BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,082
Mabalozi kuwekwa kitimoto Zbar
Faraja Mgwabati
HabariLeo; Monday,December 17, 2007 @00:04
SERIKALI itawaweka kitimoto mabalozi wake wote wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje mwezi ujao, kuona kama wametekeleza ipasavyo sera ya Serikali ya Awamu ya Nne ya Diplomasia ya Uchumi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliiambia HabariLeo jana Dar es Salaam kuwa mabalozi wote wataitwa na watakutana katika mkutano utakaofanyika Zanzibar kuanzia Januari 17 hadi 22, mwakani.
Membe alikuwa akizungumza baada ya kurejea kutoka Lisbon, Ureno na Marekani, ambako alihudhuria mikutano ya Umoja wa Ulaya na Afrika na mikutano ya kuitangaza Tanzania kupitia mkutano wa Sullivan unaotarajiwa kufanyika Arusha katikati ya mwaka ujao.
Alisema mkutano huo wa mabalozi utafunguliwa na Rais Jakaya Kikwete na utakuwa chini ya uenyekiti wake, na mabalozi wataulizwa kiasi gani wamesaidia kuitangaza Tanzania na masuala ya uwekezaji.
Alisema mabalozi hao watapimwa, pia namna walivyotumia fedha za balozi, sambamba na utekelezaji wa maagizo ya Rais Kikwete kuhusu kuifanyia kazi ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Tunakutana nao mwezi ujao na tunataka watuambie nini wamefanya na tutawapima kutokana na utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya Uchumi na mambo mengine ya kiutendaji, alisema Membe baada ya kuulizwa balozi gani anafanya vizuri hadi sasa katika kutekeleza sera hiyo.
Alisema mabalozi hao pia wataangaliwa kasoro zao za kiutendaji na kuangalia namna ya kuwasaidia katika kuboresha utendaji wao wa kazi yao. Lakini hakuweza kusema ni hatua gani zitachukuliwa kwa mabalozi ambao wataonekana utendaji wao hauridhishi.
Akizungumzia safari zake za nje, alisema katika mkutano kati ya Afrika na Ulaya (EU) uliofanyika Ureno, mazungumzo yalienda vizuri na nchi za Afrika zilikuwa na sauti moja ya kutetea maslahi ya biashara za Afrika.
Mkutano huo ambao ulifanyika chini ya mpango wa EPA, ulikuwa na lengo la kutafuta ushirika mbadala kati ya mabara hayo mawili baada ya ushirika wa mwanzo ambao uliruhusu nchi za Afrika kuuza bidhaa EU bila ushuru, kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.
Kutokana na kumalizika kwa ushirika huo, nchi za Afrika zitalazimika kulipia ushuru zikipeleka bidhaa zao EU hadi hapo makubaliano mapya yatakapofikiwa.
Kuhusu safari ya Marekani iliyoongozwa na Rais Kikwete, Membe alisema ziara hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa katika kuitangaza Tanzania kupitia mkutano wa Sullivan utakaofanyika mwakani.
Alisema katika mkutano huo, Rais Kikwete alikutana na wafanyabiashara wa Marekani wenye asili ya Afrika na marafiki wengine wa Afrika na kuweza kuitangaza vizuri nchi, hasa ushirikiano katika masuala ya utalii, uwekezaji, ufundi na taaluma.
Tunaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi katika mkutano ujao, wabadilishane uzoefu na kufanya biashara na wenzao wa Marekani, tujivunie mkutano huu kama ni wa kwetu na tufanye maandalizi mazuri, alisema Membe.
Alisema akiwa nchini humo, Rais Kikwete alipewa tuzo ya heshima na Taasisi ya Sullivan kwa utendaji wake mzuri wa kazi na Dk. Asha-Rose Migiro alipewa tuzo kwa mchango wake wa kupigania amani ukanda wa Maziwa Makuu.
Rais pia alipata fursa ya kuzungumza na mabalozi wa nchi za Afrika waliopo Marekani kuhusu umuhimu wa nchi hizo kuhudhuria mkutano huo wa Sullivan. Pia Rais Kikwete alihutubia Chuo cha Global Governance kuhusu umuhimu wa miundombinu katika maendeleo ya Afrika.
Copyright TSN 2006 All Rights Reserved