amejiunga na CUF

2. Aliyekuwa mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM, Keko, Peter Mtisi pamoja na makada 100 wa CCM wamejiunga CHADEMA.

3. Mbuge wa Sikonge Said Nkumba avaa gwanda naye.... ukombozi unaendelea

Wanaandika lakini ?
 
Back
Top Bottom